Mh. Magufuli itendee haki nchi hii - Kunatakikana Katiba Mpya

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,227
35,151
Mheshimiwa Magufuli wakati umekuwa kinara wa kuwataka wananchi wote kuweka maslahi ya Tanzania mbele hebu itendee haki nchi hii kwa kuweka maslahi yake mbele na kufanikisha mchakato wa katiba mpya.

Mheshimiwa uko katika nafasi ambayo ungeweza kuifanya nchi hii mahali pazuri pa kuishi kuliko wakati wowote ule. Utakumbuka kuwa walikuwapo wengi wakiwamo wengine ambao leo hawako tena nasi hapa duniani na wengine hawako katika nafasi tena katika nafasi adimu hizi za maamuzi ambapo wangeweka maslahi ya nchi mbele hawakufanya hivyo na leo hii majuto ni mjukuu.

Mheshimiwa rejesha wito wako kwa Watanzania kwako wewe mwenyewe. Hebu weka maslahi ya Tanzania mbele kuipatia nchi hii katiba mpya inayokubalika na wananchi walio wengi. Hii itakuwa msingi imara wa kupambana kwa mafanikio katika vita vyako vyote unazojaribu kupigana kwa niaba ya nchi hii.

Mheshimiwa tupe raha sisi wananchi wako kujivunia nchi yetu kama Kenya majirani zetu wanavyojivunia nchi yao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom