Mh. Lissu, jaji haondolewi kwa malalamiko bungeni au katika majukwaa ya kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Lissu, jaji haondolewi kwa malalamiko bungeni au katika majukwaa ya kisiasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Teroburu, Sep 5, 2012.

 1. T

  Teroburu Member

  #1
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh. Lissu, Mfunge Paka Kengele

  • Nimeshangazwa sana na hatua ya Mh. LISSU ya kuvunja Kanuni za Bunge na kutawanya katika magazeti kile alichokiita utetezi wake bila kujali haki asilia ya wale anaowatuhumu. Nitashangaa kama Bunge litashindwa kulinda hadhi na heshima yake kwa kutomchukulia Mbunge huyu hatua kali za kinidhamu.
  • Nimeshangazwa sana pia na hatua ya MH. LISSU kuendelea kulalamika katika Mkutano wa Mawakili na kutaka MAJAJI ALIOWATUHUMU WAONDOLEWE bila ya yeye kuchukua hatua za KIKATIBA.
  • Mh. LISSU na “WANASHERIA-HARAKATI” wenzako, nchi yetu iaongozwa na sheria na sio na kulalama.
  • Ni Katiba hii hii ya Jamhuri ya Muungano ambayo imempa Mh. Lissu Ubunge, vinginevyo ni watu wachache sana walikuwa wanamfahamu Tundu Lissu kabla ya kuukwa UBUNGE. Na ni kwa kutumia KINGA YA Katiba hii hii ambayo ndiyo Mh. Lissu anaitumia kuwatuhumu na kuwahukumu MAJAJI na Mhimili wote wa MAHAKAMA.

  KINGA YA KIKATIBA YA UHURU WA KUONGEA ANAYOTUMIA MH. LISSU

  • Ni katiba hiyo hiyo iliyompa uhuru wa kuongea Mh. Lissu, ndio hiyo hiyo iliyowapa majaji kinga na kuondolewa kwa utaratibu maalumu. Kinga anayotumia Mh. Lissu kuwatukuhumu na kuwahukumu Majaji ni IBARA ya 100 inayosema:
  100. Uhuru wa majadiliano na utaratibu wa shughuli bungeni
  (1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge, na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.
  (2) Bila ya kuathiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanyw ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo.


  • Pamoja na Wabunge kuwa na Kinga, Katiba hiyo hiyo iliyowapa waheshimiwa Wabunge KINGA pia inampa Mh. Rais KINGA, na pia inawapa Majaji KINGA na utaratibu wa kuwaondoa majaji kwenye nafasi zao za ujaji. Ibara zinazotoa kinga kwa Mahakama ni hizi. Ibara ya 107B IMETAMKA KUWA KATIKA KUTEKELEZA MAMLAKA YA UTOAJI HAKI, MAHAKAMA ZOTE ZITAKUWA HURU NA ZITALAZIMIKA KUZINGATIA TU MASHARTI YA KATIBA NA YALE YA SHERIA ZA NCHI.

  UTARATIBU WA KATIBA KUWAONDOA MAJAJI WENYE TUHUMA

  • Kama ilivyo kuwa kuna utaratibu wa KIKATIBA NA KISHERIA kwa Mbunge kupoteza Ubunge, pia zipo taratibu za KIKATIBA Rais kuondolewa kutoka ofisi ya Rais na MAJAJI kuondolewa kutoka katika nafasi zao za UJAJI. Tanzania ni nchi ya utawala wa Katiba, Sheria na taratibu!


  • Ni matumaini yangu kuwa Mh. LISSU aliapa kuilinda na kuitetea Katiba na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kuwa Katiba ya Tanzania imetoa utaratibu wa kupokea tuhuma dhidi ya Majaji na Mahakimu na namna ya kushughulikia tuhuma hizo. Nitaeleza baadaye kwa nini mimi nadhani Mh. Lissu anatumia isivyo KINGA yake ya Ubunge kwa kulalamika KISIASA bila kuchukua hatua za KIKATIBA NA KISHERIA.


