Mh. Kikwete: Kosa ni kulinda, kurudia na kuendeleza Makosa

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Mheshimiwa Rais Kikwete,

Waswahili wanasema kosa ni kurudia kosa. Hapo hukumu yakupasa!

Kwa uwanja wa siasa na nafasi yako ya Urais wa Jamhuri na Mwenyekiti wa CCM, Kosa ni kulinda makosa, kurudia makosa na kuendeleza makosa!

Nimekushikia bango sana, nimekukebehi, nimejaribu kukupa fununu ya njia bora ya kujiondoa katika matatizo, lakini natambua kuna moja ambalo sikulifanya nalo ni kukupa tahadhari kuwa "kulinda, kurudia na kuendeleza makosa" ni kosa kubwa sana na ndio msingi wa Taifa letu kushindwa kuendelea na kupaa kiuchumi kwa kutumia rasilimali zake.

Ulipokutana na Wazee wa Dar, ulimtetea aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa eti alikuwa ni mchapa kazi na unasikitika kuanguka kwake. Naomba ujiulize, ulitoa kauli hiyo ukiwa mzima kabisa bila kiluweluwe cha kizunguzungu?

Maana ulichofanya ni kuutangazia umma kuwa ulikuwa umeridhika kabisa na utendaji kazi wa Bwana Lowassa na hata kujiuzulu kwake haukufurahia!

Ikiwa Lowassa kama Waziri Mkuu alidiriki kufanya uzembe wa hali ya juu na kuliingiza Taifa katika mkataba hewa, je inkunkuwaje umtete?

Tayari tunajua hiyo kampuni ilikuwa imetiliwa mashaka katika utawala wa Mzee Mkapa, sasa zile ishara za ubomu wa Kampuni hii Richmond hazikuwashitua wasaidizi wako wote?

Njoo mradi wa kuchota pesa Benki Kuu, pesa zimetafunwa, lakini yaelekea walioharibu wanaendelea kupeta. Sasa hivi kuna ATC, Muhimbili na bado Kiwira zinatusumbua. Je bado unaridhika na yanayotokea?

Ikiwa utasema na kwa vitendo una ungana na wapambe wako wanao dai eti "mbona Nyerere, Mwinyi na Mkapa" walikuwa na makosa na udhaifu, basi tujiulize kama Taifa ni kwa nini tukupe tena kura zetu 2010 ili uendeleze makosa?

Tafadhali sana mnapokaa Butiama, mjisafishe roho. Ikiwa maswahiba zako wa karibu Lowassa na Rostam wamepakwa matope mazito ya mfinyanzi, tukueleweje sisi wananchi?

Tunakupa fursa na nafasi mpya ya kuja na kutuambia ukweli. Njoo tuambie ukweli, ungama tukusamehe na uongoze nchi kwa mujibu wa Sheria na Katiba.

Kinyume cha hili ni kurudia makosa, kulinda makosa na kuendeleza makosa hivyo wewe utakuwa mkosefu!
 
Rev. umesema kweli kabisa katika hii article yako. Kama Tanzania tungekuwa na kipengele cha katiba kinachoruhusu kumpigia Rais aliye madarakani kura ya kutokuwa na imani naye basi mimi ningeshiriki kati akampeni ya kuwahamasisha wananchi wampigie kura ya kutokuwa na imani naye. Sasa hivi sio usanii tena inaelekea he just don't care about the direction of Tanzania. How can you care when all culprits who are involved with stealing of $133 million are enjoying their freedom while the majority of Tanzanians are still suffering? :confused:
 
Bubu,

Kipengele hicho kipo kwenye katiba na Bunge likiahiri, linaweza kufanya hivyo. Tatizo si kumuondoa madarakani tuu, bali ni lini tutakuwa na Viongozi ambao wataachana na utamaduni wa kulinda, kureudia na kuendeleza makosa?

Ikiwa twasema MWalimu Nyerere na sera zake za Ujamaa tuliishia kuwa Maskini, je kwa nini hatujajifunza kutokana na makosa na udhaifu wake? Ikiwa tunasema mwalimu Nyerere ndiye alileta utamaduni wa kulea viongozi wabovu, kwa nini tunaendeleza libeneke la kulea viongozi wabovu wasikokuwa tayari kukiri makosa na udhaifu wao?

Mzee Mwinyi akaja na Ruksa, tukasema yeye na Azimio la Zanzibar ndio lilifungulia mafisadi. Je iweje Mkapa na Kikwete waendelee kuruhusu uhujumu na ufisadi wa waziwazi uendelee, je ni halali nasi kana taifa tukubali leo Kikwete au Mkapa au Mwinyi wakiendelea kunyooshea vidole yule aliyekuwa madarakani kabla yao kuwa vilianza na Mwalimu, vilanza wakati wa Mwinyi, Mkapa ndiye aliruhusu, kwa nini wewe Kikwete usisitishe mkondo endelevu ambao ni mbovu na unaangamiza Taifa?

Ndio maana namuomba sana akae chini na kutafakari. Alipogombea alisema ilimchukua muda kujifunza mengi ili awe Rais. Je alijifunza kulea makosa?
 
Mheshimiwa Rais Kikwete,

Waswahili wanasema kosa ni kurudia kosa. Hapo hukumu yakupasa!

Kwa uwanja wa siasa na nafasi yako ya Urais wa Jamhuri na Mwenyekiti wa CCM, Kosa ni kulinda makosa, kurudia makosa na kuendeleza makosa!

Nimekushikia bango sana, nimekukebehi, nimejaribu kukupa fununu ya njia bora ya kujiondoa katika matatizo, lakini natambua kuna moja ambalo sikulifanya nalo ni kukupa tahadhari kuwa "kulinda, kurudia na kuendeleza makosa" ni kosa kubwa sana na ndio msingi wa Taifa letu kushindwa kuendelea na kupaa kiuchumi kwa kutumia rasilimali zake.

Ulipokutana na Wazee wa Dar, ulimtetea aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa eti alikuwa ni mchapa kazi na unasikitika kuanguka kwake. Naomba ujiulize, ulitoa kauli hiyo ukiwa mzima kabisa bila kiluweluwe cha kizunguzungu?

Maana ulichofanya ni kuutangazia umma kuwa ulikuwa umeridhika kabisa na utendaji kazi wa Bwana Lowassa na hata kujiuzulu kwake haukufurahia!

Ikiwa Lowassa kama Waziri Mkuu alidiriki kufanya uzembe wa hali ya juu na kuliingiza Taifa katika mkataba hewa, je inkunkuwaje umtete?

Tayari tunajua hiyo kampuni ilikuwa imetiliwa mashaka katika utawala wa Mzee Mkapa, sasa zile ishara za ubomu wa Kampuni hii Richmond hazikuwashitua wasaidizi wako wote?

Njoo mradi wa kuchota pesa Benki Kuu, pesa zimetafunwa, lakini yaelekea walioharibu wanaendelea kupeta. Sasa hivi kuna ATC, Muhimbili na bado Kiwira zinatusumbua. Je bado unaridhika na yanayotokea?

Ikiwa utasema na kwa vitendo una ungana na wapambe wako wanao dai eti "mbona Nyerere, Mwinyi na Mkapa" walikuwa na makosa na udhaifu, basi tujiulize kama Taifa ni kwa nini tukupe tena kura zetu 2010 ili uendeleze makosa?

Tafadhali sana mnapokaa Butiama, mjisafishe roho. Ikiwa maswahiba zako wa karibu Lowassa na Rostam wamepakwa matope mazito ya mfinyanzi, tukueleweje sisi wananchi?

Tunakupa fursa na nafasi mpya ya kuja na kutuambia ukweli. Njoo tuambie ukweli, ungama tukusamehe na uongoze nchi kwa mujibu wa Sheria na Katiba.

Kinyume cha hili ni kurudia makosa, kulinda makosa na kuendeleza makosa hivyo wewe utakuwa mkosefu!

Rev.Kishoka
Umesha sema yote mimi sina la kuongeza nitaendelea kusoma michango ya wenzangu .
 
