Mh Mbowe: Bila ya haki hakuna amani

hua anasema hivyo ili kuwafurahisha watu kama nyie msiojielewa ni kama vile tu dumondo anavyotoa singo zake. hakuna jipya toka kwa huyo mtu.
 
hua anasema hivyo ili kuwafurahisha watu kama nyie msiojielewa ni kama vile tu dumondo anavyotoa singo zake. hakuna jipya toka kwa huyo mtu.
Mboe ni nani? Vijana wawe wanaangalia manake kosa kidogo tu umeandika matusi!!
 
It is very very true.

Serikali yetu inahubiri na kuwasihi wananchi wake wadumishe amani wakati serikali hiyo hiyo haizingatii misingi ya kudumisha amani hiyo.

Nitatoa mifano michache ya kuthibitisha ukweli wa kauli hiyo.

1. Wananchi wa jiji la Dar katika uchaguzi mkuu uliopita waliikataa CCM kulitawala jiji hilo kwa kuwachagua madiwani na wabunge wa Ukawa 87 wakati CCM waliambulia madiwani na wabunge 76.

Lakini linapokuja suala la kuchagua Meya wa jiji hilo serikali ya CCM ikitumia vyombo vyake vya dola, haitaki kukubaliana na hesabu hiyo na kukubali kuwa jiji hilo linastahili kuwa na Meya kutoka Ukawa, badala yake chama hicho cha CCM kinafanya figisu figisu za kila aina ili 'kuharamisha' na kudhamiria kumsimika Meya kutoka CCM.

Hivi katika mazingira hao CCM wanategemea wananchi wa jiji la Dar waridhike na upuuzi huo wa kutaka kuwapora haki yao?

2. Mfano wa pili ni kwa yale yanayoendelea huko Zenji ni kuwa dunia nzima inatambua kuwa Jecha 'aliamuriwa' na watawala wa CCM kufuta matokeo yote ya uchaguzi uliofanyika tarehe 25/10/2015 baada ya kubaini kuwa mgombea wao Dr Shein amebwagwa na Maalim Seif na huyo Jecha 'akaamrishwa' tena atangaze marejeo ya uchaguzi huo ambao itakuwa tarehe 20/03/2016.

Hivi katika mazingira hayo watawala wetu wanatumaini kweli amani ya nchi yetu itaendelea kudumu wakati haki ya wananchi waliyoitumia kwenye sanduku la kura wakiipuuza?

Kwa hiyo ni ukweli usiopingika kwa asilimia 100 kuwa watawala wetu hawawezi kuhubiri kwa wananchi wadumishe amani wakati watawala wetu hao hao wanazivunja haki za msingi za wananchi hao kama vile kuingiza mbwa na vikosi vya usalama kwenye jengo la Bunge kule Dodoma kwenda kuwapiga virungu wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi na kuingiza askari wa FFU kwenye ukumbi wa Karimjee wakati wa kufanyika uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar.
 
Katika sakata la kuchagua Meya wa jiji la Dar tumeshuhudia Polisi wakiwasaka kwa nguvu zote na kuwatia mbaroni wabunge na madiwani wa Ukawa, lakini wakati huo huo Polisi hao hao wanashikwa na 'kigugumizi' kumtia mbaroni yuke mama Theresia Mmbando ambaye akikuwa msimamizi wa uchaguzi wa Umeya na ambapo imethibitika pasipo shaka yoyote kuwa zuio la mahakama alilolisoma pale Karimjee wakati wa uchaguzi wa Umeya kumbe lilikuwa feki!

Hivi katika mazingira ya aina hiyo ambapo vyombo vyetu vya usalama vikiwaona baadhi ya wananchi kuwa UNTOUCHABLES na wapo above law na kuliona kundi lingine la wananchi kuwa ndiyo la 'kulibambikia' kesi kila siku, hivi katika mazingira hayo bado watawaka wetu wanaanini kuwa amani na utulivu tulio nao nchini utadumu milele na milele?!
 
Back
Top Bottom