  • Mh. Lissu anaweza kutoa hoja kuwa haipendi KATIBA ya sasa. Lakini hii ndio KATIBA iliyompa ngazi ya kupanda na kuwa Mh. Mbunge. Hii ndio Katiba iliyo halali inayofanya watanzania wamsikilize Mh. Lissu hata kama wengine hawakubaliani naye!! Tanzania nchi pekee ambayo utakuta Mbunge akilaani na kulaumu mfumo wa Katiba na sheria alioutumia kuupata ubunge.


  • Kama Mh. Lissu haipendi KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO, basi aachie kiapo chake cha Ubunge na ajiuzulu UBUNGE ili afanye uharakati wa kupata Katiba anayopenda. Sio uungwana na sio sheria kutumia Katiba kupata daraja la Ubunge na mara baada ya kupata Ubunge kuihujumu Katiba hiyo hiyo.

  KUWAONDOA MAJAJI KUTOKANA NA MARADHI, TABIA MBAYA

  • Kwa mujibu wa Katiba, kuna utaratibu wa kikatiba wa kumtuhumu na kuondolewa kwa JAJI.


  • JAJI ANAWEZA KUONDOLEWA kama itathibitishwa na Tume MAALUM kuwa ameshindwa kutekeleza kazi zake (ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote) au kwa sababu ya tabia mbaya inayoathiri Maadili ya Kazi ya Jaji au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.


  • Kamwe JAJI haondolewi kwa mayowe, kelele au vigelegele vya kisiasa. Jaji haondolewi kwa umahiri wa uongeaji wa Mh. Mbunge. Tusiwadanganye watanzania kuwa Mbunge Lissu anao uwezo wa kumuondoa JAJI yoyote kwa yeye kumtuhumu, kumtia hatiani na kumtaka aondoke bila kufuata utaratibu wa Kikatiba.


  • Mh. Lissu, kama unavyotegemea kinga ya Wabunge kwa mujibu wa Ibara ya 100 ya katiba, kumbuka kuwa Majaji, Rais pia wanayo kinga ambayo wewe pia ni vyema uiheshimu.


  • Mh. Lissu, IBARA 110 inazungumzia namna ya kumuondoa JAJI. JAJI haondolewi kwa kuwa tu Mbunge (Mh. Lissu) katoa tuhuma na kuchukua jukumu la kuithibitisha yeye mwenyewe na kudai JAJI aliyemtuhumu aondolewe. Huu ni utaratibu mpya sana ambao Mh. Lissu anautangazia umma wa Tanzania.


  • IBARA ya 110 inayoratibu namna ya kumuondoa JAJI inatamka:
  110-(5) Jaji wa Mahakama Kuu aweza tu kuondolewa katika madaraka ya kazi ya Jaji kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake (ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote) au kwa sababu ya tabia mbaya inayoathiri Maadili ya Kazi ya Jaji au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma; na hataweza kuondolewa kazini ila kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (7) ya ibara hii.
  (6) Iwapo Rais anaona kuwa suala la kumwondoa Jaji kazini lahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo mambo yatakuwa ifuatavyo–

  (a) Rais atateua Tume ambayo itakuwa na Mwenyekiti na Wajumbe wengine wasiopungua wawili. Na huyo Mwenyekiti na angalau nusu ya Wajumbe wengine wa Tume hiyo itabidi wawe watu ambao ni Majaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani katika nchi yoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola;

  (b) Tume hiyo itachunguza shauri lote halafu itatoa taarifa kwa Rais kuhusu maelezo ya shauri hilo lote na itamshauri Rais kama huyo Jaji anayehusika aondolewe kazini kwa mujibu wa masharti ya ibara hii kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi na sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya.

  (7) Ikiwa Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (6) itamshauri Rais kwamba Jaji ambaye habari zake zimechunguzwa na hiyo Tume aondolewe kazini kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya, basi Rais atamwondoa kazini Jaji huyo anayehusika.

  (8) Ikiwa suala la kumwondoa Jaji kazini limepelekwa kwenye Tume kwa ajili ya uchunguzi kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (6) ya ibara hii, Rais aweza kumsimamisha kazi Jaji huyo anayehusika, na Rais aweza wakati wowote kufuta uamuzi huo wa kumsimamisha kazi Jaji huyo, na kwa hali yoyote uamuzi huo utabatilika ikiwa Tume itamshauri Rais kwamba Jaji huyo asiondolewe kazini.

