Mh lema jiulize kwa nini umesusiwa hafla arusha?

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
1,222
764
Siku si nyingi nili post thread iliyohusu Arusha Development Fund - ADF. Nikashauri waangile muundo wa watendaji pamoja na kuweka trustees ambao wanakubalika kwenye macho ya jamii. Sina maana kwamba waliopo hawakubaliki ila bado ni wachanga mno kuweza kushawishi Uma katika mambo ya kuleta maendeleo.

Kulikuwa na hafla ambapo Mh Lema alikuwa anawakabidhi ada wazazi wa wanafunzi 400. Kwenye hafla hiyo viongozi wote wa mkoa walialikwa ila aliyefika ni OCD peke yake na nina hisi alikuja kwa ajili ya kucheki kama mabomu yangehitajika basi aweze kuwasiliana na vijana wake. Ni jambo la kusikitisha sana ila ADF ijiulize ni kwanini viongozi wa serikali hawakufika.
 
kwani wewe unaona kuwapatia wanafunzi 400 ada ni jambo dogo?wewe bado una fikira za zamani mpaka mafisadi wawepo ndio shughuli ziendelee? mie siko arusha lakini alichokifanya lema na wenzie kwa mpenda maendeleo ni kikubwa mno.natamani kuwa na mbunge kama lema
 
Hata Lema mwenyewe ilimsononesha kwa nini uongozi wa mkoa haukutokea na aliongea katika hotuba yake.
 
Blue Balaa, viongozi hao unaowasema ni viongozi na wanachama wa CCM maana hawabanwi na katiba ukitoa askari ambao hawana chama. Sasa ulitegemea RC, DC wahudhulie sherehe wahatarishe vibarua vyao? Nilitegemea kabisa kuwa wasingehudhuria ili kutoa picha mbaya kwa wananchi kama ambavyo nao CDM walishafanya katika baadhi ya vikao!
 
tuache majungu inajulikana kwa nini wana CCM hawakuja haihitaji rocket science kujua siasa ina-overrule hata maendeleo ya kila siku majimboni! kama alichofanya Lema ni kidogo kudharauliwa niambie Mbunge wa CCM aliyeweza kufanya alilofanya Lema kwa uwazi na kwa muda mfupi namna hiyo!
 
Hivi kutohuzuria kwao kuna athari zozote?
Pia khudhuria means kumkubali yy na mpango wke or yake unatemea cc mu wafanye hayo?
 
siasa za bongo hizo,jiulize huo mfuka kipindi cha nyuma haukuwepo?au unataka kupingana na ukweli kua hafla nyingi kama hizo wewe tangaza kuna posho usikie mziki wake,pasinge wananchi walikua wanadhulumiwa,alikuwa mbunge kabla ya lema tulikua hatumuoni kwenye tv wala magazeti,hakuwahi kuonekana kwenye shughuli za maendeleo wala misaada miaka yake yote ya ubunge,lema mpambanaji na anaweza kiukweli,big up man chapa kazi watu wanataka vitendo sio propaganda za sisiemu miaka nenda rudi.
 
ccm na siasa za maji taka hao. ndizo zinawamaliza. mfano - kama RC na Dc wangekuwepo ingepunguza upinzani kuonyesha kuwa nao walikuwa sehemu ya kufanikisha zoezi.....sasa hivi wanaonekana kuwa hawana mapenzi yoyote kwa wana arusha bali tu wana mapenzi na kura zao...wanafiki na wazandiki wakubwa!
 
Duh! umenikumbusha ule wimbo enzi za chipukizi CCM ! CC EMU CC EMU USI SI SI EMU SI SI EM SHIKA HATAMU , c

sasa inatakiwa chipukizi (kama bado wapo) cc em cc emu cc eum shika mkiaaaaa

Muheshimiwa ,the most Honourable LEMA,nakutakia mafanikio mema ktk uwakilishi wako bungeni na kwa wananchi.
 
