Mh Kimaro atetea kuua soko la mkonge, ataka JUTE ya India | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh Kimaro atetea kuua soko la mkonge, ataka JUTE ya India

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TreasureFred, Jun 18, 2009.

 1. TreasureFred

  TreasureFred Member

  #1
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wana jf nimeamua kupost hili jambo baada ya kuona mpiganaji anataka kua soko la mkonge kwa kulinda biashara ya mpiganaji mwenzie.

  "Mh kimaro amemuuliza swali PM Pinda kuwa serekali imelazimisha wakulima wa kahawa kutumia magunia ya katani huku magunia ya JUTE yanayotoka india na Bangladesh ni gharama nafuu na amemuomba waziri mkuu kutoa amri hiyo"katika hili PM amemjibu vizuri kuwa wanalinda viwanda vya ndani.

  Wana Jf nimeleta hoja hii kwakujaribu kuunganisha tukio hili la Kimaro na Uhusiano wake na Mh MWAKIEMBE.

  Kwa wafatiliaji wa mambo watakumbuka kuwa mwakiembe ndie aneagiza magunia ya JUTE toka INDIA kupitia kampuni yake ya TBC,na kwa hili pia inafahamika viwanda vinavyozalisha JUTE india vimepata soko la uhakika na kutengeneza ajira kwao ya watu zaidi ya laki tano,wakati mkonge hapa kwetu hauna soko nje baada ya soko letu kubwa la makampuni ya magari kuacha kununua bidhaa hii.

  Nachojiuliza isi out of Ignorance kimaro ameuliza au analinda maslahi ya Mwakiembe?itakumbukwa kuwa Mbunge wa Upinzani aneitwa Zitto Kabwe amekuwa akiitaka serekali kupitisha sheria ya matumizi ya bidhaa za mkonge ili kulinda zao hilo na viwanda vya magunia,pia itakumbukwa kuwa 2007 zito kabwe aliwahi kutaka kupeleka mswaada binfsi bungeni wa kutaka matumizi ya mgunia yanayotokana na mkonge liwe jambo la lazima lakini kwa uchanga wake wakati huo aliombwa na Mwakiembe asipeleke kwa hoja kuwa atakuwa ANAMSAIDIA MOHAMED ENTERPRISES kwani ndie mzalishaji mkuu na anaviwanda vingi vya magunia haina tija mswaada ukipita utakuwa unampa maslahi mtu mmoja,zito akachukua ushauri huo akaacha jambo ambalo naamini mpaka leo anajutia kwani Mutilplier effect ya mswaada/sheria hiyo ingekuwa kubwa pamoja ya kuwa MO ndie mwenye viwanda but ajira zingetengenezwa nyingi,wakulima wangepata soko,serekali ingepata kodi lakini hayao yamepita.

  Nacho jiuliza je kimaro hakujua kuwa ombi lake lingepeleka kabisa kaburini mkonge?au alikuwa analinda maslahi ya MWAKIEMBE? hebu wana JF tulijadili hili bila kuangalia maslahi/ya binafsi or kundi.

  naomba kuwasilisha.
   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  lakini kabla hatujaenda mbali ukweli ni kuwa huko nyuma ALOYCE KIMARO alielewa kama:

  3. Aloyce Kimaro – it baffles many that this semi-illiterate thug can even be a Member of Parliament. It speaks volume to the desperation of CCM to do anything, including recruiting thugs and former thieves, to win back opposition seats. The biggest comedy in the country at the moment is that this man is mentioned among principled Members of Parliament who can stand up and speak truth to power, including pointing a finger at Mkapa. Well, just few weeks ago he extorted a tender to guide VIPs to climb Mt. Kilimanjaro during the Sullivan Summit by threatening officials at the Ministry of Foreign Affairs that he will blast them in the Parliament. Pure blackmail.

  i rest my case
   
 3. M

  Mong'oo Member

  #3
  Jun 18, 2009
  Joined: Oct 13, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukiangalia kununua magunia ya mkonge kunafaidisha watu wengi zaidi kuliko kununua nje
  -Ajira
  -Kodi au pato la ndani. nk


  Upande wa pili

  Kununua magunia ya nje kuna faida kwa wakulima.

  -Bei ya magunia inakuwa ya ushindani. Bei ya chini.

  Sasa Mheshimiwa wa Vunjo nadhani anaangalia upande wa pili unafuu bei ya magunia kwa wakulima.

  Nakubaliana na kuboresha soko la ndani. lakini serikali iangalie upande wa wakulima namna ya kujazia hiyo gharama ya juu ya magunia.
   
 4. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  1.kwanza ni mwakyembe peke yake ndio anayoagiza hayo magunia.....
  2. pili mwambie metl aache ulanguzi na ashushe bei ya magunia yanayotokana na mkonge, embu fikiria mkulima wa tanga anauziwa gunia la mkonge bei mbaya kuliko lile JUTE linalotoka india... kuwalinda wa kulima ni mo kuwauzia magunia ya mkonge bei rais
  3. magunia ya jute yameanza kuuzwa TZ kabla ya mwakyembe na hamna ushindani kati ya metl na mwakyembe kwa ajili metl anapeleka asilimia kubwa ya mkonge wake NJE kwa ajili ya kutengenezea makapeti

  4. kama unaipenda nchi yako ungeuliza inakuwaje metl ameuziwa viwanda na mashamba kwa bei ya "nyumba"
   
Loading...