Mh Maulid Mtulia ndani ya makumbusho

Frey Cosseny

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
1,984
1,405
*MTULIA KUUNGURUMA KATA YA MAKUMBUSHO*

Na Mwandishi Wetu, Kinondoni

Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Maulid Said Mtulia anatarajia kuunguruma leo Jumatano Februari 7, 2018 katika kata viwanja vya Vegas, kata ya Makumbusho.

Huu ni mwendelezo wa mikutano ya kampeni inayoendelea kufanyika kata mbalimbali mgeni rasmi wa leo akitarajiwa kuwa Mhe. Livingstone Lusinde.

Watu wengi sana hujitokeza kwenye mikutano yake ya kampeni. Akizungumza juu ya mikutano hiyo, mkaazi wa Kinondoni Godfrey Baraka amesema Mtulia ameonyesha utofauti na wagombea wenzake kwa kunadi zaidi sera kuliko matusi, kebehi na ushabiki ndio maana mikutano yake hufurika Watu wa kada tofauti tofauti.

"Ukienda kwenye mikutano ya Mtulia utasikia akinadi ilani ya uchaguzi ya CCM. Utasikia Mtulia akieleza namna atajenga miundombinu, ataboresha huduma za kijamii, namna atakavyo wawezesha kiuchumi Vijana na Wanawake. Ni tofauti kabisa na wagombea wengine ambao wao kutwa kutukana, ushabiki na kebehi tu" alisema Godfrey.

Akizungumza juu ya Mkutano wa kampeni wa leo Katibu CCM wilaya ya Kinondoni amewasisitizia wakazi wa Kata ya Makumbusho na viunga vyake pamoja na wakazi wote wa jimbo la Kinondoni kuwahi mapema mkutanoni.

"Nawasisitiza Wanachama CCM na Wananchi wote kwa ujumla kuwahi mapema katika Viwanja vya Vegas Kata ya Makumbusho waje wasikilize kipi Mtulia anawahaidi kuwafanyia, waje wamsikilize mgeni rasmi
Mhe Lusinde almaarufu Kibajaji na sera anazokuja kuwaambia wana Kinondoni." alisema Katibu.

Mkutano wa leo unatarajia kuanza majira ya saa 8 mchana katika viwanja vya Vegas, Kata ya Makumbusho.
 
Mtulia alishaukataa ubunge hatuwezi kumchagua tena.Hasara ya shilingi bilioni moja alizotusababishia kwa kurudia uchaguzi zingeweza kutatua kero nyingi anazoahidi kuzifanyia kazi. Mtulia atafute tu kazi nyingine ya kufanya.
 
Huyo anayesema kuwa mkimpa ubunge, basi vioo vya gari lake vitakuwa wazi wakati wote ili awasalimie wanakinondoni?

Hivi wanakinondoni wataingia maboya ya kumchagua huyo "msaliti"?
 
*YALIYOSEMWA NA MGOMBEA UBUNGE KINONDONI (CCM) MAULID MTULIA KATA YA MAKUMBUSHO LEO TAR. 07/02/2018*

"Mimi ninafanana na nyinyi. Shida zenu ni shida zangu, matatizo yenu ni matatizo yetu" - Mtulia

"Mimi ni Mtoto wa kimaskini, mnapopatwa na matatizo ya mafuriko najua ukubwa wa tatizo." - Mtulia

"Niliguswa na matatizo yenu ya kubomolewa nyumba nikaenda Mahakamani kuzuia bomoabomoa nikafanikiwa." - Mtulia

"Nilipambana kuhakikisha Watu waliobomolewa wanapata hifadhi Magomeni. Nimekuja CCM kuhakikisha hilo linatimia." - Mtulia

"Niliacha Ubunge, Mshahara, posho na kiinua mgongo changu kwa sababu nawajali wana Kinondoni. Ukiwa Kiongozi wa upinzani hauwezi kufanya lolote." - Mtulia

"Maendeleo hayapatikani kwa kutukana, kukashifu, matusi. Maendeleo huja kwa ushirikiano na mahusiano mema" - Mtulia

"Ni kweli nampenda Magufuli. Nitaachaje kumpenda Rais ambaye anajenga reli ya kisasa, kununua ndege za kisasa, ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme. Rais mkweli na muwazi." - Mtulia

"Nitashirikiana na Meya na Mkurugenzi kugawa maeneo ya Mabwepande kwa ajili ya wana Kinondoni waliobomolewa nyumba" - Mtulia

"Mchague Mtulia arudi Bungeni kivingine akiwa Mtekelezaji wa ilani ya uchaguzi inayoongoza dola." - Mtulia

"Nikishinda nitahakikisha Vijana wanakopeshwa Pikipiki na akina Mama wanapewa mikopo ya Biashara" - Mtulia

"Nikishinda nitahakikisha Zahanati ya Makumbusho inajengwa, pesa zipo" - Mtulia

"Nikishinda nitahakikisha kiingilio Hospitali ya Mwananyamala nakifuta, Wananchi wanapata Bima za Afya na Wazee wanapewa huduma bora." - Mtulia

"Nitapunguza mrundikano wa Wagonjwa Hospitali ya Mwananyamala kwa kuhakikisha Hospitali ya Mabwepande inakamilika ili kupunguza foleni, kujenga Maghorofa Hospitali ya Mwananyamala" - Mtulia

"Nikishinda nitahakikisha njia mpya ya usafiri kutoka Makumbusho Mpaka Muhimbili, Makumbusho mpaka Posta" - Mtulia

"Tatizo la taka litakuwa Historia. Nitahakikisha tunajenga kiwanda cha taka pale Mabwepande, pesa zipo" - Mtulia

"Kwa wale Vijana wenye vipaji, nitashirikiana na Msanii Diamond Platnum kuhakikisha tunaunda timu itakayohakikisha inaibua, inakuza na inalinda kazi za Wasanii wa Kinondoni" - Mtulia

"Maji hayatoki mara kwa mara lakini bili inayotoka ni kubwa, nikishinda nitakaa meza moja na Waziri na Dawasco kurekebisha hali hii mbovu iwe historia." - Mtulia

"Nimetoka kule na kujiunga na CCM ili niweze kupata nguvu ya kuwatumikia wakazi wa jimbo la Kinondoni." - Mtulia

"Nawaombeni sana itakapofika Februari 17 mkanipigie kura za ndiyo. Kumchagua Mtulia ni kuchagua maendeleo." - Mtulia
FB_IMG_1518021059320.jpg
FB_IMG_1518021056048.jpg
FB_IMG_1518021095315.jpg
FB_IMG_1518021066705.jpg
FB_IMG_1518021070155.jpg
 
Mijini sio Vijijini.

Mijini watu wameelimika, Wanajua wanahitaji nini.
Kwa mtu mpembuzi wa mambo akiangalia hizo picha vizuri atagundua hao ni misukule waliokusanywa maalumu kwa kazi hiyo.

Hakuna mtu yeyote anayejielewa ambaye anaweza kupoteza muda wake kuja kusikiliza Contents hizo hapo juu.

Msema ukweli mpenzi wa Mungu, Kinondoni ni ya Chadema, Labda tu utokee usanii.
 
Back
Top Bottom