Mh. Kinana, 'Hatukushiba kwenye sahani vipi kwenye kijiko?

laigwenan

JF-Expert Member
Apr 13, 2012
325
195
NDUGU wanajamvi nawapenda sana,

Miradi mingi ya maendeleo inchini 'IMEKWAMA' , na sababu kubwa ikielezwa kuwa fedha za budget zinazotengewa wizara nyingi kutokufika kabisa wizarani, mathalani wizara nyingi zimepokea chini ya 30% ya budget zilizo idhinishwa na bunge msimu wa 2013/2014.

HIVYO MKWAMISHAJI MKUU WA SHUGHULI ZA MAENDELEO INCHINI NI SERIKALI chini ya CCM.

Kana kwamba hiyo haitoshi Katibu mkuu wa CCM taifa mh. Kinana na timu yake amekuwa akiwabeza mawaziri wanaotokana na chama ambacho yeye ni mtendaji mkuu kuwa ni mizigo hivyo miradi mingi ya maendeleo nchini inakwama kwa kuwa inaongozwa na Mawaziri Mizigo.

Kwa kuwa CCM imeshindwa kabisa kuisimamia serikali inayoiongoza imeamua kurudi kwa wanainchi ambao asilimia zaidi ya 70 tunaishi chini ya dollar 1 kwa siku kuwa ichangie shughuli za maendeleo ambazo serikali imeshindwa kabisa kuisimamia.

Akiwa Ziarani Singida Mh. Kinana amewabeza upinzani kwa kuwahamasisha wanainchi kuacha kuchangia shughuli za maendeleo kwani ni jukumu la serikali kuzisimamia shughuli hizo ,Mh. Kinana amekwenda mbali zaidi na kusema ni jikumu la wanainchi kuchangia shughuli za maendeleo.

Inaaminika Tanzania ni moja kati ya inchi za Afrika zinazoongoza kwa misamaha ya kodi na ni moja ya nchi duniani ambazo 50% ya budget yake ya mwaka inategemea Misaada, 'aibu kweli kweli'.

Na ripoti zinaonesha kuwa Tanzania ni moja ya nchi tatu Afrika zenye rasilimali nyingi lakini ni maskini kweli kweli.

Mh.Kinana kama serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake mwananchi wa kawaida anaweza Kweli? Atawezaje kuchangia ujenzi wa miundo mbinu kama barabara wakati kula yake ni ya MASHAKA?

Mh. tuchange shilingi ngapi ili tununue madawati,vitabu maktaba na maabara kwenye shule zetu wakati fursa za ajira hazipo?

Mh. Kinana tukusanye kwa nguvu gani gharama za Maji,Afya,Elimu,nishati,kilimo, na mazingira wakati ninaishi chini ya dollar 1 kwa siku !!

Mh. Kinana kwanini lakini unajaribu kuhamisha majukumu ya Serikali yako kwa wanainchi?

Mh.kama shughuli hizi zitafanywa na wanainchi tuambie serikali inafanya kazi gani!!, inakusanya kodi na kukopa kwa sababu gani?.

Mh. Kinana wewe kama mtendaji mkuu wa chama unawajibu wa kuisimamia serikali kutekeleza wajibu wake kwa wanainchi na si kuhamisha majukumu ya serikali kwa wanainchi na kama umeshindwa kuisimamia serikali inayo ongozwa na chama chako ili kutimiza ahadi ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA JUA UMESHINDWA KAZI MH.

MY TAKE: IKUMBUKE CHADEMA WAKATI MWINGINE UTAKAPO PIGA KURA.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom