Mh.Magufuli, Zanzibar hakuna mgogoro wa kisiasa.Wajibika usimtafute Seifu wala Shein

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,745
Kwa namna watu wanavyosukumiza unaweza ukaburuzwa kwa kuaminishwa kuwa Zanzibar kuna Mgogoro au mkwamo wa kisiasa ,hilo halipo na sio kweli.

Mheshimiwa sasa hivi huna nguvu ndani ya CCM upo kama mwanachama wa kawaida ,nguvu uliyokuwa nayo ni ile ya kuwa wewe sasa ni Raisi ni cheo kikubwa kuliko cheo cha mwenyekiti wa CCM au chama kingine chochote kile cha siasa.

Kwa hio amri ipo mikononi mwako kama utasema Sheni au Seifu atangazwe hakuna wa kukupinga zaidi ya kusikika makelele na kelele za milango.

Ukweli unaujua na unajulikana kama uchaguzi wa Zanzibar ulifanyika na mshindi kujulikana hilo hakuna asie jua na kadiri siku zinavyoenda ukweli unazidi kuja juu,

Kubwa ambalo unaweza kulifanya kwanza ni kumtaka Jecha Salum Jecha afute kauli yake hadharani kwa kutumia vyombo vya habari ili kuitengua kauli ya kufuta uchaguzi uamuzi ambao aliutoa yeye kama yeye na hakuwashirikisha washiriki wahusika wa tume katika uamuzi wake huo'

Itabidi umuweke Jecha kiti moto akupe ukweli ili uamuzi wako uwe wa uhakika juu ya kilichomtokea Jecha na makamo wake,jambo ambalo lilishuhudiwa.

la tatu ambalo linaweza kuwa la kwanza ,wewe sasa ni Jemedari wa majeshi yote ,ili kupata uhakika ,toa amri upate uhakika wa wale waliomteka makamo wa mwenyekiti wa tume ambao walivalia sare za JWTZ ,walifanya hayo kwa amri ya nani na kwa nini ?
Huna haja ya kuwa na Seifu wala Sheni wala kukutana nao ,uwezo unao na sababu unazo ,moja ya kuwa wao wameshindwa kufahamiana na doa wala matatizo hayawakuti wao utakutana nayo na kukupunguza kasi yako katika anga za kimataifa.

Mbona unamaliza kazi ndani ya siku tatu na njia yako kusafika.
 
Umeshauri vyema,ila si unajua heshima ya ushauri aweza tumia ama akauacha,ila nia yako njema japo yaweza kuwa ndefu
 
Tatizo hapo ni CCM na kumbuka mheshimiwa nae ana upande kwenye hiyo kesi anayotakiwa kuiamua ambayo napo akienda vibaya inaweza kumrudia na kuibua mengine tuliyoanza kuyasahau.
 
Shida kubwa ya mgogoro wa Zanzibar inajulikana; Unaposema taifa la Tanzania una maana ya ccm na unaposema ccm una maana ya Tanzania; hadi mawazo haya ya kipumbavu yatakapotoka vichwani mwa baadhi ya watu ndipo huo mgogoro utaisha. Ninachokiona hapa kwenye hu mgogoro ili rais autatue vizuri itategemea na msimamo wa rais wa awamu ya tatu ukoje!?
 
Jamani hivi hii dhuruma ya wazi ya wazanzibari itapatiwa ufumbuzi lini?, mweeee
 
Hiki ni kipimo cha UTANZANIA na kipimo kwa viongozi waadilifu ,tusisikie mtu kapewa tuzo ya kimataifa ni kuvuka kwenye mitihani kama hii na hapa hapana mgogoro hilo sikubaliani nalo ,sasa tumekuwa kama hatuna kazi ya kufanya ,wachache wanataka kuvunja kasi ya mabadiliko ,akili ya mjinga gani itakubali kuwa jecha amefuta uchaguzi kwa sababu za msingi ambazo zilitokea,sababu zisizo na ushahidi ,something fishy ,Nyerere alisema hataita wapumbavu atatumia mjinga ,kuna wajinga wachache ambao haijulikani hata wanategemea kuendesha vipi serikali isiyotambulika kimataifa ,ni wazi kabisa serikali ya CCM Zanzibar itakosa utambuzi kimataifa hata wakiitisha uchaguzi bado serikali ya ccm ikiibuka mshindi kama wanavyokubalisha basi msimamo wa kutoisaidia serikali hio hautabadilika ,hilo walijue ,kwa maana hio wategemee kuendesha serikali yao kwa kuuza mbata.
 
Tatizo lako wazanzibari ni kutokuona mbali. Magufuli Kamwe hawezi kwenda kinyume na malengo na matarajio ya CCM ambacho ni chama chake. Musisahau UVCCM kutoka Zanzibar basi walimpiga tafu sana Magufuli wakati wa uchaguzi ambao ni wao wanaotaka uchaguzi urejewe ili washinde kwa wizi na hila. Sasa leo iweje Magufuli aweze kwenda kinyume na matarajio ya CCM ya kurejea uchaguzi. Tusidanganyane Magufuli hana Tofauti yoyote na Makapa ama Kikwete. Tundu Lissu aliwahi kusema ya kwamba huyu jamaa hakuna cha mtu wa Mungu wala nini .Magufuli ni sawa na Kaisari kwa suala la Zenji. Mwaka 2001 Mkapa alipeleka askari na kuua watu kule Pemba na Mwaka huuu tusubiri muone ni yeye Magufuli ndie atakaye peleka Jeshi na kuua Raia huko.
 
CCM wakisema wewe ni mwanamke ghafla unakuwa mwanamke. Kama huamini basi. Wewe sikiliza serikali ya CCM inachosema na ndo ufate hicho. Achana na hayo mawazo yenu huko ya kutiana moyo n.k. mi nlishagundua hilo siku hizi wala sina presha. Kama kuna jambo linazungumzwa siulizi hata katiba inasemaje. Nauliza tu ccm wanasemaje au wanatakaje? Sasa wamesema UCHAGUZI UNARUDIWA....basi utarudiwa. Watu watalialia na kuhangaika kama kuku anayetaka kutaga na mwisho itakuwa like wat they said. Una swali? Uliza.
 
Kwa namna watu wanavyosukumiza unaweza ukaburuzwa kwa kuaminishwa kuwa Zanzibar kuna Mgogoro au mkwamo wa kisiasa ,hilo halipo na sio kweli.

Mheshimiwa sasa hivi huna nguvu ndani ya CCM upo kama mwanachama wa kawaida ,nguvu uliyokuwa nayo ni ile ya kuwa wewe sasa ni Raisi ni cheo kikubwa kuliko cheo cha mwenyekiti wa CCM au chama kingine chochote kile cha siasa.

Kwa hio amri ipo mikononi mwako kama utasema Sheni au Seifu atangazwe hakuna wa kukupinga zaidi ya kusikika makelele na kelele za milango.

Ukweli unaujua na unajulikana kama uchaguzi wa Zanzibar ulifanyika na mshindi kujulikana hilo hakuna asie jua na kadiri siku zinavyoenda ukweli unazidi kuja juu,

Kubwa ambalo unaweza kulifanya kwanza ni kumtaka Jecha Salum Jecha afute kauli yake hadharani kwa kutumia vyombo vya habari ili kuitengua kauli ya kufuta uchaguzi uamuzi ambao aliutoa yeye kama yeye na hakuwashirikisha washiriki wahusika wa tume katika uamuzi wake huo'

Itabidi umuweke Jecha kiti moto akupe ukweli ili uamuzi wako uwe wa uhakika juu ya kilichomtokea Jecha na makamo wake,jambo ambalo lilishuhudiwa.

la tatu ambalo linaweza kuwa la kwanza ,wewe sasa ni Jemedari wa majeshi yote ,ili kupata uhakika ,toa amri upate uhakika wa wale waliomteka makamo wa mwenyekiti wa tume ambao walivalia sare za JWTZ ,walifanya hayo kwa amri ya nani na kwa nini ?
Huna haja ya kuwa na Seifu wala Sheni wala kukutana nao ,uwezo unao na sababu unazo ,moja ya kuwa wao wameshindwa kufahamiana na doa wala matatizo hayawakuti wao utakutana nayo na kukupunguza kasi yako katika anga za kimataifa.

Mbona unamaliza kazi ndani ya siku tatu na njia yako kusafika.
tayari seif keshawashitaki vatcan. kwa hiyo usijali.
 
Mgogoro wa Zanzibar hautatuliki kwa amani kwa kuitumia katiba iliopo ya mfumo wa serikali mbili. Muungano wetu umepigiwa upatu kuwa ni wa kuigwa duniani, wakati ukweli ni tanuru la mkaa ambalo limekuwa likihadaa wapita njia wakiona moshi wasijue kinachoendelea ndani. Imetumika nguvu kubwa sana kulinda mfumo huu. Muunngano unahitajika kwani umoja ni nguvu. Kuendelea nao kwa mfumo huu kesho itatugharimu sana.
 
Tatizo lako wazanzibari ni kutokuona mbali. Magufuli Kamwe hawezi kwenda kinyume na malengo na matarajio ya CCM ambacho ni chama chake. Musisahau UVCCM kutoka Zanzibar basi walimpiga tafu sana Magufuli wakati wa uchaguzi ambao ni wao wanaotaka uchaguzi urejewe ili washinde kwa wizi na hila. Sasa leo iweje Magufuli aweze kwenda kinyume na matarajio ya CCM ya kurejea uchaguzi. Tusidanganyane Magufuli hana Tofauti yoyote na Makapa ama Kikwete. Tundu Lissu aliwahi kusema ya kwamba huyu jamaa hakuna cha mtu wa Mungu wala nini .Magufuli ni sawa na Kaisari kwa suala la Zenji. Mwaka 2001 Mkapa alipeleka askari na kuua watu kule Pemba na Mwaka huuu tusubiri muone ni yeye Magufuli ndie atakaye peleka Jeshi na kuua Raia huko.
Uvccm haikufanikiwa kumsaidia magufuli kwenye kura za urais huku zanzibar,imemuangusha na itendelea kumuangusha kama ataendelea kuwasujudia,tukirudi kwenye hoja tanganyika ndio inayoamua mustakbali wa siasa za zanzibar tokea 1964 hii maana yake tanganyika inaikoloni zanzibar kwa kupitia koti la muungano na ndio ukaona jwtz walifika pale bwawani panapotangazwa matokeo wakaondoka nae mwenyekit wa tume.
 
Back
Top Bottom