Mh. Lissu na Mgongano wa Katiba ya JMT na Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Lissu na Mgongano wa Katiba ya JMT na Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mambomengi, Nov 17, 2011.

 1. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Muungano wetu hauwezi kuokolewa kwa maneno matamu kama 'Muungano ni lulu', etc. tu. Muungano huu umekuwa na matatizo makubwa ya kimsingi kwa miaka yote ya uhai wake. Kujifanya matatizo haya hayapo ni
  kuchopeka vichwa vyetu kwenye mchanga kama mbuni na kutokuyatafutia ufumbuzi. Hii ndio hatari kubwa zaidi kwa Muungano kuliko 'wapigania uhuru' wa Zanzibar kama ZARFA au wanaotaka Tangayika ifufuke kama sisi wanaCHADEMA. Napendekeza msome hotuba yangu Bungeni juzi juu ya nafasi ya Zanzibar kama bado hamjaipata. (Bofya hapa kupakua nakala)

  Kwa wanaopenda kuangalia the ugly truth on its face, napenda kuwaomba mtafakari mambo yafuatayo ambayo yametokana na Muafaka wa CCM na CUF Zanzibar na kuzaliwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Haya, kwa maoni yangu, yame-sound the death knell ya Muungano wetu lakini hakuna mtu yeyote kati ya machampioni wa Muungano mwenye kudiriki kuyasema hadharani:

  1) Ibara ya 1 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inatamka wazi kwamba "Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano." Ibara ya 2 ya Katiba ya Zanzibar inatamka wazi kuwa "Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."

  2) Ibara ya 2(2) ya Katiba ya Muungano inampa madaraka Rais wa Muungano "... kuigawa Jamhuri ya muungano katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo...." Hata hivyo, kabla hajaigawa Zanzibar katika mikoa, "... atashauriana kwanza na Rais wa Zanzibar...." Ibara ya 2A ya Katiba ya Zanzibar inampa Rais wa Zanzibar madaraka ya "... kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo...."

  3) Ibara ya 33(2) ya Katiba ya Muungano inatamka wazi kwamba Rais wa Muungano ni "Mkuu wa Nchi" (ya Tanzania?) Ibara ya 26(1) ya Katiba ya Zanzibar inatamka wazi kwamba Rais wa Zanzibar "ni Mkuu wa Nchi ya Zanzibar...."

  4) Ibara ya 4(3) ya Katiba ya Muungano ikisomwa pamoja na Ibara ya 147(2) na vifungu vya 3, 4 na 7 vya Nyongeza ya Kwanza inaipa Serikali ya Muungano mamlaka ya ulinzi na usalama, polisi na uhamiaji na uwezo
  wa kuanzisha majeshi katika Jamhuri ya Muungano. Ibara ya 121 ya Katiba ya Zanzibar inaunda 'Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar' ambazo ni JKU, KMKM na Chuo cha Mafunzo. Aidha, Ibara ya
  121(3) inampa Rais wa Zanzibar uwezo, "... ikiwa ataona inafaa kuanzisha Idara nyingine yoyote kuwa Idara Maalum." Ibara ya 123(1) inamfanya Rais wa Zanzibar "Kamanda Mkuu wa Idara Maalum na atakuwa na
  uwezo wa kufanya chochote kile anachohisi, kwa maslahi ya Taifa (la Zanzibar?), kinafaa."

  5) Ibara ya 117(3) ya Katiba ya Muungano inaipa Mahakama ya Rufani ya Tanzania mamlaka ya kusikiliza rufaa kutoka Mahakama Kuu (ya Tanzania na ya Zanzibar). Ibara ya 117(4) inaruhusu Bunge au Baraza la
  Wawakilishi kutunga sheria ya kuweka utaratibu wa kupeleka rufaa kwenye Mahakama ya Rufani. Ibara ya 24(3) ya Katiba ya Zanzibar inafuta mamlaka ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania kusikiliza rufaa zozote zinazohusu ukiukwaji wa haki za binadamu kama zilivyoainishwa na Katiba ya Zanzibar na vile vile na Katiba ya Muungano.

  6) Ibara ya 105(1)(b) ya Katiba ya Muungano inamtambua 'Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar' kama mmoja wa wajumbe wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar. Ibara ya 39 ya Katiba ya Zanzibar
  imefuta nafasi hiyo na badala yake kuanzisha nafasi za 'Makamo wawili wa Rais' wa Zanzibar.

