Mh.kikwete na majeshi yako ya ulinzi na usalama v/s nguvu ya umma ni sawa na daudi v/s goliati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh.kikwete na majeshi yako ya ulinzi na usalama v/s nguvu ya umma ni sawa na daudi v/s goliati

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DOUGLAS SALLU, Nov 16, 2011.

 1. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,635
  Likes Received: 4,746
  Trophy Points: 280
  Kwako Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kikwete, serikali yako kwa kipindi kirefu sasa imekuwa ni serikali ya kibabe, kidhalimu na kikandamizaji. Damu nyingi imeshamwagika tangu umeingia madarakani.

  Kila mahali ambapo watu walisimama kidete kudai haki zao serikali yako imeona jibu sahihi ni kutumia mabomu ya machozi, maji ya upupu na hata risasi za moto. Rejea yaliyotokea kule Arusha mwanzoni mwa mwaka huu amabapo watu watatu wasio na hatia walipigwa risasi na kuuawa na polisi wako katika maandamano ya amani yaliyoandaliwa na Chadema kupinga uhuni uliofanyika kwenye uchaguzi wa meya wa Arusha.

  Kule Nyamongo wanachi wasio na hatia waliuawa kwa risasi na polisi wako kisha maiti zao kwenda kutupwa barabarani na polisi hao wauaji.
  Kama vile haitoshi, katika uchaguzi mdogo kule Igunga polisi wako walitumika kwenda kubaka demokrasia hadi kupelekea watu wengi kuumizwa na pia wakala wa Chadema kuuawa kikatili.

  Mwanzoni mwa wiki iliyopita polisi wako walirudia tena ushenzi wao kwa kuwashambulia wana Chadema walioamua kukesha kwa amani kwenye viwanja vya Unga Ltd kule Arusha. Kama vile somo halijaeleweka huko Mbeya nako Polisi wako waliendesha zoezi la kuwa piga kikatili kwa mabomu na risasi za moto wamachinga waliokuwa wakisimamia haki zao kuondolewa kwenye maeneo ya kufanyia biashara kwa maelekezo ya Dikteta Kandoro.

  Kule Mbeya ngoma ilikuwa nzito kwa polisi wako hadi kuomba msaada wa JW na JKT, lakini hata hivo mitutu ya bunduki na mabomu haikufua dafu, mwisho wa siku nguvu ya umma ilishiinda.

  Somo ninalotaka kukupa Mh. Raisi ni kuwa Tanzania ya leo siyo ile ya enzi ya chama kushika hatamu, wanachi wamesha pata ujasiri wa kudai haki zao kwa gharama yoyote ile, na wameshajua kuwa utawala wako ni utawala wa ghilba na mabavu na sasa hawako tayari tena kusikiliza ghilba za CCM, ndiyo maana wamekuwa wakiitikia kwa moyo mmoja maandamano na mikutano ya Chadema bila kubebwa na na kulipwa hela ili kuhudhuria kama mnavyofanya CCM.

  CCM mna majeshi ya ulinzi na usalama, lakini Chadema wana umma wa Watanzania katika mioyo yao, sasa hizo silaha zenu haziwezi kunyamazisha mamilioni ya watz, ni kama vile kijana mdogo Daudi katika Biblia ambaye hakuwa na ujuzi wowote wa vita akitokea kuchunga kondoo, lakini kwa vile alikuwa mpakwa mafuta wa Bwana aliweza kumuua kirahisi jemadari Goliati wa jeshi la adui.

  Kama alivyoanguka Goliathi ndivyo utawala wako wa mabavu utakavyoangushwa na nguvu ya umma. Na hizo silaha mnazotegemea kutuulia sisi umma wa watz ndiyo hizo hizo zitakazowageukeni kwani hao askari mnowatuma kutuua siyo roboti , ni binadamu ambao nao ni wahanga wa ufisadi unaofanywa na genge lako.

  KAMA MUNGU AISHIVYO UTAWALA DHALIMU WA CCM LAZIMA UTAANGUKA KWA KISHINDO KIKUBWA.
   
Loading...