Mh JK ukimaliza ziara zako,naomba uanze ziara za kukagua miradi isiyo ya maendeleo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh JK ukimaliza ziara zako,naomba uanze ziara za kukagua miradi isiyo ya maendeleo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Calnde, Dec 8, 2008.

 1. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Naamini muda si mrefu utakuwa umemaliza mikoa yote na hivyo utakuwa umebakisha nchi za nje tuu unless uanze za kila wilaya! Sasa nakuomba yafuatayo! Uanze kukagua miradi isiyo ya maendeleo.
  1.Uanze kukagua ujenzi wa BOT kisha ukague akaunti hadi akaunti kwa mwaka hadi mwaka!
  2.Upite kila wizara kuona mapato na matumizi yao.Usisahau kukagua zile wizara ambazo zimepangisha kwa gharama kubwa ambayo ndani ya mwaka mmojawanaweza wakajenga majengo yao binafsi.
  3.Usiache kupita vituo vya polisi ambavyo kila siku hawana karatasi lakini pembeni kidpgo kuna stationery ambapo wanaohitaji huduma huagizwa kununua karatasi hapo.
  4.Usiache kukagua wizara ya elimu ambapo mradi wa kuvujisha mitihani na kutoa vyeti feki bila wahusika kuwajibishwa unaendelea.Pita mpaka vyuoni uone digrii feki zinzvyouzwa.
  5.Ukiwa Dar usiache kupiga jicho nje ya gari lako uone mighorofa inavyoporomoshwa mita mbili toka barabani kama vile hatuna mawazo ya upanuzi wa barabara.
  6.usiache kukagaua magari ya serikali yanavyobeba majani toka pugu na chanika as if kuna maradi wakufuga ng'ombe wa maziwa.Magari hayo hayo ndio yanabeba viti na maua yakupambia harusi.
  7.Morogoro umejionea mwenyewe jengo la mkuu wa wilaya limegharimu over bilion Tsh,pita kila wilaya uone miradi ya namna hii ilivyo mingi.Nakuomba usiache kupita ziko sehemu nyingi natamani uzitembelee.....

  Ukimaliza kukagua utakuwa na mambo mawili yakufanya 1.Uwakusanye wasaidizi wako pale ngurdoto kuwapa semina mpya elekezi au 2.Umrudishe Lowassa Madarakani mfanye fataki ya kujenga mahabusu na jela kila kata kwa msaada wa nguvu za wananchi. Usipofanya hivi 2010 itakukuta umetumia muda mwingi ukikusanya mawe na kumbe umepoteza dhahabu nyingi!
   
 2. z

  zetiti2008 New Member

  #2
  Dec 8, 2008
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sawa ila asitoe taarifa akienda. akifika mfano kituo cha polisi (hasa matrafiki) wakaguliwe na wakuu wao-wataona mabulungutu ya hongo yanavyofichwa kwenye soksi.
   
 3. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Bado nasisitiza afanye ziara akague miradi mingi isiyo na maendeleo? Hapo ataona umuhimu wa kuwa na mahabusu kila kata
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2008
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hautahitaji feedback akimaliza hiyo kazi uliyompa?
   
 5. share

  share JF-Expert Member

  #5
  Dec 8, 2008
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,293
  Likes Received: 2,277
  Trophy Points: 280
  Akishamaliza ziara zote hizo, mshauri pia aende karibu na Lugoba mbele kidogo tu ya Chalinze-mzee njia kuu ya lami ielekeayo Segera kijiji cha Mboga (kama sikosei, nikikosea mnisahihishe wakuu) atupe jicho upande wa kushoto aone jumba kubwa la kifahari linalojengwa bila kubandikwa kibao cha contract ya ujenzi kama sheria inavyotaka. Akishaona atuambie pia jumba hilo ni la nani.
   
 6. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #6
  Dec 8, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Nitaona mwenyewe mkuu.Cha msingi aende kwanza!
   
 7. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #7
  Dec 9, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180

  Hao ambao wanashikilia nafasi za sehemu hizo wafanye nini ? yaani kuwa rais wa Tanzania ni utumwa.
   
Loading...