Mh. Kikwete, Tundu hatafuti umaarufu wa kisiasa!

we mkuu yaaani huwezi kuwa hata state attoney kama huna first degree ya sheria,yaani huo ujaji aliopewa ni jambo la kushangaza sana,only in Tanzania.

Kama unasema state attorney, Marekani haina first degree ya sheria.
 
Realman:

Natumia haki yangu. Watu wote ni muhimu katika jamii ndio maana katika nchi za wenzetu wamehamua kuwa vigezo vya shule kwa majaji wa ngazi zote ni sawa. Ukiashaanza kufanya kazi kitakachokupandisha juu ni performance yako ya kazi na sio shule tena.

mkuu acha kukariri,sio kwa fani zote wanaangalia perfomance kwanza,cheti pia kina nafasi yake,mfano marekani huwezi kusoma sheria as a first degree,lazima ume na degree nyingine ya fani nyingine ndipo usome school of law.
 
Sasa unataka kusema kuwa Arusha hipo Zanzibar? Soma hiyo quote chini.
Mkuu ni mimi niliyejichanganya, Mbarouk anatokea Zanzibar na sio Arusha.
But kuna another judge anatokea Arusha ambaye yumo kwenye orodha ya majaji vihiyo walioteuliwa na JK hivi karibuni ambaye nimemchanganya na huyu Mbarouk.

Sorry for inconvinient!!
 
Kama unasema state attorney, Marekani haina first degree ya sheria.

najua hilo ina school of law na ina criteria zake.tunaangalia bongo mkuu,sisi tunafata mfumo wa sheria wa uingereza,mkoloni aliyetutawala..
 
Nakuomba google maana ya diploma.

Unamaanisha Diploma katika 'qualifications' za Tanzania? Labda nikuulize, kwanini waliweka Degree kama sehemu ya qualification ya jaji (kwa Tanzania) na sio Diploma? Hawajui tofauti ya Diploma na Degree?

Yote tisa, kumi, utendaji wa majaji wasio na sifa stahiki umeonekana. Hukumu zao zimejaa utata na wengine wameshindwa kuandaa hukumu! Hivi inaingia akilini kwa jaji kuchukua zaidi ya miaka 2 kuandaa hukumu? Huo ndio utaratibu mzuri wa kutoa HAKI?
 
Baada ya kusoma posti nyingi hapa inaonyesha kuwa jamaa anayo digrii ya kwanza ambayo sio ya sheria na postigraduate ya sheria. Na vilevile amefanya kazi kwa muda mrefu. Sioni kitu tatizo lolote hapo.
 
Mkuu ni mimi niliyejichanganya, Mbarouk anatokea Zanzibar na sio Arusha.
But kuna another judge anatokea Arusha ambaye yumo kwenye orodha ya majaji vihiyo walioteuliwa na JK hivi karibuni ambaye nimemchanganya na huyu Mbarouk.

Sorry for inconvinient!!

No problem, Let us move on.
 
Nchi nyingi siku hizi hazitoi digrii ya kwanza ya sheria. Kwa hiyo hata hao majaji watanzania itabidi waangalie upya.

Unapoongelea 'academic qualifications' ni lazima uzingatie mazingira ya sehemu husika (context). Baadhi ya nchi hawana neno 'Degree' wao wanatumia neno Diploma. Kwa Tanzania tuna Diploma na tuna Degree.

Kwenye red, nchi nyingi, especially nchi nyingi zinazofuata Commonwealth Judiciary System (Tanzania included) zinatoa DEGREE ya kwanza ya sheria.
 
Unamaanisha Diploma katika 'qualifications' za Tanzania? Labda nikuulize, kwanini waliweka Degree kama sehemu ya qualification ya jaji (kwa Tanzania) na sio Diploma? Hawajui tofauti ya Diploma na Degree?

Yote tisa, kumi, utendaji wa majaji wasio na sifa stahiki umeonekana. Hukumu zao zimejaa utata na wengine wameshindwa kuandaa hukumu! Hivi inaingia akilini kwa jaji kuchukua zaidi ya miaka 2 kuandaa hukumu? Huo ndio utaratibu mzuri wa kutoa HAKI?

Katika vipengere vya kuwa jaji mlivyovileta vinasema mtu afanye kazi miaka 15. Je hao majaji walipokuwa mahakimu walitoa hukumu vipi? Kumbuka wengine walikuwa mahakimu wakati Mwinyi ni raisi wa nchi. Je waliwatendea watu haki kivipi?

Mnataka kuweka standard za juu kwa mahakama za juu wakati mnapigana vichwa mahakama za chini?
 
Nchi nyingi siku hizi hazitoi digrii ya kwanza ya sheria. Kwa hiyo hata hao majaji watanzania itabidi waangalie upya.

Una maana gani kuwa nchi nyingi hazitoi degree ya kwanza ya sheria? Ni hivi acha kuchanganya wanaposema degree ya kwanza ya sheria maana yake uwe umesoma degree ya sheria kuanzia masomo ya awali, mfano Marekani na Australia unapoenda kusoma degree ya sheria lazima uwe na degree kwanza ya kada yeyote ile yaani ukienda kusoma degree ya sheria pamoja na kwamba unadegree nyingine mathalani biashara au uchumi au uhandisi utakapoingia kusoma degree ya sheria utaanza mwanzo kabisa kama nchi zingine ambazo mtu kuingia degree ya sheria awe kamaliza high school kwa Marekani na Australia kuwa na degree kwanza kabla hujasoma sheria ni qualification ambazo wao wameamua kuzifuata kwahiyo bado huyo mtu atakuwa kasoma degree ya kwanza ya sheria pamoja na kuwa alikuwa na degree nyingine maana haitapandilia kwa juu kuitwa masters bali itakuwa sambamba katika urali lakini kwasababu alikuwa na degree pia basi yeye hataitwa LLB bali ataitwa JD yaani Juris Doctor lakini pamona na hayo muda wa kusoma hiyo degree ya sheria atasoma kwa miaka ya kutosha kuanzia mitatu mpaka minne tofauti na post graduate ni mwaka mmoja umedondoa tu sheria huendi deep.

