Mh Mbowe awaonya polisi kufanya kazi za uchama

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=3]
2011174328507360_20.jpg
[/h]

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amelionya Jeshi la Polisi akisema haliwezi kuzima vuguvugu la mabadiliko (M4C) nchini kwa kutumia risasi kutisha na kuua wananchi.
Badala yake, amelitaka kufanya shughuli zake kwa utaalamu kwa kuzingatia sheria na kanuni zinazolisimamia na kuepuka kutumiwa kutekeleza matakwa ya watawala wanaowaagiza kuwanyanyasa wapinzani.
Mbowe alitoa onyo hilo juzi wakati akimnadi mgombea wa udiwani wa Kata ya Daraja mbili, Prosper Msofe katika Mtaa wa Jamhuri, ambaye hata hivyo hakuweza kuhudhuria mkutano huo kutokana na kulazwa Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru akipatiwa matibabu ya uti wa mgongo baada ya kushikiliwa na polisi.
Licha ya mgombea huyo kutokuwepo mkutanoni, Mbowe alimtaka kutotishika na tukio lililompata badala yake iwe changamoto ya kuzidi kudai na kupigania haki kwa maslahi ya umma.
“Kama sababu ya CHADEMA kuitwa chama cha vurugu ni kwa kutokana na hatua yetu ya kuwahamasisha watu kudai na kupigania haki zao, basi acha tuendelee kutambulika hivyo,” alisema.
Mbowe alieleza kushangazwa na hatua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kushindwa kutangaza uchaguzi katika kata nne za Jiji la Arusha ambazo zilikuwa zinaongozwa na madiwani waliotimuliwa CHADEMA tangu mwaka jana licha ya juhudi walizofanya kuikumbusha kwa maandishi.
Kata hizo ni Elerai, Kimandolu, Kaloleni, Themi na Sombetini iliyokuwa ikishikiliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia aliyekuwa diwani wake, Alphonce Mawazo, ambaye alijivua gamba kwa kujiunga na CHADEMA.
“Woga wao wanajua nguvu ya CHADEMA kwa sasa, wanaogopa kuona tukishinda viti hivi na kuingiza madiwani sita pamoja na wa viti maalum, idadi ya madiwani wetu itakuwa kubwa, hivyo tutaongoza Halmashauri ya Jiji la Arusha,” alisema.
Akizungumzia utaratibu wa CHADEMA kuwachangisha wanachama wake fedha kwenye mikutano yao kwa ajili ya kuchangia gharama za uendeshaji, alisema kuwa chama kinajengwa na watu wenye fedha safi kama hizo.
Naye Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa wa CHADEMA, Godbless Lema, aliwataka polisi wadogo kutokubali kutumiwa kutekeleza amri za kikandamizaji za viongozi wao kuumiza wananchi kwani mwisho wa siku watakaohukumiwa ni wao.
Alisema kuwa kwenye vurugu za Arusha za Januari 5 mwaka jana, walikufa watu watatu ambapo polisi wa vyeo vya juu ndio walioongezewa vyeo huku wale wa chini wakiambulia patupu.
 
Ila hii serikali yetu imejaa watu walioziba macho yao maana mambo yanayofanyika ni dhahiri inahusoka.kwa kila namna sasa wanampiga mtu wa watu dah
 
Mbowe pambaneni tu kufa na kupona hawa mafisadi wanawaogopa sana ndiyo maana wanatumia polisi. Ningalikuwa polisi ningalipigania haki ya watu na mali zao kwani hao wanaowatumia hawatadumu milele. Akili za kuambiwa changanya na za kwako kwani tunahitaji ukombozi wa kweli.
 
Jamni hi picha inatisha. Ni kwa nini tusiwaue polisi wanapojipitisha huko mitaani? Yaani haya ndiyo wanatendea wapinzani? Watanzania tuko wangapi na polisi wako wangapi? Juzi walimlipua Mwangosi leo haya? Hivi tunafanya nini?
 
Hili angalizo la Mbowe kwa Polisi limetolewa mara ngapi kwenye haya majukwaa ya propaganda? Kama Polisi wangekuwa wanasikiliza si wangesikiliza?
 
