Mh JK Usiingie kwenye mtego wa Ubabe, wote hawa ni watoto wako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh JK Usiingie kwenye mtego wa Ubabe, wote hawa ni watoto wako

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Profesa, Jul 3, 2012.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  nakumbuka nilipokuwa teeneger kama 15-16 hivi, niliwahi kupambana na Mzee wangu, bila kujitambua, siwezi kuelewa kwanini niliamua tu kuanza vurugu. na nilikuwa na kampeni kabambe nikipinga nguvu aliyokuwa anatumia Baba ambayo ilikuwa inapita kiasi. Mfano, alikuwa akitumia ubao kuniadhibu na si fimbo peke yake, na wakati mwngine alikuwa akisema maneno ambayo ni ya kunikatisha tamaa, kinyume kabisa na matarajio yangu kwake. Nilikuwa nampenda, na nilitaka nimuangalie yeye kama baba na awe mfano na kioo kwa maisha yangu. So matarajio yangu yalikuwa juu sana lakini hayakuwa yanatimia na wakati wote hakuwa tayari kuwasiliana na mimi.

  Nilipoanza vurugu nyumbani, ambazo zilihusisha kuharibu mali, kuahca ujumbe mbali mbali zenye maneno makali ya kupinga matendo yake na kutaka haki, na nilikuwa sionekani, akija anakuta message au uharibifu.

  Mwisho wa siku alimtumia rafiki yake kuja kuongea na mimi, haikuzaa matunda, kwani nilimwambia nataka kuongea nae binafsi anieleze kwanini ananichukia.

  Huwezi amini, siku baba alipoamua kuniita kupitia rafiki yake tukakutana mbali kabisa na nyumbani, na aliongea na mimi very positively akinipa mifano yake binafsi, matarajio yake, changamoto anazozipata kunilea na katika maisha, na frustrations alizonazo, mambo yalibadilika. Aliongea kirafiki sana na in details kiasi kwamba nilipata uchungu mno na kujilaani kwanini nilikuwa namfanyia vile. Ila nisingejua kama asingeitafuta na kuitumia nafasi ile kuzungumza na mimi kwanjia muafaka. TANGU SIKU HIYO, TULIKUWA MARAFIKI WA KARIBU SANA, na tulianza kujadiliana mara kwa amara changamoto za nyumbani na jinsi ya kuzisshughulikia. Hali duni ya nyumbani haikuwa kero kwani niliona nina wajibu pia wa kusaidia kuboresha hali pale nyumbani.

  Fimbo ziliisha kabisa na hata kukaripiwa hakukuwepo. Nilanza kufanya kazi kwa bidiii pale nyumbani, nilianzisha mifugo, maua, bustani za mboga, na hata shuleni nilikokaribia kuacha niliendelea na kufaulu vema nikachaguliwa kwenda "A" level kati ya wanafunzi 5 tu out of zaidfi ya 150 waliokuwepo darasani.

  Mh Raisi una nafasi ya kuzungumza na hawa wanaohamasika kugoma, na kwa kutumia ushawishi, na kuonyesha upendo kama baba wa wote, wataelewa tu. Usiwe na hasira, najua inaudhi, unaweza kutumiwa vibaya na kundi la wale wanaokusudia mabaya kwako binafsi. Binafsi watu wanakujua huna hulka ya ubabe, so ukikubali kuingia kwenye mtego wa kutumia nguvu, ni shida kidogo utawaingiza wengi kwenye mgogoro.
   
 2. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Watu mna roho ngumu kweli kweli
   
 3. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ili kujenga mahusiano mazuri majadiliano inabidi yapewe nafasi ''well said Profesa'' ila kujua jinsi ya kujadiliana na mbinu gani zitumike hilo ndo linabaki kuwa tatizo.
   
 4. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,171
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  Kumbuka baba hapigiwi kura! Na baba anayetapanya mali za familia kwa zigawia nyumba ndogo hafai kabisa
   
 5. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Hivi mwisho wa siku, madaktari bado wamesimamia hoja yao, na walimu wakajiunga, na manessi, then what next? kama Mh JK hukuwa na desturi ya Ubabe usiianzishe sasa, itakugharimu, punguza hasira baba.
   