Hata Lema mwenyewe ilimsononesha kwa nini uongozi wa mkoa haukutokea na aliongea katika hotuba yake.
Jamani embu kabla hamjaongea chochote,jifunze kazi ya mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya kikatiba then ulete mawazo yako finyu hapa,nachojua watu hao ni wahamasishaji tu nothing else.hivyokutokuwapo wao no effect bali ni wajinga.
jjjamanijJa
 
Siku si nyingi nili post thread iliyohusu Arusha Development Fund - ADF. Nikashauri waangile muundo wa watendaji pamoja na kuweka trustees ambao wanakubalika kwenye macho ya jamii. Sina maana kwamba waliopo hawakubaliki ila bado ni wachanga mno kuweza kushawishi Uma katika mambo ya kuleta maendeleo.

Kulikuwa na hafla ambapo Mh Lema alikuwa anawakabidhi ada wazazi wa wanafunzi 400. Kwenye hafla hiyo viongozi wote wa mkoa walialikwa ila aliyefika ni OCD peke yake na nina hisi alikuja kwa ajili ya kucheki kama mabomu yangehitajika basi aweze kuwasiliana na vijana wake. Ni jambo la kusikitisha sana ila ADF ijiulize ni kwanini viongozi wa serikali hawakufika.

Hata ungekuwa wewe usinge hudhulia shughuli za waasisi wa fujo
 
Wewe ili ndio umeliona leo! Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu Kikwete alikuwa akipita mikoani viongozi wote wa serikali wa juu wa mkoa walikuwa wanaudhuria lakini Dkt Slaa alikuwa akipita mikoa hiyo hiyo ulikuwa huoni hata mmoja. Madaraka ya rais ambaye pia ni mwenyekiti wa ccm ni makubwa sana,ndio maana tunadai katiba mpya.
 
Rudini kwenye hoja ya msingi alichofanya lema ni sahihi na anastahili pongezi zake lakini hoja hiyo kamati inayosimamia huo mfuko ina walakini kuanzia mkiti mpk wengi wa wajumbe wake si watu wa kuaminika kimienendo yao amemchomeka na hawara yake hata viongozi wa cdm c wote walihudhuria na tatizo ni hilo lema haaminiki katika masuala ya fedha na kamati yake hivyo hivyo
 
ADF ni ya kupongezwa licha ya ada pia wanafunzi hao wanapewa matibabu bure na taasisi fulani. Ni fikira finyu kuwategemea RC na DC.
 
Waliosusa kuhudhulia hafla ile hawakumsusia Lema kama wanavyodhani bali waliowasusia wale watoto 400 abao masikini ya Mungu ni innocent.
 
Siku si nyingi nili post thread iliyohusu Arusha Development Fund - ADF. Nikashauri waangile muundo wa watendaji pamoja na kuweka trustees ambao wanakubalika kwenye macho ya jamii. Sina maana kwamba waliopo hawakubaliki ila bado ni wachanga mno kuweza kushawishi Uma katika mambo ya kuleta maendeleo.

Kulikuwa na hafla ambapo Mh Lema alikuwa anawakabidhi ada wazazi wa wanafunzi 400. Kwenye hafla hiyo viongozi wote wa mkoa walialikwa ila aliyefika ni OCD peke yake na nina hisi alikuja kwa ajili ya kucheki kama mabomu yangehitajika basi aweze kuwasiliana na vijana wake. Ni jambo la kusikitisha sana ila ADF ijiulize ni kwanini viongozi wa serikali hawakufika.

Kwani Tanzania kuna serikali hadi kuwe na viongozi?
 
Huu utaratibu wa kualika wanasiasa kwenye mambo ya maendeleo ulitoka wapi? Kuja kwao wangechangia pesa kiasi gani? Kwani failure yao si ndiyo iliyosababisha umaskini wa hao waliokuwa wanasaidiwa, sasa kwa nini uwaalike tena?
 
Duh! Naona BB kasepa into trees! kakimbia bakora! Nani anaitaka CCM siku hizi?
 
Back
Top Bottom