Mh. Kikwete achana na utumwa wa fikra | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Kikwete achana na utumwa wa fikra

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Noboka, Sep 14, 2012.

 1. N

  Noboka JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 1,144
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Dr. Kikwete wakati anahutubia mkutano wa wawekezaji huko Kenya nilimsikia anazungumza Kiingereza chetu kile cha kuunga unga, alipopewa nafasi balozi wa Kenya nchini Tanzania yeye akaongea Kiswahili. Binafsi nimekuwa nashangaa inakuwaje viongozi wetu hawataki kukitukuza kiswahili? Nakumbuka wakati mmoja Mkapa kwenye mkutano wa AU alitoa hotuba kwa kiingereza (ingawa Mkapa kiingereza chake ni kile cha kwa Malkia hasa), lakini alipohutubia Joakimu Chisano akaongea kiswahili fasaha mkutano huohuo.

  Wazo langu:

  Kiingereza ni muhimu lakini Kiswahili nacho kina nafasi yake, hata kama tumeshindwa kuuza vizuri rasilimali kama madini na mbuga za wanyama, bado viongozi wetu wangelitilia umuhimu suala la lugha ya kiswahili bado tungeweza kuuza hiyo huduma kwa wale wanaoihitaji. Siwezi kushangaa kwa wale mlioko huko majuu kuwa walimu wa kiswahili huko ni kutoka Kenya au Ghana. Kama mkuu wa nchi bado fikra zimefungwa na ukoloni je anatuongoza anatupeleka wapi?
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Sep 14, 2012
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hakika ! Hakika !

  Kuna ushamba wa matumizi ya Kingereza , mara nyingi tunaaminishwa kuwa ni Lugha ya Kisomi ! Ujinga kabisa
   
 3. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Alafu wapambe wake wanamsifu kwamba amepigania kiswahili kuwa lugha rasmi ya AU. Anashindwa kukitumia hapo Kenya tu, sijui huko Au atakitumiaje? Ushamba tu kama wa katibu wa Umofia kwenye riwaya ya No longer at ease!
   
 4. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kazi kweli kweli!! Dr Presid.....
   
 5. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Hiyo cha mtoto, kali ya mwaka ilikuwa hapa hapa Dar, nafikiri wakati wa Tsunami ya Japan, Bw. Mkapa (raisi mstaafu) alikwenda kutoa pole Ubalozini, kama kawaida yake akatoa hotuba yenye maneno magumu ya kiingereza ilipofika zamu ya Balozi wa Japani akatoa Hotuba kwa Kiswahili fasaha kabisa! Kwa kifupi kituko kama hiki huwezi kuona sehemu yoyote Dunia hii isipokuwa Kusini mwa Jangwa la Sahara tu! Halafu Dr Watson (DNA nobel laureate) akisema sisi waafrika tuna IQ ndogo Duniani tunaandama na kudai afukuzwe kazi, lakini matukio yanayoendelea Barani kwetu (kusini mwa Sahara) ni ngumu kufikiria vingine!
   
 6. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Mi-AFRIKA NDIVYO TULIVYO
   
 7. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Inashangaza tuna waalimu wa kiswahili kutoka mexico, of all the places! kwanini isiwe kutoka Tanzania?
   
 8. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kicheko! Mkuu Naifurahiaga sana hii signature!
   
 9. Alwayz on top

  Alwayz on top JF-Expert Member

  #9
  Sep 14, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 558
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  unashangaa kiingereza cha kuunga kuunga wakat yeye doctor wa kupewa? wenzake wanasoma yeye anapewa udaktar....majanga
   
 10. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,454
  Trophy Points: 280
  Huyo ****** jamani msameheni.....unajua tena pale Msoga yeye ndio king kijogoo so lazima ajitutumue wasije wakadhani ni mla mihogo mwenzao!

  JK ni DHAIFU. Kwa hisani ya JJ Mnyika.
   
 11. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Sijui kama huu ni uvumi tu lakini numesikia kwamba kanuni za utendaji katika serikali ya Bongo zinasema kwamba ukivaa ile suti ya malkia (yaani 3-piece akimbatana na kitanzi shingoni) unatakiwa upige lugha ya malkia (potlea mbali kuungaunga vipande). Ukivaa suti ya kaunda basi ni ruksa kuchapa kile kipwani. Sasa mlitaka mzee na pamba zake kali avunje kanuni??!!
  BTW, kuhusu Kiswahili kama taaluma na kama raslimali ya kuuza na kupata faida, Wakenya wametuzidi hatua kumi. Kwa mfano asilimia kubwa ya waalimu wa Kiswahili ughaibuni ni Wakenya. Sisi Wabongo iko maneno mingi tu, vitendo ni zero. Hatuna ujasiri na elimu yetu (iwe ni katika Kiingereza au Kiswahili) haijengi moyo wa kujiamini. Badala yake ni elimu ya ukariri na matokeo ya ukariri ni kama hayo mnayoyashuhudia kwa mkuu wa kaya na washauri wake!:eek2:
   
Loading...