  (9) Masharti ya ibara hii yatatumika bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (12) ya ibara ya 109 ya Katiba hii.


  • Utaratibu wa kumuondoa Jaji kwa mujibu wa Ibara ya 110 ya Katiba unazingatia msingi muhimu wa katiba ambao Mh. Lissu amewanyima Majaji aliowatuhumu, yaani haki ya kusikilizwa kabla ya kuhukumiwa kwa mujibu wa Ibara ya 13 (6) (a) na (b) ya Katiba yaani:-

  - haki ya MAJAJI waliotuhumiwa na MH. LISSU kupewa fursa ya kusikilizwa na chombo cha kikatiba kilichoundwa kwa mujibu wa IBARA ya 110 ya Katiba;

  -haki ya MAJAJI waliotuhumiwa na MH. LISSU kutotendewa kama TAYARI wana makosa anayodai Mh. LISSU mpaka itakapothibitika kwa mujibu wa IBARA ya 110 kuwa wanayo makosa anayodai Mh. Lissu;


  • Mheshimiwa Lissu hana budi kuheshimu kiapo chake cha kuilinda na kuiheshimu Katiba ya JAMHURI ya Muungano wa Tanzania na afuate utaratibu wa kikatiba badala ya kutumia kinga yake ya Bunge kutuhumu, kuhukumu na kutoa adhabu kwa majaji ambao amewataja kwa majina.


  • Watanzania ni vyema tukachukua tahadhari dhidi ya watanzania wenzetu ambao wamejiweka katika daraja la juu kuliko hata Katiba na sheria iliyowapa uongozi.

  KAMATI ZA MAADILI ZA MAJAJI NA MAHAKIMU

  • Mwaka jana, Bunge letu lilipitisha Sheria iitwayo JUDICIARY ADMINISTRATION ACT, 2011 (SHERIA YA BUNGE NAMBA 4 YA MWAKA 2011) na MH. LISSU alishiriki kikamilifu katika kutunga Sheria hii inayotoa muongozo wa kupokea malalamiko na tuhuma dhidi ya majaji na mahakimu. Kwa sababu zake mwenyewe, Mh. Lissu ametumia jukwa la kisiasa kulalamika badala ya kufuata utaratibu wa malalamiko ili hao anaodai hawafai waondolewe kwa mujibu wa KATIBA na Sheria.
  • Kumbu Kumbu za Bunge zinaonyesha ushiriki wa Mh. Lissu kwa ukamilifu. Sheria hii kimeanzisha KAMATI ZA MAADILI ZA MAJAJI, MAHAKIMU NA MAAFISA WENGINE WA SHERIA.
  • Kwa mfano SHERIA YA BUNGE NAMBA 4 YA MWAKA 2011 imeanzisha Kamati ya Maadili ya Majaji (Judges Ethics Committee) iliyopewa jukumu la:

  • kupokea tuhuma dhidi ya uvunjifu wa maadili dhidi ya Majaji wa Mahakama ya Rufaa, Jaji Kiongozi na Majaji wa Mahakama Kuu. Tuhuma dhidi ya Majaji hawa ni lazima iwe ni kwa maandishi na iwasilishwe kupitia Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.
  • Kazi ya Kamati ya Maadili ya Majaji ni kuchunguza Tuhuma na kuwasilisha Maoni yake kwa Tume ya Utumishi wa Mahakama.
  • Tume ya Utumishi wa Mahakama itasikiliza na kutoa mapendekezo yake kwa Mh. Rais kuhusu kuundwa Tume Maalum ya Kikatiba ya Kumchunguza Jaji.

  SHERIA YA BUNGE NAMBA 4 YA 2011 IMEANZISHA KAMATI YA MKOA YA MAADILI

  • Kila Mkoa unayo Kamati ya Mkoa ya Maadili inayoshughulikia nidhamu ya Mahakimu Wakazi na Mahakimu wa Wilaya (Region, the Regional Judicial Officers Ethics Committee). Kila Wilaya pia inayo Kamati za Maadili ya Wilaya inayoshulikia nidhamu ya Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo.


