Mh. Kikwete Pongezi Ulizozipata Usije Ukaharibu Tukakuchukia Zaidi

jnuswe

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,270
549
Wana JF

Nianze kwa ku declare interest kuwa mimi kwa upande wa masuala ya siasa niko upinzani lakini kuwa mpinzania haina maana ya kukosoa kila kitu hata pale panapostahili kupongeza

Mh. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa awamu ya nne, katika jambo ambalo utakumbukwa ni kurusu uundwaji wa katiba mpya ya nchi yetu, hilo ni jambo zuri sana ulilolifanya mpaka hatua hii.

Lakini yameanza kusikika masikioni mwa watu na baadhi ya vyombo vya habari vimeeleza kuwa CCM watakuwa na kikao maalum cha kuijadili rasimu ya Katiba mpya chini ya unyekiti wa mweshimiwa Rais. Mimi sijaona popote katika mchakato wa uundwaji wa katiba inapoelezea vyama vya siasa vitakaa rasimi na kujadili rasimu ya katiba. Kwa kazi hiyo yapo mabaraza ya katiba na bunge la katiba na si vyama vya siasa.

Chonde chonde rasimu iliyopo angalau imekidhi haja ya mioyo ya watanzania, tunawaombeni CCM msije mkatualibia mchakato na kuipeleka nchi katika machafuko yasio ya lazima
 
mkuu tuombe mungu mambo yaende vema vyama vya siasa vyote vitajadili hii rasimu kwa sababu vyama vya siasa ni taasisi na wanauhuru wa kujadili kama ambavyo zitafanya taasisi zingine zilizopo hapa nchini.
 
kikwete ni mtu muungwana mno, hawezi kufanya kitu cha kumharibia wakati ameshafanya mengi mazuri ya kupigiwa mfano hadi hapo alipofikia
 
wakati wa utawala wa JK kumekuwa na uhuru mkubwa sana wa kutoa maoni, uhuru wa kukosoa na uhuru wa kuzungumza mtu atakalo...........tuutumie uhuru huu kuijenga tanzania yetu
 
Kishukuriwe kwanza chama kilicho ona mbali na kuamua kuweka swala la Katiba kama sera yao namba moja.....Kwa maneno mengine tunaishukuru Chadema na pia tunaishukuru CCM pamoja na JK kwa kutekeleza Ilani ya CDM....
 
Huu ndiyo uungwana wa JMK kwa kuwa angeweza kukataa kutekeleza ilani ya CDM na bado akabaki kuwa rais. Big Up prezzida.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom