Mh, Kangi Lugora shughulikia kero hii MWIBARA na wanamwibara toa maoni hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh, Kangi Lugora shughulikia kero hii MWIBARA na wanamwibara toa maoni hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mbutalikasu, Jun 11, 2012.

 1. m

  mbutalikasu Member

  #1
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh, KANGI NATI YA KIRUMI kwanza nikupongeze kwa uamuzi wako mugumu ulioufanya na ni wa kijasiri na kizalendo zaidi kwa wana Mwibara wa kupiga kura ya kotokuwa na imani na Waziri Mkuu kwakweli hilo ulitukuna sana wana mwibara.
  Sasa kero yangu na wana mwibara pia ni kuhusu tatizo la umeme ktk vijiji vilivyopitiwa na nguzo za umeme kwenda Ukerewe huku baadhi ya vijiji vikipata na vingine kukosa, vijiji hivyo ni Bunere, Nansimo, Genge, Mwitende, Makwa, Kabilizi, Masahunga na muda huohuo vijiji kama nansimo na busambara vina shule za sekondari zinazotegemewa kupandishwa hadhi ya kuwa high school. Kuna kijiji cha Nansimo jirani na sekondari kuna minara ya mitandao ya simu yenyewe imepata umeme lakini taasisi ya serikali imepitwa bila hiyo huduma sasa sijui wewe unalichukuliaje hilo. Pale kisorya umeme umesambazwa lakini pia kuna sekondari lakini hadi leo hakuna umeme.Halafu kuna wenzetu wa kisiwa cha nafuba wao tatizo lao kubwa ni usafiri wa uhakika sijui kama umewahi kufika pale na ukakumbana na adha ya usafiri wanaotumia nafikiri utalia, hivyo wao ukiwapatia ufumbuzi wa tatizo kama hilo basi utakuwa umewakomboa na uombe pia fungu wakatengenezewe barabara maana nacho ni kikwazo kikubwa kwa wakazi wa kisiwa hicho. Na lingine kwa wakazi wa nafuba linalowsumbua ni afisa uvuvi wa kata ya Nansimo kwenda kunyanyasa wavuvi pale kisiwani kwa kuwaomba RUSHWA na kuwachukulia mali zao bila utaratibu na mwisho ni kuwaboreshea kituo chao cha afya kilichojengwa kwa pesa nyingi lakini kikabaki bila kutoa huduma isiyokidhi haja.Kumbuka Nafuba ndo huwa inawapa ushindi wabunge wa jimbo la mwibara kila uchaguzi hivyo usile ukashiba ukasahau Nafuba
  Nafikiri kuwa unatambua uwepo wa haya yote na nichangamoto kwako ktk uchaguzi ujao
   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  who ia s/he?
   
 3. B

  BMT JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  elli we ni great thinker kweli katka jukwaa la siasa kama humjui kangi lugola mbunge wa mwibara?
   
Loading...