Mh. Joseph Mbilinyi hadi sasa umetufanyia nini Mbeya mjini?

KIBE

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
943
184
Toka kuingia madarakani kwa huyu mbunge kwa tiketi ya CHADEMA, naomba kujua mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbiilinyi...nini umefanya ambacho sisi vijana wa Mbeya tunaweza kujivunia ama hata yeye kujivunia kuwa ametuwakilisha ipasavyo??
 
Usifanye kazi, kaa subiri "sugu" aje akufanyie, na atakufanyia kweli. Au labda ulitaka akufanyie nini? Vijana wa siku hizi bwana, mnapenda kufanyiwa sana.
 
Wewe kama kijana umelifanyia nini jimbo lako?...au huna viungo vya mwili?...au unangoja akili za MKOPO toka kwa Mbunge?
Rais wako kipenzi ameifanyia nini TZ?
 
We sidhani kama ni kijana kweli,we utakuwa ni mzee tu ndio maana hata ulicho kiandika hukijui.
Sasa haya maswali una muuliza nani?
Kama unaona ujafanyiwa kitu si useme ili tujadili, yani una tuuliza sisi wote ni vijana wa mbeya?
Lini umewai kuwa na imani na cdm kama si unafiki?
 
Don't ask what your country can do for you ask what you can do for your country JFK.
 
hana hoja chama chake kinachokusanya kodi tu kimeshindwa kutupunguzia shida zetu,huko mbeya mjini mna mkuu wa mkoa wa ccm,mkurugenzi wa ccm,mkuu wa wilaya wa ccm,rais anatoka ccm kwann huwaulizi wamewafnyia nn vijana wa mbeya?huna hoja
 
Mi nafikiri hii thread ina mhusu mbunge SUGU sasa kama tungetaka kujadili mkuu wa mkoa,wilay,nchi au mkurugenzi tungefanya hivyo ktka thread nyingine...tuna haki wana mbeya kuuliza tulichofanyiwa kwani ktk kampeni zake kuna vitu aliahidi kama alijua hawezi asingeahidi kuna usemi unasema AHADI NI DENI yeye alijua kuwa hana kodi alijua hawezi kushawishi serikali kuweka rami barabara na kufanya mambo yoote aloyaahid je kwa nn aliahidi?!!?? mbona vijana wengine wabunge kama Zitto wanajitokeza mbele za watu kusema walichofanya je wanakusanya kodi wale acheni ushabiki woote twajua Mbunge hana hela ya kufanya maendeleo ila ni uwezo wake wa kusimamia na kushawishi serikali na mamlaka kuelekeza bajeti kwenye real need ya wananchi NDO MWAKILISHI WETU ETI!!!! Angalizo sio.kila anayehoji ni CCM wengine hatuna vyama tunaangalia mtu anafanya nini IS HE WALKING THE TALK au.anatuzuga tu.
 
hana hoja chama chake kinachokusanya kodi tu kimeshindwa kutupunguzia shida zetu,huko mbeya mjini mna mkuu wa mkoa wa ccm,mkurugenzi wa ccm,mkuu wa wilaya wa ccm,rais anatoka ccm kwann huwaulizi wamewafnyia nn vijana wa mbeya?huna hoja
Usifikiri umbali wa pua yako! SUGU alikuwa na manifesto yake wakati wa uchaguzi ikiainisha ni kwanini wamchague kuwa Mwakilishi wao. Ajitokeze ajibu. Kama alijua hakusanyi kodi alikuwa na mbinu mbadala, na kama angetaka kusema kuhusu hao wakurugenzi, rais, wakuu wa wilaya na mkoa angewauliza! Huyu ni mwakilishi wa wananchi, sio mwajiriwa wa serikali.
 
Usiulize sugu kaifanyia nini mbeya,jiulize wewe umeifanyia nini kitongoki,tarafa,kijiji,jimbo,wilaya,mkoa na nchi yako? Anza Hapo ndio tutakujibu.
 
We sidhani kama ni kijana kweli,we utakuwa ni mzee tu ndio maana hata ulicho kiandika hukijui.
Sasa haya maswali una muuliza nani?
Kama unaona ujafanyiwa kitu si useme ili tujadili, yani una tuuliza sisi wote ni vijana wa mbeya?
Lini umewai kuwa na imani na cdm kama si unafiki?

Wewe ndo mzee na hujui nini unasema, soma kichwa cha habari kama kauliza vijana wote... Swali limeelekezwa kwa Sugu. Tumia akili yako vizuri ndugu, usikurupuke kama nguruwe pori.
 
Usiulize sugu kaifanyia nini mbeya,jiulize wewe umeifanyia nini kitongoki,tarafa,kijiji,jimbo,wilaya,mkoa na nchi yako? Anza Hapo ndio tutakujibu.

Wabunge hawa ni majanga ya taifa:
1. Mdee
2. Mnyika
3. Wenje
4. Msigwa
5. SUGU
6. Nyerere
7. Mbowe
8. Silinde
9. Shibuda
10. Selasini
11. Ndesamburo

Wapiga kura wao wanaisubiri 2015 wapigwe chini
 
Wabunge hawa ni majanga ya taifa:
1. Mdee
2. Mnyika
3. Wenje
4. Msigwa
5. SUGU
6. Nyerere
7. Mbowe
8. Silinde
9. Shibuda
10. Selasini
11. Ndesamburo

Wapiga kura wao wanaisubiri 2015 wapigwe chini
duuuuh we jamaa unatisha huo utafiti wako umeegemea katika nini maana kattika hiyo list ambaye hatarudi ni shibuda pekee. tembelea majimbo yao kwanza ndo uje useme ulichokisema hapo juu
 
Wabunge hawa ni majanga ya taifa:
1. Mdee
2. Mnyika
3. Wenje
4. Msigwa
5. SUGU
6. Nyerere
7. Mbowe
8. Silinde
9. Shibuda
10. Selasini
11. Ndesamburo

Wapiga kura wao wanaisubiri 2015 wapigwe chini

Kweli aisee walitakiwa wawe kama akina Lusinde wanapiga kazi wale wewe acha tu,au wawe kama Lowassa wazalendo kweli aisee!
 
Wabunge hawa ni majanga ya taifa:
1. Mdee
2. Mnyika
3. Wenje
4. Msigwa
5. SUGU
6. Nyerere
7. Mbowe
8. Silinde
9. Shibuda
10. Selasini
11. Ndesamburo

Wapiga kura wao wanaisubiri 2015 wapigwe chini

Labda kama hapo kwenye taifa unamaanisha ccm
 
Toka kuingia madarakani kwa huyu mbunge kwa tiketi ya Chadema, naomba kujua mbunge wa mbeya mjini Joseph Mbiilinyi...nini umefanya ambacho sisi vijana wa mbeya tunaweza kujivunia ama hata yeye kujivunia kuwa ametuwakilisha ipasavyo??

Waliopiga kura wameridhika na utekelezaji wa ahadi za mbunge wao kazi kwako wewe mchimbi
 
Mkuu kwenye hiyo list no 2,3, 4 na hakika hawarudi.Mdee bado anayonafasi kurudisha imani kwa wananchi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom