Mh. Lukuvi analipwa na Pay roll Ipi? Ubunge, Ukuu wa Mkoa au Waziri wa Nchi TAMISEMI?

Ta Muganyizi

R I P
Oct 19, 2010
5,361
2,734
Katika hali ambayo mie siielewi ni ile ya mtu mmoja kuwa na madaraka nyeti kana kwamba yeye pekee ndo kaenda shule. Au ndo tuseme serikali inabana matumizi kwa kumneemesha mmoja tu alafu wengine wabaki bila kazi? Yeye ni mbunge kule kwao kusini, bado ni mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, bado ni waziri wa nchi Sera na Bunge why! Sasa mie ninachojua ni kuwa kwa vyeo hivi kila cheo unapewa dreva na gari. Kwa Ukuu wa Mkoa na Uwaziri Ulinzi unakuwepo. Sasa yeye ana magari mangapi ya Serikali, dreva wangapi na walinzi wangapi na ni kwa busara zipi alizonazo huyu bwana mpaka mtu mmoja afanye shughuli tatu alone? Ufanisi upo kweli hapo. Wanaojua nisaidieni Mtanzania mwenzenu.
 
hapo ndo sielewagi, hivi maana nzima ya kufanya hivi ni nini? ifikie muda tukatae haya mambo nna katika mpya ihighlight haya
 
Ukuu wa mkoa ameshakabidhi ofisi kwa msaidizi wake, kwasasa yeye ni waziri hivyo anatumia prifeleji za uwaziri, kwa ubunge mawaziri wote ni wabunge na wabunge hawapewi madereva bali hukopeshwa magari kama sijakosea
 
Katika hali ambayo mie siielewi ni ile ya mtu mmoja kuwa na madaraka nyeti kana kwamba yeye pekee ndo kaenda shule. Au ndo tuseme serikali inabana matumizi kwa kumneemesha mmoja tu alafu wengine wabaki bila kazi? Yeye ni mbunge kule kwao kusini, bado ni mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, bado ni waziri wa nchi TAMISEMI! Sasa mie ninachojua ni kuwa kwa vyeo hivi kila cheo unapewa dreva na gari. Kwa Ukuu wa Mkoa na Uwaziri Ulinzi unakuwepo. Sasa yeye ana magari mangapi ya Serikali, dreva wangapi na walinzi wangapi na ni kwa busara zipi alizonazo huyu bwana mpaka mtu mmoja afanye shughuli tatu alone? Ufanisi upo kweli hapo. Wanaojua nisaidieni Mtanzania mwenzenu.

Nafikiri ukuu wa mkoa ameshakaimisha permanently, Yeye anabaki na posho za ubunge na Uwaziri wake (PMO's Sera na Bunge) siyo TAMISEMI. Hata hivyo nafikiri katiba mpya itabidi izungumzie suala la waziri kuwa mbunge, au Mkuu mkoa kuwa Mbunge. Mfano mkuu wa mkoa wa Mwanza, ni mbunge kule iringa sijui anajigawa vipi
 
Mbunge akisha kuwa waziri halipwi tena kama mbunge analipwa kama waziri kwavile kuna mfumo wa kuwalipa mawaziri pia anapata mafao yake kama waziri kwa kipindi ambacho atakuwa ametumikia nafasi hiyo. Ukuu wa mkoa ni cheo cha kisiasa kama hajakabidhi ofisi hiyo kwa mtu mwingine kukaimu basi na huko atakuwa analipwa. Pia ukumbuke wapo wabunge ambao wilikuwa wakuu wa mikoa nao walikuwa wanachukua kotekote. Ni mfumo mbaya sana wa kiutendaji kwani mtu anaweza kuutumia mwanya huo kwa maslahi binafsi au maslahi ya kikundi flani, lazima haya mambo yawekwe bayani kwenye katiba mpya.
 
Nyie acheni tu, hii nchi nadhani kua watu wanadhani ni ya kwao pekee na cc wengine tumepanga tu!
 
Kwa maana hiyo mkuu wa mkoa wa Dar ni nani? Jamaa badala ya kuhakikisha kuna watendaji nchini, anaenda kuzungumzia ya wengine huko ivory coast, kwake kumeozaaaaaa.
 
Huko tuendako sitashangaa hata mlinzi na yeye akawa na mlinzi wake na dereva na yeye akawa na dereva wake.... full ulaji kwa wachache.
 
Ufisadi tu kila kona yaani sijui mpaka dr Slaa aingie ikulu ndio nchi hii itakua nzuri
 
waziri wa TAMISEMI ni mkuchika banaa
Katika hali ambayo mie siielewi ni ile ya mtu mmoja kuwa na madaraka nyeti kana kwamba yeye pekee ndo kaenda shule. Au ndo tuseme serikali inabana matumizi kwa kumneemesha mmoja tu alafu wengine wabaki bila kazi? Yeye ni mbunge kule kwao kusini, bado ni mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, bado ni waziri wa nchi TAMISEMI! Sasa mie ninachojua ni kuwa kwa vyeo hivi kila cheo unapewa dreva na gari. Kwa Ukuu wa Mkoa na Uwaziri Ulinzi unakuwepo. Sasa yeye ana magari mangapi ya Serikali, dreva wangapi na walinzi wangapi na ni kwa busara zipi alizonazo huyu bwana mpaka mtu mmoja afanye shughuli tatu alone? Ufanisi upo kweli hapo. Wanaojua nisaidieni Mtanzania mwenzenu.
 
waziri wa TAMISEMI ni mkuchika banaa

ok kaka ni sera na Bunge, hata kama bana, kwa nini yeye vyote tuu. Kakabidhi lini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar, Umesikia huyo kaimu akisema chochote kuhusu Dar? Rais anaacha kushughulikia mambo muhimu fasta anapiga miseleeeee. AGGGh
 
Back
Top Bottom