Tunarudi pale pale tu:
Namna pekee ya kupata mabadiliko ya kweli ya kisiasa na kiuchumi Tanzania ni Msajiri wa Vyama vya Siasa nchini kukifuta chama cha Mapinduzi.

Sababu ni hizi:
Chama cha Mapinduzi kimejivisha madaraka makubwa sana. Amini usiamini chama hiki kina nguvu kuliko Bunge, Serikali, Mahakama au chombo kingine chochote hapa nchini.
Chama hiki kina uwezo wa kuvunja sheria yoyote ya nchi bila kufanywa lolote na yeyote. Kina uwezo wa kuvunja sheria ya nchi halafu kikaliagiza jeshi la polisi na mahakama nini cha kufanya!
Viongozi wake wanaweza kukaa miaka 5 bila kufanya lolote la maendeleo kwa taifa, halafu wakati wa uchaguzi wakamwagiza mtu au taasisi yeyote ikipe chama fedha na mtu huyo akashinda uongozi tena.
Chama hiki pia kimetambua kuwa namna ya kuendeleza ufisadi ni kuhakikisha kwamba watanzania wanaendelea kuwa maskini siku zote ili wawe waoga na wasiwe na hoja. Ukiwapa sh. 10,000 au 100,000 umepata uongozi bila maswali!
Umaskini wa watanzania sio swala la hali ya nchi au hali ya hewa. Ni wale wanaojiona wajanja wachache sana wamepanga hivyo!
Chama hiki pia kinatisha. Wanachama wake ambao wangeweza kuwa viongozi wazuri (na kinao wengie kimewaficha) wanagwaya kukohoa (kusema ukweli kwenye matatizo) au kutoka kwenye chama hiki. Kupata uongozi Tanzania sio kwa sifa za utendaji bali ni kwa jinsi unavyoweza kutii wakubwa hata kwa jambo ambalo ni kinyume kabisa na maadili au hekima za kawaida za binadamu.
Kimelifanya jambo la kutoka kwenye chama kama kosa la ki-ugaidi. Hivyo wengi hawathubutu!
Lakini kina wanachama ambao wanaweza kuwa viongozi wazuri sana na watendaji wazuri sana kama nchi yetu ingekuwa na uhuru na demokrasia ya kweli. Lakini watu hawa wamezidiwa nguvu na Chama hiki.
Chama hiki kimekuwa ni taasisi iliyo mbele kuvunja sheria za nchi kuliko mtu au taasisi yeyote nyingine.

Namna ya kuleta mabadiliko ya kweli ni kukifuta chama hiki kwa sababu ya ufisadi na uvunjaji wa sheria za nchi uliokithiri ili wanachama wake watawanyike kwenye vyama mbali mbali na kuwe na balance ya nguvu za kufanya maamuzi za kisiasa.
Kwa matendo yake chama hiki hakina tofauti na mtu anayeanzisha chama kwa sababu za ugaidi au ufisadi - HASTAHILI. CCM HAISTAHILI pia. TUIWEKE KWENYE JUMBA LA MAKUMBUSHO kwa kumbukumbu na historia yetu watanzania. Sasa hivi hamna lolote jipya ndani ya CCM.
Kumbuka silaha yao kubwa ni wingi wao. Na hatari moja ya "demokrasia" ndio hiyo: kura nyingi ndio ushindi. Wendawazimu wakiweza kujiunga kwa wingi wakawa wanafanya maamuzi yao ya kiuchizi-uchizi (ukiwahoji machizi hao watakwambia kwamba ni demokrasia ndiyo inatumika), nchi hiyo ina hatari mpaka litokee kundi jingine litakolokuwa kubwa zaidi na lenye nguvu za kisiasa.
Kwa Tanzania kundi jingine ni vigumu kujiandaa na kuizidi nguvu CCM kwani CCM wataingiza mamluki wao na muda si mrefu mnaanza kuulizana “nani kajamba", “nani kajamaba" bila kupata jibu.
Kumbuka Chama hiki kina uwezo wa kuiagiza mahakama au polisi kitu chochote kile, kwa hiyo hamna pa kwenda. Ni kama vile kuwa kinyume na CCM ni sawa na kuwa kinyume na dola. Vyombo hivi ndio ambavyo vingetusaidia kujenga uswa na haki na demokrasia ya kweli (kama ipo) lakini vinashirikiana na CCM kuvunja sheria za nchi na kuwantika wananchi haki zao za kisheria.
Kama hatuwezi kupata hayo yote kwa sababu ya kuwepo fisadi CCM kwa nini tusitatue tatizo letu kubwa kwanza - kufuta CCM halafu tujenge taifa.