Hawa pilisi ni wa kuwaonea huruma sana, kwa sababu wanafanya mambo wasiyoyajua. Polisi ndugu zetu na tunawaelewa wanavyoshindwa kukataa amri za wakubwa wao ambao wameamua kuhudumia watawala kwa makombo ya mafisadi. Wengine tunasali nao na kwa kweli wanajisikia vbaya lakini wafanye nini mbele ya blood thirsty kamanda kama Chagonja, Kamuhanda, Shilogile and the like?
 
Hili angalizo la Mbowe kwa Polisi limetolewa mara ngapi kwenye haya majukwaa ya propaganda? Kama Polisi wangekuwa wanasikiliza si wangesikiliza?

Watasikiaje na masikio hawana? wao wana mitutu tu! Msalimie Kamuhanda..............
 
CHADEMA wanafadhiliwa CDU, Christian Democratic Union ili waeneze ukristo, chama cha kidini hiki. hata makao makuu ukienda pale kuna SANAM ya BIKRA MARIA.
 
CHADEMA wanafadhiliwa CDU, Christian Democratic Union ili waeneze ukristo, chama cha kidini hiki. hata makao makuu ukienda pale kuna SANAM ya BIKRA MARIA.
Ni kweli mkuu halafu wanachama wake wanavaa pekosi na wanakaa sana kwenye vijiwe Wanakunywa gahawa na wanapenda pilau sana na huwa wanapita njiani Huku wakihesabu shanga mikononi
 
CHADEMA wanafadhiliwa CDU, Christian Democratic Union ili waeneze ukristo, chama cha kidini hiki. hata makao makuu ukienda pale kuna SANAM ya BIKRA MARIA.
Endelea kumeza sindano mkuu maana muda si mrefu utaanza kujisaidia haja kubwa ya mitalimbo!
 
Hili angalizo la Mbowe kwa Polisi limetolewa mara ngapi kwenye haya majukwaa ya propaganda? Kama Polisi wangekuwa wanasikiliza si wangesikiliza?

Mwanakijiji hata kama ingekuwa 7x70 kwa siku hatutakiwi kuchoka katika hili kwani kama ni kuhubiliwa binadamu tungehubiliwa mara moja tu.
 
CHADEMA wanafadhiliwa CDU, Christian Democratic Union ili waeneze ukristo, chama cha kidini hiki. hata makao makuu ukienda pale kuna SANAM ya BIKRA MARIA.

Kama huna point si lazima kuchangia. Serikali haina dini iweje chama kiwe cha kidini, serikali isingekisajili.
 
Jamni hi picha inatisha. Ni kwa nini tusiwaue polisi wanapojipitisha huko mitaani? Yaani haya ndiyo wanatendea wapinzani? Watanzania tuko wangapi na polisi wako wangapi? Juzi walimlipua Mwangosi leo haya? Hivi tunafanya nini?

Anza kuua mmoja wewe kwa kutumia nondo au sumu ya panya
 
CHADEMA wanafadhiliwa CDU, Christian Democratic Union ili waeneze ukristo, chama cha kidini hiki. hata makao makuu ukienda pale kuna SANAM ya BIKRA MARIA.

Je CCM na Mkewe CUF wanafadhiliwa na Al-Shabab? Acha kuongea upuuzi
 
CHADEMA wanafadhiliwa CDU, Christian Democratic Union ili waeneze ukristo, chama cha kidini hiki. hata makao makuu ukienda pale kuna SANAM ya BIKRA MARIA.

Duh kama hali ni hii CDM haifai nchi hii aisee, watu wakisema hiki ni chama cha kidini na kikabila wanabisha, haya ushahidi huu
 
Duh kama hali ni hii CDM haifai nchi hii aisee, watu wakisema hiki ni chama cha kidini na kikabila wanabisha, haya ushahidi huu

Kweli tunakazi watanzania!! Huo ushahidi uko wapi? Vp hapo ulipo umepiga pedo na kobasi au? Manake hayo mawazo sio ya kawaida. Mimi ni muislam, ila siwezi shadadia huo udini!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom