Kwani digrii ya sheria ya OUT ina tofauti gani na ya UDSM?
Mheshimiwa Zakumi nafikiri hujailewa mada au unataka kupotosha maana makusudi.
Mtoa mada anasema Mh. J. K. kamteua jaji anaysema degree ya sheria OUT sasa. Sheria yetu inataka Lazima jaji awe na degree ya sheria anapoteuliwa. Huyu jaji ndo anaisomea hiyo degree. Hata kama angekuwa naisomea UDSM ilimradi hajaipata asingestahili kuteuliwa kuwa jaji.
Kimsingi degree ya sheria ya UDSM na OUT zinatakiwa ziwe sawa. Mtoa mada hajasema kuwa mtu akisoma OUT hastahili kuwa jaji ila kasema mtu ambaye hajapata degree hawezi kuteuliwa kuwa jaji bila kujali chuo anachosomea.