 6. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Ujumbe wako mzuri sana lakini anaeambiwa anaona suluhisho ni ubabe.
   
 7. Mpangamji

  Mpangamji JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 536
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Well said, but to the wrong person
   
 8. d

  dada jane JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi kwanini Rais asiwe na washauri kama hawa akina Professor?
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Raisi yupo kwenye mstari ,jamani amesema wazi tena kwa sauti kuu ,serikali yake haina hela ,sasa kuna kauli zaidi ya hiyo ? Hata ukienda dukani kama huna hela au hela yako haitoshi sidhani kama utapewa bidhaa.Madaktari na wengine wasubiri uchaguzi wachague chama ambacho kitaweka serikali itakayowalipa mishahara minono.
   
 10. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Sijasahau mwalimu wangu mmoja ambaye yeye alikuwa mfanyakazi wa kawaida tu chuoni, lakini alipopata nafasi ya wafadhili kusoma PhD na kuipata akabadilika ghafla. Bora badiliko lingekuwa chanya, lahasha. Alianza kubagua kikabila akipenda sana wa kwao, akisikiliza sana wanawake (yeye mwanaume), akiwa mbabe kwa kila anayeitwa mwanafunzi asitake kumsikilisa isipokuwa kwa ubaguzi. Siku moja nilimpigia simu kumweleza matatizo yangu kwa sababu alitoa mwenyewe simu, tena tatizo lenyewe lilikuwa limefanywa na ofisi, mimi nilikuwa najibidisha kulisahihisha kupitia kila mwalimu kwa somo lake. Niliwaona wengine wote na walishirikiana vizuri. yeye alikuwa hapatikani kirahisi. Nilimpigia simu naye akapokea. Nilipoanza kujieleza kwamba mmimi ni mwanafunzi wa...Akanikatisha kwa kusema "Mimi siongei na wanafunzi kwenye simu, sorry" akakata simu. Nikachukia kwelikweli kwa sababu kwanza hata kiumri alikuwa mdogo tu, tatizo ni kule kusoma uzeeni, pili kosa halikuwa la kwangu lakini kuliacha kosa vile lingenigharimu sana. Tatu sikuwa na hofu sana na somo lake kwa vile nililiona kama somo la kawaida tu isipokuwa yeye akiangalia kazi alikuwa anakuangalia wewe na sio kazi uliyoifanya, kisha anakupa alama wewe na sio kazi yako na ubora wake. Aliamini kwamba asemacho mwanafunzi kila kitu ni ***** tu. Alitaka akuone uko chini sana na yeye yuko juu sana kiasi haiwezekani mkajadiliana kitu, mkali wakati wote. Kama amesikia simu ya mwanafunzi imeita kwa bahati mbaya alisahau kuizima, usipime! Alikuwa anasema yuko tayari kuondoka darasani. mwanafunzi akinywa maji darasani utamsikia anasema "Just like americans, everytime chewing like a cow....."

  My take: Rais au serikali yake kujiamulia wao watakavyo kwa kudhani wenyewe ni bora zaidi kuliko watu wengine nchini na hata kwamba wao wanajua kufikiri kwa usahihi zaidi kuliko wengine haiwezi kuleta muafaka katika jamii. Madaktari wamepakwa rangi isiyo ya kwao. KIla serikali inaposema kuhusu madaktari ni kinyumenyume na ni ubayaubaya tu. lengo la serikali bila shaka ni sehemu ya kutaka kuwaambia wananchi hivyo wanavyoaambia ili waonewe huruma na kuungwa mkono hata kama kwa kuuficha ukweli. Hilo lawezekana kwa sababu hata bungeni sasa hivi hoja ya madaktari imepigwa marufuku kuzungumzwa, lakini serikali inaendelea kutoa maamuzi kivyao pasipo kuruhusu mijadala ingawa ati suala liko mahakamani. Sasa maintern wanafukuzwa na registrars wakiwa wamezibwa midomo.
   
Loading...