Nilipotoa hii mada mtu mmoja (sijui mwana-CCM yule) akadai nipunguze hasira. Kuna nini la kufurahia hapa sasa?
 
Uvumilivu Unamwisho Wake Whether You Like It Or Not One Day Things Will Turn Upside Down.tunaelekea Mwisho Wa Uvumilivu,tukifika Mwisho Wa Uvumilivu Sijui Ni Nini Kitafuata.
 
Mheshimiwa Rais Kikwete,

Ulipokutana na Wazee wa Dar, ulimtetea aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa eti alikuwa ni mchapa kazi na unasikitika kuanguka kwake. Naomba ujiulize, ulitoa kauli hiyo ukiwa mzima kabisa bila kiluweluwe cha kizunguzungu?

Maana ulichofanya ni kuutangazia umma kuwa ulikuwa umeridhika kabisa na utendaji kazi wa Bwana Lowassa na hata kujiuzulu kwake haukufurahia!

Ikiwa Lowassa kama Waziri Mkuu alidiriki kufanya uzembe wa hali ya juu na kuliingiza Taifa katika mkataba hewa, je inkunkuwaje umtete?

Tayari tunajua hiyo kampuni ilikuwa imetiliwa mashaka katika utawala wa Mzee Mkapa, sasa zile ishara za ubomu wa Kampuni hii Richmond hazikuwashitua wasaidizi wako wote?

Njoo mradi wa kuchota pesa Benki Kuu, pesa zimetafunwa, lakini yaelekea walioharibu wanaendelea kupeta. Sasa hivi kuna ATC, Muhimbili na bado Kiwira zinatusumbua. Je bado unaridhika na yanayotokea?

Ajitokeze mtu mwnye akili timamu atuonyeshe wapi Raisi alijitokeza na kukemea kwa Dhati ya uwazi na utashi makosa au udhaifu wa Waziri mkuu aliyejiuzulu kwa sakata la RDC!!! Sasa vijana na wantanzania wengine wakikosa kuona uimara wa Viogozi wetu wajuu kukemea ...maovu kwa namna inayostahili.. wao washike lipi? ... Wakijiunga na maovu wazazi na viongozi...,walioonyesha kigugumizi kama na richmond..watawakemea ?/? Vinginevyo ni kurithisha ufisadi ....! Jambo hili lazima lipigwe vita!!!
 
Wala tusiendelee kujidanganya kuwa JK ni mtu mzuri. Hili ni genge la mafisadi ambao ajenda yao ilikuwa ni kuitafuna nchi tartibu. nadhani wanazidiana ujanja na ndio maana baadhi wanaanza kugeukwa.
Iwapo tunataka kuondokana na mtegi huu, tunapaswa kufanya mabadiliko makubwa sana
 
Kikwete si mzuri ila mimi naona anaafdhali. Mnataka apewe nani tena? Sumaye?
 
Mbona watu mnataka sana kujipendekeza sana kwa huyu JK kumpalilia kuwa sio mchafu. JK mimi bila wasiwasi ni mchafu kweli. Kiongozi yeyote msafi anachukua hatua moja kwa moja bila kusita kama ilivyokuwa kwa Marehemu Moringe Sokoine.
 
Nyangumi,

Kama una ushahidi wa Uchafu, ulete. Sisi tunazungumzia ushahidi wa kuzembea kazi na kurudia yale yale yalioangamiza maendeleo.
 
Back
Top Bottom