Hakikwanza
JF-Expert Member
- Dec 11, 2010
- 4,034
- 1,003
Mh Makamu wa Rais na mbunge wa jimbo la Ismani kwanza pole na majukumu yenu ya kila siku katika kulijenga taifa letu. Tunaungana moja kwa moja nanyi na serikali yetu katika kulisukuma gurudumu la maendeleo katika taifa hili na utekelezaji wa kauli mbiu ya Mh Rais ya HAPA KAZI TU . Kilio chetu ni huu utekelezaji wa sera ya mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira umekuwa mkali mno na hauja zingatia uhalisia uliopo kwa wakazi waishio pembezoni mwa mto Ruaha (ndogo).
Tumepokea ujumbe toka kwa uongozi wa vijiji vya tarafa ya Pawaga . Taarifa hiyo imesemwa kwa mdomo toka kwa viongozi wa vijiji vyetu inasema:-
-Tunatakiwa kutojihusisha na kilimo cha aina yeyote ile ndani ya mita sitini toka kwenye kingo za mto huu.
-Tunatakiwa kutovuta maji toka mtoni kwa kutumia mashine za kupampu maji.
Wakulima wamelikubali sharti la kwanza la kuachana na kilimo ndani ya mita sitini toka kingo za mto na kulitunza eneo hilo ikiwemo kupanda miti ya kuukinga mto kwa manufaa ya kizazi hiki na kijacho kwa moyo mkunjufu. Ila pendekezo la pili wamelipokea kwa masikitiko makubwa sana, simanzi na huzuni kubwa sana, kwani litaathiri maisha ya kila siku ya watu wote wa bonde hili la Pawaga. Ikumbukwe eneo hili linapata mvua kidogo sana kwa mwaka ambazo kwa kiasi kikubwa huwa hazisaidii kuivisha mazao mengine ukiacha mashamba ya mpunga unaolimwa chini ya mradi wa umwagiliaji.
Hivyo wakulima hulima bustani ndogo ndogo bondeni kwa kutumia mashine za kuvuta maji mtoni kustawisha mbogamboga kama nyanya, vitunguu, hoho, pilipili nk . Mzao haya husaidia kuboresha lishe za wakazi wa Pawaga na kutoa ajira kwa ujumla wake
Hivyo tunaomba swala hili liangaliwe upya kwani litatupa mateso makubwa ikiwepo utapiamulo na magonjwa mengine kwa ukosefu wa matumizi ya mboga mboga na dhana ya kila mtu afanye kazi litakuwa ndoto huku. Pia ajira itakuwa ni tatizo kwani kazi za kufanya zitakuwa hakuna na hivyo kuchochea uhalifu.
Baadhi ya picha za bustani ambazo toka sasa hazitapata maji na hatimaye kukauka na wakulima wake wamekopa mikopo kwa watu binafsi na taasisi za kifedha.
Mmiliki wa hii bustani hadi sasa ni mgonjwa BP ipo juu na ukimwona amejaa simanzi na huzuni kuu sana. Kwani hii bustani ni tegemeo lake kuendesha maisha
Hii ni bustani ya mboga mboga ya mzee mwenye umri miaka 75 ipo hatarini kukauka kutokana na katazo la kutotumia maji ya Ruaha
Hiyo ni mbegu ya vitunguu ambayo imemgharimu mwenye hilo shamba TSH 700,000/= hadi sasa na hatakiwi kuimwagia maji na ipo nje ya mita sitini
Huyu ni mkulima wa nyanya na matikiti mpaka hapo ametumia zaidi ya TSH 800,000/= anatakiwa kuacha kumwagilia hadi hayo mazao yafe