Mh Kikwete, Tunaomba Noti ya Laki Moja Mkuu (100,000) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh Kikwete, Tunaomba Noti ya Laki Moja Mkuu (100,000)

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Amoeba, Nov 8, 2011.

 1. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Wachumi sijui wataelezaje hali ya uchumi inavyoendelea nchini kwetu hivi sasa, pesa yetu inaporomoka kwa kasi ya ajabu sambamba na kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali na gharama za maisha kwa ujumla. Kwa mwannanchi wa kawaida kama mimi inabaki maumivu, lakini maumivuu hayo hayanizuii kuendelea kupigania maisha; kwani nikilegeza kamba tu watu wanapita kwa mgongo wangu, tena kwa kasi ya ajabu kama mtoto wa Mkuu anavyoibuka na mafanikio makubwa ya kiuchumi ndani ya muda mfupi. Namaanisha kwammba; nitaendelea na mapambano-NO MATTER WHAT, ili kurahisisha kidogo mapambano yangu, Ni ombi langu kwa Mkulu aangalie uwezekano wa kuchapa noti ya Laki Moja, hata ikiwa kwa kiwango kama cha noti hizi mpya ambazo naona sasa wanaziondoa kwenye mzunguko kimyakimya, si unajua tena kuchapa noti za maana ni gharama, halafu vilevile zinaweza kuwanyima wakina fulani uwezekano wa kuchomeka kwenye mzunguko noti zao wanazzotengeneza paleee mitaa fulani! Kama bado haujaelewa namaanisha nini ngoja nijaribu kueleza kwa mifano; Lat week nilikuwa huku kwetu mabonde kuinama mkoa wa kusini katika wilaya ambayo ni makao makuu ya Mkoa huu, nina kaproject ambako naona kanasuasua kila mwaka kutokana na hali ngumu ya uchumi, basi mwaka huu nikawa nimeppishana na dili nzuri ya kuwapangija jamaa fulani wametoka mashariki ya Mbali, jirani yangu mmoja akawa ananicheka nimefulia, nikaingiwa na hasira na kuamua kwenda kununua mifuko 350 ya cement muda huohuo, unajua nilinunua bei gani kwa mfuko?....21,000/=! ndiyo....cement sasa hivi inauzwa bei hiyo huku! ndiyo kusema 350x21000=7,350,000 mifuko mia 350tu! Kichekesho huyo muuzaji akadai hanifahamu, hvyo anataka "keshi", unajua hiyo pesa nilibebea kwenye nini?.....RAMBO! Najua siyo wote tuliojaliwa kuelewa kwa mifano, hivi unajua huku niliko kilo moja ya nyama ni bei gani?......elf12000!!!..ee ndiyo, wafugaji wanadai dola imepanda!!!! Sitaki kuorodhesha bei ya vitu viiingi ntawatia watu uvivu wa kusoma buree, wakati kinaeleweka kabisa kwa sisi wakina kapuku ukitoka home na kashilingi elf20 kako mfukoni ujue jioni utarudi home kwa miguuu!...ndiyo, 20 yote maji ya kunywa na mihogo ya kuchoma, kwishnei, hata nnauli!!!!

  Aaaaargh, wacha niishie hapa; nguruwe huko nje wanalia balaa sjui kama chakula chao bado kipo. Ah!...Mh. Kikwete, im serious with this one; tunataka noti ya laki!...usione aibu baba Ritz! Naona mke wangu ananitolea macho hapa, yeyye ni ticha anasema; "ina maana mimi mshahara wangu utakukwa noti moja tu!" eee ndiyo, noti moja laki na kama mshahara wako ni laki chunga sana, usije ukaweka mfukoni baadae ukajisahau ukapengea kamasi!..au wakat unatoa leso kanoti kakadondoka ukabaki empty majalala- WANAO WATAKULA NYASI MWEZI MZIMA!
   
 2. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Huu ni ushauri murua kabisa, watengeneze pia noti za 20,000 na 50,000
   
 3. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Mimi nimetengeneza tolori umbo lake linafanana na yale magari ya kampuni za ulinzi yanayobeba fedha kupeleka kwenye mabenki na ATM,siku hizi siweki hela tena kwenye soksi kama zamani ,haiwezekani au itabidi niwe kama kile kibonzo cha matairi ya Michellin
   
 4. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Mkuu, hii shilingi yetu sasa ni makaratasi yasiyo na thamani yoyote! Tunatembea na rundo lamakaratasi kwenye wallets!
   
 5. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe mkuu, waache kuona aibu; huku wananchi tunateseka bana, elf5 iwe noti ndogo kabisa, hizo nyingine ziwe coins tu-2000,1000,500,200,100,50-hivi kwanza hamsini na mia bado zinatumika?
   
 6. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  halafu ili kuepuka gharama zaidi wazichapishie china
   
 7. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Ni kweli mkuu, China Manufacturers wanaweza kutuchapisha kwa bei nafuu sana; hizi noti walizochapisha last time n vichekesho vitupu, hapa nilipo naiangalia mia tano mpya ilivyochoka-kuna huu uzi wa security uliopo upande wa kulia-nadhani walichomoa kwenye ile mifuko ya mbolea ndy wakatumia katika hizi noti!!! SAFARI NI NDEFU!
   
 8. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #8
  Nov 8, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  • bado anakula ubwabwa na prince charles
   
 9. mwanawao

  mwanawao JF-Expert Member

  #9
  Nov 8, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 1,982
  Likes Received: 1,639
  Trophy Points: 280
  Me kinachoniuma ni kwa nini shilingi ya tanzania tu? Me nahisi wachumi wanaomshauri Rais kuna haja ya kuachishwa kazi wawekwe watu watakaweza kuja na mbinu yakinifu zitakazoweza kukomboa uchumi wa tanzania
   
 10. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #10
  Nov 8, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Yaani kwa sisi mabachela kwa siku unatumia 15,000 au 20,000 kwa chakula tu!!!
   
Loading...