Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,533
Mheshimiwa Rais Kikwete,
Waswahili wanasema kosa ni kurudia kosa. Hapo hukumu yakupasa!
Kwa uwanja wa siasa na nafasi yako ya Urais wa Jamhuri na Mwenyekiti wa CCM, Kosa ni kulinda makosa, kurudia makosa na kuendeleza makosa!
Nimekushikia bango sana, nimekukebehi, nimejaribu kukupa fununu ya njia bora ya kujiondoa katika matatizo, lakini natambua kuna moja ambalo sikulifanya nalo ni kukupa tahadhari kuwa "kulinda, kurudia na kuendeleza makosa" ni kosa kubwa sana na ndio msingi wa Taifa letu kushindwa kuendelea na kupaa kiuchumi kwa kutumia rasilimali zake.
Ulipokutana na Wazee wa Dar, ulimtetea aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa eti alikuwa ni mchapa kazi na unasikitika kuanguka kwake. Naomba ujiulize, ulitoa kauli hiyo ukiwa mzima kabisa bila kiluweluwe cha kizunguzungu?
Maana ulichofanya ni kuutangazia umma kuwa ulikuwa umeridhika kabisa na utendaji kazi wa Bwana Lowassa na hata kujiuzulu kwake haukufurahia!
Ikiwa Lowassa kama Waziri Mkuu alidiriki kufanya uzembe wa hali ya juu na kuliingiza Taifa katika mkataba hewa, je inkunkuwaje umtete?
Tayari tunajua hiyo kampuni ilikuwa imetiliwa mashaka katika utawala wa Mzee Mkapa, sasa zile ishara za ubomu wa Kampuni hii Richmond hazikuwashitua wasaidizi wako wote?
Njoo mradi wa kuchota pesa Benki Kuu, pesa zimetafunwa, lakini yaelekea walioharibu wanaendelea kupeta. Sasa hivi kuna ATC, Muhimbili na bado Kiwira zinatusumbua. Je bado unaridhika na yanayotokea?
Ikiwa utasema na kwa vitendo una ungana na wapambe wako wanao dai eti "mbona Nyerere, Mwinyi na Mkapa" walikuwa na makosa na udhaifu, basi tujiulize kama Taifa ni kwa nini tukupe tena kura zetu 2010 ili uendeleze makosa?
Tafadhali sana mnapokaa Butiama, mjisafishe roho. Ikiwa maswahiba zako wa karibu Lowassa na Rostam wamepakwa matope mazito ya mfinyanzi, tukueleweje sisi wananchi?
Tunakupa fursa na nafasi mpya ya kuja na kutuambia ukweli. Njoo tuambie ukweli, ungama tukusamehe na uongoze nchi kwa mujibu wa Sheria na Katiba.
Kinyume cha hili ni kurudia makosa, kulinda makosa na kuendeleza makosa hivyo wewe utakuwa mkosefu!