Mh. Kikwete, Tundu hatafuti umaarufu wa kisiasa!

CCM ni janga la kitaifa.
Mheshimiwa JK, nimekusikia ukiwahutubia majaji na kuwaombna samahani kuwa wanasiasa wanatafuta umaarufu na wala hujamchagua jaji ambaye ni jamaa yako kutoka barabarani. Let us be scientific, jibu hoja za Tundu Lissu moja baada ya nyingine. From there we will reach a just, reasoned conclusion.

1. Je yule jaji anayesoma first degree OUT, ana degree ya sheria kama sheria inavyotaka? Toa majibu na kwa hoja zingine.
2. Umepitia hukumu za hawa majaji uliowateua na kuzisoma kama zinakidhi matakwa ya kisheria ya hukumu?- umepima lugha wanayotumia kama ni kiingereza cha kisheria?
3. etc, etc,etc, etc,............................................................................

MAJAJI: JIHUKUMUNI WENYEWE:
1. SOMA HUKUMU ZA MAJAJI WA KIKWETE MTAUONA UKWELI WA LISU
2. MAADILI YA WENZENU YAJADILI MTAUONA UKWELI WA LISU

Kama alivyosema jaji Mihayo, afadhali kuwaachia watuhumiwa 10 walioua kuliko kumnyonga mtu mmoja ambaye hakuua! The opposite is the case with JK appointed judges
 
Hivi watu wengine Kweli mnatumia MASABURI kufikiri!!!

Degree ya OUT na UDSM hakuna tofauti na siyo issue kwenye mada hii. Issue ni kwamba huyo JAJI hata hiyo ya OUT HAJAISOMA NA KUIMALIZA, HANA degree yoyote bado anasoma huku akiwa JAJI ambapo ni kinyume cha sheria!!!

FIKIRI kwa kutumia mifumo sahihi.

Man mind your business.
 
ukweli ni kuwa Jk anaweza akashauriwa vibaya na watu wenye interest zao katika kufanya uteuzi. kusema kuwa hateui kutoka mabarabarani haimaanishi uteuzi hauwezi kuwa na makosa hasa hili la nepotism kupitia yeye mwenyewe na wengine
 
Sileti hoja ya kumpinga lissu,lakini tujiulize kwanza hivi lissu anayo orodha ya majaji mahili ambao hawakuteuliwa?pili hivi rais kikwete huwatoa wapi majaji anaowateua?tatu na mwisho tunamuomba mh.lissu atupe orodha ya majaji wote ambao ni feki ili wasiteuliwe tena,vilevile kuorodhesha majaji mahili wote ili iwe rahisi kuwatambua/kuwapendekeza.katika hili sioni sababu yoyote ya mh.lissu kumlazimisha mh.raisi kuwaondoa majaji aliowateua.katika hili sidhani kama mh.lissu anawatendea haki waliomchagua maana badala ya kukomalia masuala madogox2 ya kiuchumi na kijamii,yeye ni kupambana na sheria tu.
 
Mheshimiwa J. K. asipopigiwa kelele anaweza kaja rais mwingine akateua watoto wake wa A Level kuwa majaji kwa sababu tu wanasoma HGL ati kuwa ni dalili ya kuwa watasomea sheria!!!
 
Jaji ktk katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 109 kifungu cha 7 amewekewa sifa zake na hii ni pamoja na kuwa na shahada ya juu ya sheria kutoka chuo kinachotambuliwa. Jaji Mbarouk anayezungumziwa na anasoma sasa hivi OUT ametokea Zanzibar, ambapo kule alikuwa hakimu. Uhakimu Zanzibar unaweza kupata kutokana na uzoefu. Yaani ni mtu mwenye busara/hekima na anasaidia kusuluhisha - 'wakil' Aliingizwa rasmi kwenye mfumo huko Zanzibar ambako sheria haiweki masharti ya elimu kama katiba ya muungano.

Wakati tume inapitia mapendekezo ya majaji, suala la elimu ya Jaji mtarajiwa lilielezwa wazi, lakini pamoja na mapendekezo ya tume kumshauri Rais kuwa asimteua, yeye alimteua Mbarouk.

Hivyo tunamtaka Rais aache kuhadaa umma. Katika uteuzi wa majaji alikuwa hafuati ushauri wa tume na alivunja katiba. Pia katiba inasema Rais ndiyo anateua majaji na siyo tume - kwa hiyo kama wamarekani wanavyosema "The buck stops here!" Yeye ndo anawajibika kama rais - ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho si mwingine.

Inawezekana tatizo siyo anayeteua bali Katiba yenyewe. Katiba inampa Rais madaraka makubwa tena sana.

Kwa mfano, Ibara hiyo ya 109 inasema kwenye Ibara ndogo ya 7 kuwa "Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (9) ya ibara hii, mtu aweza tu kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ikiwa ana sifa maalum, kama ilivyofafanuliwa katika ibara ndogo ya (8) ya ibara hii, na awe mtu ambaye amekuwa na mojawapo ya sifa maalum kwa muda usiopungua miaka mitano.

Ibara ndogo ya 8 inasema kuwa "Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa ibara ndogo ya (7), ya (9) na ya (11) ya ibara hii, "sifa maalum" maana yake ni sifa zilizotajwa katika Sheria ya Mawakili (au Sheria nyingine yoyote inayobadilisha hiyo sheria ya Mawakili au inayotumika badala yake) ambazo ni lazima mtu awe nazo mojawapo ya sifa hizo ili aweze kukubaliwa kuandikishwa kama Wakili Tanzania Bara.

Ibara ndogo ya 9 inasema kuwa "Iwapo Rais atatosheka kwamba ijapokuwa mtu mwenye sifa mojawapo ya hizo sifa maalum hakuwa nayo sifa hiyo kwa muda usiopungua miaka mitano, lakini mtu huyo ana uwezo, ujuzi na kwa kila hali anafaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu na kuna sababu za kumfanya mtu huyo astahili kukabidhiwa madaraka hayo, basi Rais aweza kutangua lile sharti la kuwa na sifa maalum kwa muda usiopungua miaka mitano, na baada ya kushauriana na Tume ya Kuajiri ya Mahakama, Rais aweza kumteua mtu huyo kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Hapo unaweza kuona jinsi Katiba inavyompa Rais madaraka ya kuteua majaji kiasi kwamba anaweza kutangua lile sharti la kuwa na sifa maalum yaani degree ya sheria. Labda hapo unaweza kuhoji kama alifanya hivyo "baada ya kushauriana na Tume ya Kuajiri ya Mahakama", lakini kwa jinsi mambo yanavyoendeshwa nchi hii sishangai.

Kama Katiba isingempa Rais Madaraka ya kutangua lile sharti la kuwa na sifa maalum yaani degree ya sheria, then asingeweza kumteua jaji ambaye hana degree ya sheria. Whether Rais anatakiwa kutumia hayo madaraka reasonably, Katiba haisemi hivyo. Imempa unrestricted power. So, a better approach is to address the root cause of the problem.
 
kama katiba kwa makosa imempa madaraka makubwa kiasi hicho, je yeye busara zake binafsi ziko wapi? kwa nini kujiingiza kwenye controversy inayoepukika?
 
Mjinga huteua wajinga wenzake kama ambavyo mwizi anavyokuwa karibu na mwizi mwenzake, mhuni na malaya wake, mfanyabiashara na vitu mbalimbali anavyou nunua na kuuza. Mlitaka JK aende kinyume na sheria ya msingi kuwa ndege wenye mbawa zinafanana kwa rangi huruka pamoja???
 
Back
Top Bottom