  Haya yote ni maeneo ambayo Katiba ya Jamhuri ya Muungano imevunjwa kutokana na Muafaka wa CCM na CUF. Sijawahi kusikia 'machampioni wa Muungano' wakipigia kelele ukiukwaji huu wa Makubaliano ya Muungano wala wa Katiba ya Muungano. Mimi na chama changu tunaodai kwamba Muungano huu uwekwe kwenye kura ya maoni ili wananchi wa pande zote mbili waamue kama wanataka kuendelea nao ndio tunaotukanwa kwamba tunawadharau Wazanzibari, au ni maadui wa Muungano, au tukiachiwa nchi
  tutauua Muungano, n.k. Sisi tunadai kufufuliwa kwa Serikali ya Tanganyika kama namna ya kuuokoa Muungano wetu kwa sababu hatuwezi kuendelea kufumbia macho vitu hivi kwa hofu ya 'kuwaudhi Wazanzibari' kama alivyosema Mwalimu miaka 18 iliyopita! We can no longer maintain this lie! Na 'Muungano ni lulu' is an expensive lie. Muungano uliozaliwa under pressure ya imperialist powers, i.e. Marekani na
  Uingereza na hofu ya Mwalimu na Sheikh Karume juu ya wanamapinduzi wa mrengo wa kushoto kuigeuza Zanzibar kuwa Cuba ya Pwani ya Afrika Mashariki hauwezi ukawa lulu isipokuwa tu kama tunafumbia macho historia halisi ya kuzaliwa kwake.

  Nalidhani ni muhimu na mimi niweke mawazo yangu juu ya jambo hili ili kuuweka mjadala into its proper perspective.

  Tundu


  source: Wavuti - Home
   
 2. Officer2009

  Officer2009 JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 563
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Magamba yamewajaa hadi kwenye ubongo hao wanaojiita machampioni wa muungano kiasi cha kutoweza kufikiria! They are fanatics, and as such, can not reason.
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  tundu lisu ulisha maliza tunasubili mtuongoze kwenye maandamano..arusha tuko tayari
   
 4. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Una uhakika na hilo??
  What kind of proof unaweza kutoa kwa wananchi kuhusiana na hilo?
   
 5. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,586
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Soma makala za Mihangwa katika Raia Mwema na pia Marekani walisha release telegraphic cables ambazo mwanzoni zilikuwa classified documents ambazo zinaonyesha kuwa palikuwa na shinikizo.
  Bahati si Mwalimu wala Karume walio hai leo ambao wangeweza ku respond kuhusu hizo documents.
  Well done Tundu.
   
 6. H

  Haika JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  What kind of proof do you think is enough for someone who has a blocked mind?
  Just go around and read history, even during Nyrere's lifetime he never opposed these claims. Maybe you were not yet born
   
 7. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sisomi makala za mtu yoyote yule, kwa sababu declassified cables za CIA ziko wazi na hazizungumzii uhusikaji wowote wa Marekani kwenye muungano.
   
 8. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  I'm open minded ndio maana sikubali maneno bila proofs.
   
 9. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #9
  Nov 17, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Well! Do you need a proof or an evidence?
   
 10. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #10
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Maandamano, maandamano, maandamano. Tumechoka longolongo. Tunataka ZANZIBAR YETU. Na TANGANYIKA IRUDI. That's all. Hizi hadithi za PAUKWA PAKAWA hatuzihitaji tena. Watanganyika, Wazanzibar tumechoka. INATOSHA. VIVA JF.
   
 11. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Proof....
   
 12. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Hivi wale watuhumiwa wa uhaini (CUF) wakati wa Komandoo waliachia na mahakama kuu kwasababu

  Mahakama kuu iliamua kwamba Zanzibar sio nchi, hivyo uhaini hauwezi kufanywa Zanzibar peke yake.

  Hiyo ni kumbukumbu ipo mahakama kuu itaendelea kuwa referred, labda pale tukapobadilisha muundo
  wa muungano. Acha Wazinzibari (CUF) wajifurahishe kwa kumpinga Tundu Lissu for the sake of kupinga.
   
 13. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #13
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  waliokolewa na mahakama ya rufaa kumbe baadae wameizunguka na kushiriki kufuta madaraka yake juu ya Znz!!
   
 14. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #14
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  wewe twambie sababu za tanganyika kuungana na zanzibar zilikua ni zipi?
   
 15. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #15
  Dec 12, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Pamoja na vifungu vyote vilivyo kaririwa mimi bado nashindwa kuona namna Katiba ya Zanzibar ilivyokiuka Katiba ya Muungano. Sijaona kifungu chochote katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano kinachoifanya Katiba ya Zanzibar kuwa dhalili kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Wala sijaona kifungu chochote katika Katiba ya Muungano kinachoonesha kwamba msingi wa Katiba ya Zanzibar ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wala kinyume chake. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kuwepo ukinzani kati ya Katiba ya Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano hukuwezi kuwa na tafsiri sahihi ya kisheria kwamba Katiba ya Zanzibar imekiuka Katiba ya Jamhuri. Ingekuwa hivyo kama kungekuwa na kifungu katika Katiba ya Jamhuri kinachoitiisha Katiba ya Zanzibar kwa Katiba ya Muungano kama ilivyo, kwa mfano kifungu cha 64 cha Katiba ya Jamhuri kinachozitiiisha sheria za Bunge kwa Katiba. Kinatamka wazi kwamba sheria za Bunge zitaowana na Katiba na kwamba sheria yoyote ya Bunge inayokinzana na Katiba itakuwa batili kwa kiwango inachokizana na Katiba.

