Polisi wetu wakipokea amri wao wanafanya bila kuangalia sheria zinasemaje au wanajua lakini wanajaribu kutekeleza amri ya boss wao. Hii ni hatari kwa demokrasia ya kweli kwenye nchi. Hivi unawezaje kumzuia mbunge asikutane na wapiga kura wake? Mimi nafikiri mbunge hapashwi kuomba ruhusa polisi ili kufanya mkutano, anapashwa kutoa taarifa tu kwamba siku fulani nina mkutano na wapiga kura wangu tarehe fulani na mahali fulani basi!!!. Na polisi wanapashwa kutoa ulinzi basi!!! sio kutoa ruhusa!!!
Tiba
Tiba,
neno sio "Kupashwa"..........neno sahihi ni...... "Kupaswa/Kupasa"...........
Kupasha maji, chai, chakula, misuli, au habari..........e.g .Tiba alipashwa habari ya maendeleo wilaya ya Bukoba vijijini
Ukiwa Mfanyakazi Inakupasa kwenda Ofisini.............na unapaswa kufanya kazi
Inawapasa Polisi kutoa ulinzi......au...Polisi wanapaswa kutoa ulinzi
Mrdennis,Hivi kikwekte pamoja na kuiba kura na kupewa urais, baado ana hofu gani na chadema?
ccm wametumia mbinu zote chafu ktk vitabu wakati wa uchaguzi, bado hawajaridhika, na sasa wanawanyima wananchi haki ya kukukutana na kuongea na wawakilishi wao! This is going too far na inaonyesha wazi yanayosemwa kwamba , ccm wao wapo kwa ajili ya masilahi ya utawala tuu, hawajali wananchi wanataka nini! It's pathetic, wanazidi kujichimbia mashimo.
Hivi hawa watu huwa hawana watu wa kuwashauri, hii nayo ni strategy ya namna gani kama si ujinga, wanadhani watazuia hiyo mikutano hadi lini? naona nia yao ni kutaka wananchi waanzishe fujo.