  • Mh. Lissu anafahamu fika kuwa zipo taratibu za kushughulikia mapungufu au malalamiko dhidi ya Majaji, Mahakimu na Maafisa wengine wa Mahakama. Ila amechagua tu kuwadhalilisha Majaji ili wawe waoga na wasiweze kutoa maamuzi yao bila upendeleo wala uoga.
  UKIMYA WA WANASHERIA, WASOMI MAHAKAMA INAPOSHAMBULIWA

  • Uwoga ni kitu hatari sana katika ujenzi wa demokrasia. Ufundi wa kuongea Bungeni hauna maana kuwa kila kisemwacho na muongeaji mahiri ni sahihi!
  • Ni kwa bahati mbaya WASOMI, WANASHERIA, magazeti na vyombo vingine vya habari WANA AMINI KUWA KILA KISEMWACHO na Mbunge LISSU ni sahihi na wamefumba macho kuhusu haki ya msingi ya kila mtanzania kusikilizwa na kufuata utaratibu.


  • MAGAZETI YANAONA KUWA ni sahihi kwa Mh. Lissu kujipa jukumu la kupeleleza “makosa ya majaji”, “kuwatuhumu na kuwatia hatiani majaji” na “kupendekeza adhabu yeye mwenyewe”.


  • Watanzania tusicheze na haki asilia ya kusikilizwa na umuhimu wa wanasiasa wa wanasheria kuheshimu sheria walizotunga wao wenyewe. Hata MH. LISSU anastahili HAKI asilia ya kutotuhumiwa bila ya kupewa nafasi ya kusikilizwa na kwa utaratibu uliowekwa kisheria.

  JE TUHUMA DHIDI YA MAJAJI NI MUENDELEZO WA LENGO LA JAMHURI YETU ISITAWALIKE?

  • Naogopa kuamini kuwa tuhuma dhidi ya Mhimili wa Mahakama ni muendelezo wa SERA ya kuhakikisha kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitawaliki.


  • Mimi nadhani ni Mhimili wa Mahakama tu ndio ulikuwa umebaki katika mtikisiko huu wa kuhakikisha kuwa Tanzania haitawaliki.


  • Na njia pekee ni kuwashambulia na kuwashushia majaji heshima mbele ya jamii. Lengo ni kuwafanya Majaji wawe waoga na wasitoe maamuzi magumu.


  • Kwa Waheshimiwa MAJAJI na MAHAKIMU, huu ni wakati wenu wa kuwa kitu kimoja. Huu ni wakati wa kutokuwa na uoga na kutimiza wajibu wenu kwa mujibu wa katiba, sheria na masharti ya viapo vyenu. JAJI HAONDOLEWI KWA KELELE ZA KISIASA!


  • Nasikia eti “WANASHERIA-HARAKATI” wametayarisha WARAKA WA KUWAKATAA MAJAJI. WAKILI YEYOTE ambaye anachukuliwa kuwa anaelewa utaratibu wa kuwasilisha malalamiko dhidi ya JAJI au HAKIMU akiwasilisha WARAKA basi huyo WAKILI atakiwe ajieleze kwa nini asitolewe katika orodha ya mawakili kwa kuwa hajui sheria za Tanzania za namna ya kuwasilisha Malalamiko dhidi ya JAJI au HAKIMU.

  WANAOTAKA TANZANIA ISITAWALIKE WANAJUA KUWA UKITIKISA MAHAKAMA UNATIKISA UTAWALA WA SHERIA NA UNATIKISA UHAI WA TAIFA LETU.

  WANAOTAKA NCHI ISITAWALIKE HUITWA “ANARCHISTS” au “DEMAGOGUES”. Hawa wameongezeka sana chini ya kivuli cha demokrasia na haki ya kusema chochote popote bila kjali sheria yoyote au haki ya mtu mwingine yeyote.

  MAHAKAMA MKIYUMBA SISI WANANCHI WA KAWAIDA NDIO TUTABAKI MIKONONI MWA ANARCHISTS na DEMAGOGUES WASIOHESHIMU SHERIA NA AZMA YAO YA TANZANIA ISITAWALIKE itatimia.