  Ninachoweza kuhitimisha ni kwamba ukinzani kati ya Katiba ya Jamhuri na Zanzibar ndio matatizo yenyewe ya Muungano wala sio ukiukwaji wowote wa Katiba ya Jamhuri. Kwa hilo Tundu Lisu na wenzake hawakujiongoza kwa usahihi katika hoja zao.

  Kwa elimu kiasi niliyonayo, kinachopaswa kuwa chimbuko la Katiba ya Jamhuri ni Mikataba ya Muungano. Hata hivyo, miaka michache baada ya kuandikwa kwa Katiba ya Jamhuri maagano kazaa ambayo kwayo iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar walifungamana yamekiukwa.
   
 16. M

  Mutambukamalogo JF-Expert Member

  #16
  Dec 12, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Sawa mkuu. Ila naomba nielimishe.Miaka si mingi nyuma Mahakama ya Zanzbar iliwaachia wanachama wa CUF ambao walishtakiwa kuwa kuwa ni wahaini. Judge alisema kwamba mtu yeyote hawezi kufanya kosa la u haini Zanzbar kwa anayeitwa Rais wa Zanzbar kwani Zanzbar si nchi na ili aweze kusemekana amepinduliwa huyo wa Zanzbar anatakiwa awe Amiri jeshi mkuu!. Kwa sasa atakayempindua Rais wa Zanzbar atakuwa ni sawa na mtu aliyempindua mkuu wa mkoa kwani atatulizwa mara moja na Amiri jeshi mkuu wa Jamhuri ya Muungano. Swali:inakuwaje kule bado kunaitwa nchi na kiongozi wake anaitwa rais?. Usinielewe vibaya naomba ufafanuzi tu wa hii sintofahamu mkuu.
   
 17. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #17
  Dec 12, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Du Lisu kiboko hizi nondo zimetulia ngoja nitafakari kwanza kabla ya kuchangia
   
 18. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #18
  Dec 12, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Nyingine ni ipi?
   
 19. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #19
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35

  Ukitizama vizuri marekebisho ya Katiba ya Zanzibar utaona kwamba pamoja na mambo mengine yalilenga kuadress mapungufu ya udola wa Zanzibar yaliyotokana na tamko hilo la Mahakama ya Rufaa. Maana, katika kutoa hukumu yao majaji wa Mahakama ya Rufaa, walipitia kwa makini vifungu vya Katiba ya Jamhuri na ya Zanzibar kama ilivyokuwa wakati huo. Pengine kwa kuzingatia tafakari yao katika uamuzi wa kesi hiyo, kama ingelertwa leo uamuzi ungekuwa tofauti au kama ungekuwa huo huo kungekuwa na mabadiliko katika tafakari. Hoja inabaki pale pale kwamba Katiba ya Zanzibar kisheria haiwezi kuikeuka Katiba ya Zanzibar. Zinaweza kukinzana tu na hamna inayo prevail dhidi ya nyingine kama kuna ukinzani. Hayo ni baadhi ya maeneo, kwa mtizamo wangu, yanayopaswa kutizamwa kwa chicho la upevu katika uundwaji wa Katiba mpya.
   
 20. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #20
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kwa nini kule panaitwa nchi na kiongozi wake anaitwa Raisi majibu yake yanapatikana katika Hati za Muungano (Articles of Association) kama zilivyotiwa ngivu ya kisheria katika Sheria ya Muungano (Act of the Union between Tanganyika and Zanzibar). Utaona kwamba kusudio la Muungano toka awali ilikuwa ni kuwa na mfumo wa shilikisho wenye sertikali tatu. Walioufuma muungano baadae na kuandika Katiba ya muda na baadae ya 1977 waliamua serikali tatu ziwe katika mfumo tulio nao leo. Kwamba serikali ya Zanzibar ibaki kama sehemu moja ya Muungano ikiwa na Raisi wake na mamlaka yake katika mambo yasiyo ya Muungano. Kwamba serikali ya Tanganyika ife na mamlaka yake yahamie katika serikali ya Jamhuri ya Mungano katika mambo yasiyo ya Mungano. Kwamba serikali ya Muungano iwe na himaya (jurisdictions) mbili. Mosi jurisdiction ya serikali ya Muungano katika maana yake halisi kuhusiana na mambo ya muungano. Plili, jurisdiction ya iliyokuwa serikali ya Tanganyika katika mambo yasiyo ya Muungano. Ndio maana leo Waziri wa Afya ni Waziri wa Jamhuri ya Muungano japo afya sio suala la Muungano
   
Loading...