Vinyo hivyo hata udaktari katika Marekani huingii kwa kutokea high school lazima uwe na degree nyingine yeyote ile ndio unaanza kusoma medicine ni utaratibu wamejiwekea katika kada hizi mbili kuhakikisha watu wanaohitimu wameiva ili kutokuwa na vihiyo maana kada hizi zinagusiana na masiha ya mwanadamu ya kila siku moja kwa moja hiyo ni kwa mujibu wao sio mimi mie nawakilisha
 
Kwani digrii ya sheria ya OUT ina tofauti gani na ya UDSM?

alichoongea mdau hapo na kama umeelewa ni kwamba huyo jaji hana digrii ya sheria ila ndo kwanza yupo chuoni Out anaitafuta,there4 tuna jaji ambaye hana digrii ya sheria
 
Soma tena hapa na kazia zaidi hapo kwenye bold.

2/Uwe na Degree ya kwanza ya Sheria kutoka katika chuo kikuu chochote duniani inayotambulika na kukubalika na Common Wealth Judiciary System.

Judiciary system ya Urusi ni tofaufi na 'Commonwealth'. Nchi zinafuata Commonwealth judiciary system kwa lugha nyepesi na kwamba sheria zao zina-base kwenye sheria za Uingereza.

Jamaa ni hakimu wa mkoa. Na anatumia sheria za Tanzania kutoa hukumu kwa zaidi ya miaka kumi. Kupata ujaji utasema lazima awe na digrii ya Commonwealth judiaciary system. Kwenye uhakimu anatumia Commonwealth judiaciary system.

Kwenye nchi yenu ina vichwa.
 
Ni vitu gani vinakufanya utambue kuwa chuo husika kinatambulika kutoa digrii ya kumfanya mtu awe jaji. Kuna rafiki yangu kasoma Urusi na ni hakimu Tanzania. Je unataka kuniambia kuwa uzoefu wake na digrii yake havitoshi kumfanya awe jaji?
Mkuu tukiachilia vigezo vingine vya msingi vya mtu kuwa jaji na kujikita kwenye issue ya Bachelor of Law pekee ni kwamba;

1/Mifumo ya kisheria duniani kote inatofautiana sana hivyo hata mafunzo ya kimsingi ya kisheria yanatofautiana sana.

2/Nchi zilizo chini ya jumuiya ya Madola zina mfumo wa kisheria unaoshahabiana sana hivyo mafunzo ya mwanzo yanafananafanana.

3/Chuo chochote duniani huwa kinajieleza ni mfumo upi kinatumia katika kutoa mafunzo ya kisheria hivyo kabla ya kwenda kusoma chunguza hilo kwanza.

4/Russia ina vyuo vingi na mifumo mingi ya ufundishaji kulingana na soko la ulimwengu(International Student) hivyo huyo rafiki yako sijui amesomea mfumo upi lakini kwa kuwa ameajiriwa kwenye mahakama za Tanzania basi inaonekana Degree yake ametambuliwa na kukubalika katika mfumo wa sheria za jumuiya ya madola hopeful ipo siku atakuwa jaji.
 
Katika vipengere vya kuwa jaji mlivyovileta vinasema mtu afanye kazi miaka 15. Je hao majaji walipokuwa mahakimu walitoa hukumu vipi? Kumbuka wengine walikuwa mahakimu wakati Mwinyi ni raisi wa nchi. Je waliwatendea watu haki kivipi?

Mnataka kuweka standard za juu kwa mahakama za juu wakati mnapigana vichwa mahakama za chini?

Kama mahakama za Wilaya zina jaji vihiyo, then huku juu nako kuna jaji vihiyo hapo tuna Mahakama? Just think about it na ndio utajua umuhimu wa kuwa na jaji wenye 'proper' qualification - walau huku juu! How would you feel kama umetuhumiwa kuuwa mtu halafu kesi yako ikawa chini ya jaji ambaye sifa zake (za ujaji) zinatiliwa shaka?

It is easy for us to debate, lakini kuna watu hatma za maisha yao zimo mikononi mwa watu wanaotiliwa shaka!
 
alichoongea mdau hapo na kama umeelewa ni kwamba huyo jaji hana digrii ya sheria ila ndo kwanza yupo chuoni Out anaitafuta,there4 tuna jaji ambaye hana digrii ya sheria

Anayo digrii ya kwanza ambayo sio ya sheria lakini posti ni ya sheria.
 
Jamaa ni hakimu wa mkoa. Na anatumia sheria za Tanzania kutoa hukumu kwa zaidi ya miaka kumi. Kupata ujaji utasema lazima awe na digrii ya Commonwealth judiaciary system. Kwenye uhakimu anatumia Commonwealth judiaciary system.

Kwenye nchi yenu ina vichwa.

Corrections: Alikuwa jaji wa Wilaya (sio mkoa). From Wilaya moja kwa moja hadi juu (bila ya kuwa degree).
 
Back
Top Bottom