Mh.Makonda hujafa hujaumbika acha kiburi

Euphransia

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
937
778
Nimeshangazwa Na ripoti ya Tume iliyoundwa Na Waziri wa Habari Mh.Nape iliyosema Mkuu wa Mkoa wa DSM Bw.Makonda ameikimbia Tume hiyo Kwa kupita mlango wa nyuma.Nilitegemea Bw.Makonda ni Jasiri kumbe hana lolote .

Kibaya kilichonishtua ni kauli aliyoitoa wakati alipovamia Clouds ya kuwaambia watangazaji atawaweka katika orodha za watuhumiwa wa Dawa za kulevya.Inaonyesha Bw. Makonda anaitumia kampeni ya madawa kukomesha wabaya wake na kujipatia Mali Kwa aliowatuhumu.

Mh Makonda haya ni maisha hata wewe lolote linaweza kukutokea hujafa hujaumbika.
 
Na kamanda kasema waliovamiwa wapeleke taarifa polisi.

Yaani kamanda yeye hajaona wala kusikia habari hii?!

Tutaamini vp polisi kuwa watawashughulikia watuhumiwa inavyotakiwa ikiwa hata habari ya wazi wanasema hawaioni?

Ndipo ninapoamini wengi waliopewa madaraka huchumia tumbo, bila vyeo vyao vya sasa, maisha yao yatakuwa magumu.

Ndiyo maana wanajipofusha.
 
Back
Top Bottom