Mh Magufuli Fuatilia Pia Ajira za Upendeleo katika Mashirika ya Umma

lubajaro

JF-Expert Member
Mar 29, 2015
1,255
364
Poleni na Majukumu ya leo wana JF.
Hivi karibuni ilitolewa tangazo na serikali juu ya kuhakiki ajira za watumishi wa umma na wale wa mashirika ya umma ili kubaini watumishi hewa na wale wasio na vyeti vya taaluma lakini wakaajiriwa na serikali au katika mashirika ya umma pasipo kuzingatia taaluma zao walizosomea. Mfano:~ Mhasibu kuajiriwa kama HR katika serikali au katika shirika la umma.

Pia, hivi karibuni tumeshuhudia kusimamishwa kazi kwa wakurugenzi wa mashirika ya umma kama vile NSSF na NHIF. Ili kupisha uchunguzi na ikiwezekana ajira zao kuweza kutangazwa upya na vile vile hawa waliosimamishwa kazi kuweza ku apply upya katika nafasi hizo.

Ombi langu kwa Rais Mh Magufufuli ambaye ndiye Mwajiri Mkuu kwa watumishi wote wa serikalini na mashirika ya umma, kwamba aweze kutatua kero ya baadhi ya mashirika ya umma kama vile NSSF, PSPF, NHIF, PPF, LAPF, NHC, BoT, GEPF, n.k. ambao kipindi cha miaka ya nyuma walikuwa wanaajiri watumishi wa kada za chini kama vile Principal Officers, Senior Officers, Officers I & II, n.k. kwa upendeleo, kuweza kutoa Government Notice (GN) kusitisha ajira zote za kada hizo katika mashirika yote ya umma hususani hayo yaliyotajwa hapo juu, na ajira hizo kutangazwa upya na watanzania wote hata kwa wale watoto wasiokuwa na network kuweza kufanya application katika ajira hizo na kuwepo na independent board ya kuajiri watumishi wa umma kama ilivyo kwa ile sekretarieti ya serikali ya kuajiri watumishi wa serikali kuu na mitaa, pamoja na wakala za serikali na vyuo vya umma.

Hii itasaidia sana kuondoa manung`uniko kwa watoto wa masikini wenye uwezo mkubwa wa kiakili na utendaji wa kazi na wao pia kuweza kupata ajira katika haya mashirika ya umma na hii itapelekea ufanisi kuongeza katika kuendesha mashirika haya ya umma, kwa maana ajira za upendeleo zimewaacha watoto wa masikini kutupwa nje katika mashirika haya ambayo ya umma.

Katika mashirika haya ya umma, kuna wakurugenzi wa utumishi na utawala wameshatengeneza syndicate yao kwamba ajira zao katika mashirika haya hutolewa kwa vimemo tena mpaka DG akubali kupitisha ajira hizo kwa hao watoto wa vigogo hususani NHC, NSSF, PSPF, GEPF, PPF, LAPF, n.k.

Nawasilisha
 
Ushauri wa giza. Kama kuna walioajiriwa kwa upendeleo na ushahidi upo watolewe taarifa na sio kwa ujumla
 
Hivi umekunywa viroba vya wapi? Au na wewe utakuwa muathirika wa jambo hili? Na ndiyo maana ufanisi katika mashirika haya umeshuka sana
 
Poleni na Majukumu ya leo wana JF.
Hivi karibuni ilitolewa tangazo na serikali juu ya kuhakiki ajira za watumishi wa umma na wale wa mashirika ya umma ili kubaini watumishi hewa na wale wasio na vyeti vya taaluma lakini wakaajiriwa na serikali au katika mashirika ya umma pasipo kuzingatia taaluma zao walizosomea. Mfano:~ Mhasibu kuajiriwa kama HR katika serikali au katika shirika la umma.

Pia, hivi karibuni tumeshuhudia kusimamishwa kazi kwa wakurugenzi wa mashirika ya umma kama vile NSSF na NHIF. Ili kupisha uchunguzi na ikiwezekana ajira zao kuweza kutangazwa upya na vile vile hawa waliosimamishwa kazi kuweza ku apply upya katika nafasi hizo.

Ombi langu kwa Rais Mh Magufufuli ambaye ndiye Mwajiri Mkuu kwa watumishi wote wa serikalini na mashirika ya umma, kwamba aweze kutatua kero ya baadhi ya mashirika ya umma kama vile NSSF, PSPF, NHIF, PPF, LAPF, NHC, BoT, GEPF, n.k. ambao kipindi cha miaka ya nyuma walikuwa wanaajiri watumishi wa kada za chini kama vile Principal Officers, Senior Officers, Officers I & II, n.k. kwa upendeleo, kuweza kutoa Government Notice (GN) kusitisha ajira zote za kada hizo katika mashirika yote ya umma hususani hayo yaliyotajwa hapo juu, na ajira hizo kutangazwa upya na watanzania wote hata kwa wale watoto wasiokuwa na network kuweza kufanya application katika ajira hizo na kuwepo na independent board ya kuajiri watumishi wa umma kama ilivyo kwa ile sekretarieti ya serikali ya kuajiri watumishi wa serikali kuu na mitaa, pamoja na wakala za serikali na vyuo vya umma.

Hii itasaidia sana kuondoa manung`uniko kwa watoto wa masikini wenye uwezo mkubwa wa kiakili na utendaji wa kazi na wao pia kuweza kupata ajira katika haya mashirika ya umma na hii itapelekea ufanisi kuongeza katika kuendesha mashirika haya ya umma, kwa maana ajira za upendeleo zimewaacha watoto wa masikini kutupwa nje katika mashirika haya ambayo ya umma.

Katika mashirika haya ya umma, kuna wakurugenzi wa utumishi na utawala wameshatengeneza syndicate yao kwamba ajira zao katika mashirika haya hutolewa kwa vimemo tena mpaka DG akubali kupitisha ajira hizo kwa hao watoto wa vigogo hususani NHC, NSSF, PSPF, GEPF, PPF, LAPF, n.k.

Nawasilisha
ASANTE SANA KWA HOJA ZAKO KUMBE UMELIONA HILO,NDUGU YANGU IZO TAASISI ZILIFANYA JUU CHINI ZISIPELEKE AJIRA TUME YA AJILA ILI WAENDELEA KUWEKA NDUGU ZAO NA JAMA ZAO,MARA NYINGI WATOTO WA MASKINI WANAPATA AJIRA KUPITIA TUME YA AJIRA,TASISI IZO ULIZOZITAJA INGAWA UMESAHAU TANAPA NA BANDARI ZETU N.K NI UNDUGULARIZATION MTUPU SENSA INGEPITA WAKINA NIMEPATA KWASABABU YA SHANGAZI,MJOMBA,KAKA N.K. NI WENGI SANA MPAKA SASA NITASISI ZA WATU FLANI WEWE MWENZANGU MFUGA NG'OMBE PALE HUPATI SUBIRI TUME YA AJIRA ITANGAZE UKASHINDANISHWE UKIFAULU USAILI UTAPATA.
 
Mh Rais Magufuli anatakiwa aliangalie hili, hili pia ni jipu la kutumbua...!

Sent from my HUAWEI Y330-U11 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom