MH. MAGUFULI, HIKI NI KIINI CHA SHIDA, UOZO (MAJIPU) TANZANIA.

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Mh. Rais Najua Una Kazi Nyingi, Na Pia Nina Imami kuwa Wewe Unauwezo wa Kufikiri Hivyo Sita poteza Muda wako Mwingi Kusema haya.

Kiini Cha Matatizo au Unayoyaita Majipu ya Tanzani hasa Ni Hiki.

1) Uhuni na Mizengwe ya Chama Chako cha Mapinduzi, CCM, Kuhakikisha mnachukua Madaraka Muhimu Nchini Iwe wananchi wamewachagua au la.
2) Pamoja na Kuwepo Viongozi wachache Katika CCM wanaotia Moyo Kama wewe, Wengi walilindwa na Bado wanalidwa.
3) Ukandamizaji wa Demokrasia Kiwaziwazi.
4) Ukiukaji wa Uhuru na Haki za Binaadamu.
5) Madaraka yanayopatikana kwa Njia za hadaa na Njia za Mikato.
6) Unyanyasaji wa wanasiasa wa Upinzani kwa Kutumia Dola.
Mifumo na Viongozi wapatikanao Katika Mazingira Niliyoyataja, Wanakuwa na dhana kwamba Lolote wafanyalo hakuna wa wakuwawajibisha. Hivyo Wanafanya Watakavyo. Na Ndio chanzo cha Madudu Uliyoyakuta.

Unachonishangaza, Umekiwa Kinara, Pengine Kwa Nia Nzuri au Dangaya toto, Nataka Niamini Ni kwa Nia Nzuri, Umekuwa Kinara wa Kupambana na Matunda ya Mizizi Niliyoitaja. Huku Mizizi na Mashina yanayozaa Matunda hayo Ukiyalea, tena Kwa Kutumia hata Jeshi na Polisi.

Nakushangaa sana, Nakushangaa sana, Unafoka wamama Kulala chini Muhimbili, Nadhani Unawapenda wamama hawa, najua Unawaheshimu wamama hawa, Mbona Huheshimu Kura zao hawa wamama walipoamua Ukawa wawe na Mameya Wengi na Wabunge wengi Dar.

Katika Kampeni Ulikuwa Ukisema, "CUF wangu, CHADEMA wangu, NCCR Wangu" Mbona Unakubali CUF wanadhulimiwa Zanzibar, Mbona Unatuma Polisi Kufanya Mizengwe Uchaguzi wa Meya Dar es salaam. Kama sio wewe Uliowatuma, Waambie WAKOME! Waambie Na CCM wakome Uhuni wao.

Vinginevyo, Unajihujumu Vibaya sana Wewe Mwenyewe Binafsi na Kikwete na Mkapa wanaokushinikiza wanakuhujumu sana. Mbona watu wanawakatalia Baba zao Vitu Vingine? Mwambie Kikwete na Mkapa No! Nawaheshimu Wazee lakini kwa haya No, No!

Huu Uhuni wa Umeya wa Dar es salaam Ni Wa wazi wa Aibu, Na likitokea lolote baya, na Niseme it will only getting more uglier Wote hawa, Watakuja kukuruka, hasa Kikwete Ni Mnafiki sana.

NI AIBU SANA, NI UONEVU SANA, HOW CAN YOU SLEEP AT NIGHT MR. PRESIDENT.
 
Wengi wetu tunaamini kuwa Magufuli anatumbua majipu, Kutokana na kufukuzwa wachache kwenye uongozi. Lakini majipu makubwa Tanzania ni Mkapa na Kikwete ndio waliojirisisha mali za Watanzania na hao ndio waliomuweka huyo Magufuli. Hivi kweli Magufuli anao uwezo wa kuyatumbua yaha majipu yaliomuweka hapo alipo? Huyu jamaa hayupo kwa kuleta maendeleo ila kaekwa hapo kwa lengo la kukaza buti tu. Kikwete alikuwa yupo too soft kwa wapinzani ndio kaletwa hapa kazi tu ya kuwashuhulikia wapinzani na waleta fyokofyoko.
 
jipu kubwa na sugu hapa tanzania ni ccm yenyewe. maghufuli hana ujanja wa kulitumbua kamwe...
 
Back
Top Bottom