Mh. Kabwe Zitto na Wabunge Wenzako, Hivi ni Kwanini Bajeti ya Bunge....(Mfuko wa Bunge)..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Kabwe Zitto na Wabunge Wenzako, Hivi ni Kwanini Bajeti ya Bunge....(Mfuko wa Bunge).....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SolarPower, Jul 11, 2011.

 1. S

  SolarPower JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 226
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa Mwaka wa Fedha wa 2011/2012 ni zaidi ya shilingi bilioni 80 wakati ambapo Serikali "haipeleki" fedha yoyote kwenye shule zetu za Sekondari kama CAPITATION GRANTS kwa ajili ya kuendesha shule hizo? Mnaonaje Capitation Grant kwa Shule za Sekondari kwa Mwaka wa fedha wa 2011/2012 ikawa sawasawa na bajeti ya Bunge Lenu na hiki ndiyo kiwe kigezo cha kutumika kila mwaka kwa ajili ya kupata kiwango cha CAPITATION GRANT kwa shule zetu za Sekondari na kisha kuzigawa fedha hizo kwa kila shule kwa kufuata idadi ya wanafunzi katika kila shule ya Sekondari????.

  Pia tunaomba muongeze Capitation kwa kila Mwanafunzi wa Shule ya Msingi kutoka shilingi 10,000 kwa mwaka mpaka Shilingi 50,000 kwa mwaka kwa Mwanafunzi. Pia hakikisheni fedha za Capitation Grant zinatumwa moja kwa moja Mashuleni kwenye akaunti za shule tokea HAZINA badala ya kupitia TAMISEMI NA KWENYE HALMASHAURI. TAMISEMI NA HALMASHAURI ziwe zinapewa taarifa tu kwa ajili ya kufuatilia matumizi yake.
   
 2. S

  SolarPower JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 226
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Leo nimepata bahati ya kuzungumza na Mwallimu Mkuu wa shule moja, taarifa za fedha alizonionyesha kuhusu fedha walizotumiwa toka Serikalini zinakatisha tamaa. Wabunge wetu kama hamtafanya juhudi zozote za maana katika elimu hakika vizazi vijavyo vitawahukumu.
   
Loading...