NORTHERN ROCK
Senior Member
- May 2, 2012
- 108
- 124
Katika ukurasa wa Yericko amelipoti kwamba:
"Leo nimekutana na kaka mkubwa kamanda wa Anga, Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Kiongozi wa Upinzani Bunge Mh Freeman Mbowe.
Tumezungumza mengi kwa mapana yake, lakini kubwa yakigusa mambo ya kiusalama, siasa na mengineyo... Mh Mwenyekiti ameunga mkono juhudu zangu kwa kukinunua Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, na kusema ni furaha kwake kuona vijana aliowalea na anaoendelea kuwalea kama mimi, wanaonyesha vipawa vyao na kuthubutu.
Mh Mwenyekiti amepongeza hatua yangu ya kuandika kitabu na kulitaja kama tukio la uthubutu. Amesisitiza kwamba vijana tutumie fursa zilizopo hasa kitendo cha kuwapo ndani ya chadema, tuonyesha vipawa vyetu bila woga, na zaidi amesema ili tudumu katika misimamo yetu ya kisiasa, ni vema vijana tukahakikisha tunakuwa na shughuli za kutuingizia vipato halali, hapo hatutarubuniwa na kuhamahama vyama.
Katika eneo lingine katikati ya mazungumzo yetu, Mh Mwenyekiti amesema Chadema na washirika wetu (UKAWA) tunapigana vita vya kisayansi dhidi ya adui yetu CCM, na kwa namna tunavyosonga tumewashinda maadui zetu, 2020 tutashinda kwa kishindo.
Mwisho amenizawadia zawadi maalumu ya kitabu kiitwacho The Spycraft Manual kilichoandikwa na Barry Davies, B.EM
Na Yericko Nyerere"