  MUNGU IBARIKI JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
   
 2. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Wewe ni FUNDI hodari wa kuongea na kuandika. Lakini hata hivyo, wewe na wote mliothubutu kumjibu Mheshimiwa Mbunge Lisu, hakuna hata mmoja aliyekanusha POINT baada ya point. Lisu aliwataja kwa majina na UGOLO wenu, mbona hamfanyi uchambuzi wa ki-hoja kumpinga LISU? Hiyo tume ya uongozi wa mahakama unayoshauri ati Lisu angepeleka malalamiko,ndiyo wale wale..!!
   
 3. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Wewe hujamwelewa Mh.Lisu,lengo lake ni kuufahamisha umma jinsi gani mambo yanavyofanywa kinyume kabisa na utaratibu yote hayo uliyoyaongelea hata Mh.Lisu anajua sana tatizo taratibu hazikufuatwa tu ndiyo malalamiko yake na yetu pia maana hatukupata waliostahili.
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nachukia mtu anapoandika habari ndefu iliyojaa pumba na mashudu tupu! Huenda nawe ni jaji wa kitaa! Tundu Lisu was right simple
   
 5. p

  politiki JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Nimesoma nimeshindwa kuelewa point yako hasa nini unaelekea hujui unachopinga kwa maana malalamiko mengi ya Lisu yapo kwenye tume iliyoundwa na kukuta uozo mtupu miongoni mwa majaji, tume yenyewe ikapendekeza wahusika watimuliwe kwani wengine walifikia mahala mpaka pa kudanganya kwenye CV zao na ELIMU zao pia lakini ndio hivyo tena hatuna Rais ikulu kilichopo ikulu pale ni empty suit imepita miaka minne toka akabibidhiwe hotuba ile hakuna chochote alichokifanya.
   
 6. mauro

  mauro Senior Member

  #6
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Katiba hii hii ndio imempa rais mamlaka ya kuteua Majaji wa Mitaani na wa mikataba hehehehehe I thought mmngemjibu Tundu Lissu mmngepangua hoja zake moja baada ya nyingine badala ya kutafuta kipori cha kujificha ?
   
 7. Deus F Mallya

  Deus F Mallya Verified User

  #7
  Sep 5, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 707
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mhe.Kwanza mbna umekuwa too low kwenye majibu yako? Sijaona ulichomjibu Mhe.Lissu kutokana na tuhuma zake kwa Rais JK. Unachotaka kusema ni kwamba kwakuwa kuna katiba na sheria (Ambavyo vilikiukwa wakati wa kuteuliwa kwao) basi katika kuwaondoa zifuatwe. Sasa aliyewateua naye usisahau kuwa aliapa kuilinda na kuihifadhi katiba hiyo.

  Anajua alichokifanya (Iwe alidanganywa au alijua mwenyewe). Sidhani kama uko sahihi kuelezea hoja nzito vile (Ya Mhe.Lissu) kwa majibu mepesi kwa kiwango hiki.
   
 8. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2012
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Teroburu mbona umekuja na pumba? Brabra nyiiiiingi hoja hakuna, Jaribu kujibu Hoja za Tundu Lissu eg Jaji.YYY..ana sifa zote kwani alitunukiwa shahada XXX,kutoka chuo zzzz etc
   
 9. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Naona Tony umeamua kuhamishia mjadala hapa baada ya kuona kule "wanabidii" hoja zako zote zime "fail"

  Jipange tena na acha ubishi wa kijinga Mkuu!!
   
 10. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  @Teroburu , kwani katiba/sheria inasemaje kuhusu jaji/majaji walioteuliwa kinyume cha katiba/sheria? Leo hii muheshimiwa Rais akimteuwa mkewe Salma kuwa jaji licha ya kuwa hana sifa za kuwa jaji, je bado atatambulika kikatiba kuwa ni jaji na hivyo kupata kinga zilizomo kwenye katiba? Utaratibu uliousema, kwa sehemu kubwa naamini unawahusu majaji ambao uteuzi wao ulizingatia matakwa ya kikatiba.

  Hata hivyo nakubaliana na mantiki yako kuhusu kufuata utaratibu wa kikatiba. Kama kweli tunaamini (bunge) kuwa rais amekiuka katiba ambayo aliapa kuilinda, then mtu wa kuwajibishwa kwanza ni Rais na baadae tufuate hao ambao 'wamepewa ulaji' kinyume cha katiba.

