Mh.MAKINDA: Kwa jina MUNGU sifanyi upendeleo bungeni

kelao

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
8,132
5,785
Akizungumza wakati wa kuahirisha bunge hadi mwezi wa 8,spika wa bunge amesema kwa jina la Mungu hafanyi upendeleo wowote bungeni dhidi ya wabunge wa upinzani.

Amesema waandishi wanaoandika kuwa anapendelea wabunge wa CCM wana matatizo yao na wamwogope Mungu.

my take, Makinda anajisafisha kutokana na dhuluma ya wazi anayowafanyia wapinzani kwa kuzima hoja zao zenye mantiki bungeni.
 
Mungu amsanehe bure, maana hajui atendalo, lakini majibu sahihi atayaona 2015, naye atakuwa upande wa kupigwa tu, kwa jinsi wanavyo tuchosha sasa
 
kwani waandishi wa habari ndo wanaoangalia bunge wananchi si tunajionea wenyewe
 
Bibi Kiroboto amesahau kuwa lile zengwe lake la kukataza bunge lisioneshwe live kwenye luninga lilishindwa hivyo bado anadhani wananchi wanategemea magazeti kupata habari za bunge!!!!
 
Muongo sana yule mama.
Nisaidieni, hivi huwa anasali wapi, inabidi padiri wake akampe malipizi mazito sana kwa kusema uwongo hadharani!
Ina maana Watanzania wote tunaomwona tumekuwa akina PINDA?
 
Enzi za spika Samweli Sitta bunge lilikuwa na hadhi kutokana na uendeshaji mzuri wa bunge. Hata kama mheshimiwa Sitta alipendelea chama chake ilikuwa kwa kificho tofauti na spika Anne Mkinda.Wananchi tunaona na hatuwezi kudanganywa mchana kweupe kwamba eti spika wa sasa hana upendeleo. Upendeleo umekishushia hadhi kiti cha spika.Makinda shtuka sasa!!!
 
Akizungumza wakati wa kuarisha bunge hadi mwezi wa 8,spika wa bunge amesema kwa jina la Mungu hafanyi upendeleo wowote bungeni dhidi ya wabunge wa upinzani.amesema waandishi wanaoandika kuwa anapendelea wabunge wa ccm wana matatizo yao na wamwogope Mungu.my take Makinda anajisafisha kutokana na dhuluma ya wazi anayowafanyia wapinzani kwa kuzima hoja zao zenye mantiki bungeni.

...Angetuambia ni Mungu yupi...kwani wapo mungu wengi....kama alikuwa nanamaanisha Mungu wa Ibrahim, Yacob na Isaka basi hata wenye akili watamzomea.....haihitaji akili kubwa kujua anajaribu kujikosha...kama hapendelei mashitaka?malalamiko ambayo yako mezani kwake tangu 2011 mbona hayajatolewa uamuzi.....Ndugai alivyomtukana Mdee bungeni mbona ulikaa kimya?????........wabunge ambao kila kukicha wanapigwa polisi mbona hujawahi hata wasemea??????mauaji yaliyotekea Arusha mbona hatukusikia unasema pole kwa wafiwa?????

upendeleo wako hata mtoto wa chekechea anauona
 
Akizungumza wakati wa kuahirisha bunge hadi mwezi wa 8,spika wa bunge amesema kwa jina la Mungu hafanyi upendeleo wowote bungeni dhidi ya wabunge wa upinzani.

Amesema waandishi wanaoandika kuwa anapendelea wabunge wa CCM wana matatizo yao na wamwogope Mungu.

my take, Makinda anajisafisha kutokana na dhuluma ya wazi anayowafanyia wapinzani kwa kuzima hoja zao zenye mantiki bungeni.

Historia itamhukumu.
 
Hivi Mungu yupi anayemsema, ni miungu yake ya huko Njombe au Mungu wa Yesu Kristo? Bunge kilikuwa chombo chenye heshima, lakini leo kimekuwa kitu cha karaha na aibu kwa jamii. Sijui ndio Beijing hiyo, au ndio na sisi madem tunaweza. Aibu!
 
Back
Top Bottom