  By the way, kama mtu unateuliwa kuwa jaji na unajua kuwa hustahili kuwa jaji kikatiba (i.e. unajua anayekuteuwa anavunja katiba), je ethically na hata kisheria unatakiwa kufanya nini?
   
 11. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #11
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Mkuu, yaani huyu ZUZU anajifanya ana stori ndeeeeeefu, kumbe pumba tupu. anadhani maneno mengi ndo kushawishi watu, hakuna lolote hapo. Hoja za TL zipo wazi kabisa, TL alihoji uhalali wa mtu kupewa ujaji wakati kiwango cha elimu hakiruhusu, Mbona huyu ZUZU hajajibu??? TL alihoji ukiukwaji wa katiba kwa kumpa mtu ujaji wakati umri wa kustaafu ulishatimia, mbona huyu ZUZU hajajibu??? TL alihoji uhalali wa mtu kupandishwa cheo wakati afya yake haimruhusu kutekeleza jukumu hilo, mbona huyu ZUZU hajajibu??? badala yake anakimbilia kumshangaa TL, kwa kifupi TEROBURU una tia huruma sana, mimi ndo nimekuwa nikijiuliza, hivi kama viongozi wa serikali ndo mna uwezo mdogo hivi wa kuchambua mambo, hivi kweli mtaweza kubuni mbinu za kututatulia matatizo yetu??? SIDHANI, yaani mmekalia KUTETEANA TU NA KULINDANA, MBAYA ZAIDI HATA UKWELI NYIE MNAUBADILI UONEKANE VINGINE, ILI TU MUENDELEE NA UPUUZI WENU. yaani nyie ccm MLAANIWE HAKYANANI!!!!!! aaaaarrrrrrrrggggggggggghhhhhhhhhh!!!!!!
  Tuendeleeni kuwaelimisha watanzania, waelimike ili waling'oe madarakani hili li serikali la ccm MAONGO/MAJAMBAZI/MAFISADI/WAUAJI.
   
 12. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #12
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Kumbe.....
   
 13. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #13
  Sep 5, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hilo tunalijua, katika utawala wa kidikteta hakuna muhimili unaotenda haki. Hivyo ni vizuri tu sisi wananchi tumejua ukweli na tutajua cha kufanya 2015 ili tuondokane na mapungufu haya yanayoligharimu Taifa.
   
 14. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  @Teroburu Ulichoandika hapo ni kujaribu kutetea ndugu/kujitetea mwenyewe kama wewe ni mmoja wa majaji wa Kitaa. Vinginevyo, huna hoja ya kuweza kupangua alichokiwakilisha Tundu Lissu. Ni bora ukae kimya kuliko kuendelea kuwafungua watu masikio wakaendelea kuujua ukweli kwa undani zaidi.
   
 15. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #15
  Sep 5, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  we torabora ndo unasoma open nini? jibu hoja how come jaji wa rufaa ambayo ni the supreme court hapa nchini mmoja wa majaji wake hana LLB. hii ni tanzania tu inawezejana.
   
 16. f

  fakisi Member

  #16
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  Ha ha ahaaaa Tony kashindwa kule analeta kelele huku, jamaa Tundu Lissu kawashika pabaya sana!
   
 17. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #17
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mwalimu!
  Nina hakika ni huyu huyu!! Alielekezwa sana na hata Lissu mwenyewe alimpa darsa tosha lakini naona hajaridhika!

  Huyu mtu inaonesha ubishi ni kipaji chake!

  Ni wa kupuuzwa tu!
   
 18. m

  mamajack JF-Expert Member

  #18
  Sep 5, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  wewe mtoamaada,toka lini mtu aliyeteuliwa ki magumashi akaondolewa na mtu yuleyule kwa sababu za ukweli.tundu amefanya kazi yake na wananchi tumejua ukweli.kumwondoa au kumbakiza sio juu yake personally ninaemuona ni mpuuzi hapa,ni yule aliyemteua na wengine wote walishiriki uteuzi huo.
   
 19. 654

  654 Senior Member

  #19
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 173
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Moderators, huyu nae katokea wapi? ...............dhaifu
   
 20. M

  Mundu JF-Expert Member

  #20
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Uko sahihi mkuu. Heri mimi sijasoma.
   
Loading...