Mh.JK kupandisha ushuru wa Magari ya Mitumba Tanzania 2005 nini faida?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh.JK kupandisha ushuru wa Magari ya Mitumba Tanzania 2005 nini faida??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halfcaste, Feb 7, 2011.

 1. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Mh.Rais J.Kikwete baada ya kuapishwa 2005,alihutubia Bunge na kutangaza kuongeza ushuru wa magari ya Mitumba(recondition cars) yaingizwayo tz kwa kisingizio kwamba 'yanachafua mazingira,na vilevile kuwa repair yake inagharimu uchumi'. Ushuru ulipandishwa na uko juu.Leo hii tunaona watanzania wanahangaika kununua magari yale yale Rwanda,Burundi,Uganda,Zambia,Kenya etc,kwamba eti ushuru wa hizi nchi ni mdogo.

  1.Vijijini wagonjwa vijijini bado wanapakiwa kwenye Machela, baiskeli na malori ya mchanga...
  2.Ugonjwa Fistula kwa akina mama,ndo unazidi kukua kutokana na akina mama hawa kukaa na uchungu mda mrefu kwa kukosa usafiri kufuata vituo vya afya.

  3.Je Wabunge wa CCM na Upinzani mliompigia makofi rais siku hiyo mlikuwa na maana gani? Je, uchumi wa Mlala wima(hoi) wa Tanzania unaweza kununua Gari brand?
  4.Je, Wabunge,viongozi wa serikali mnaotegemea magari mapya yalionunuliwa na kodi za mlala wima mnafurahishwa na hali hii si ndio ?

  CHADEMA kwa hili nawapa sufuri(0%
  )
   
 2. makandokando

  makandokando JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mh rais point sio kuongeza ushuru, point ni kuhakikisha ushuru uliopo hautumiki vibaya na mafisadi hawagawani......kama system ni mbovu, ukiongeza ushuru huku mafisadi wanaongezeka upande wa mbili....wala hubadilishi kitu.....unachofanya ni kuwaongeza hasira wananchi, halafu matokeo yake utayaona muda si mrefu....we endelea tu.
   
 3. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  Kama vile tukikuwa pamoja kwenye mada yako. Watanzania wengi tunaishi kwa kuangalizia, hata serikali yetu ina mtindo wa kuangalizia, hili la magari ilicopi kutoka kenya, wenzetu kiuchumi wametuzidi 80% hivyo wanauwezo, sisi hatujafika huko, hapa ndipo tunapomkumbuka Mzee wetu Mwinyi, alikuwa na huruma, alikuwa naupeo wa kupima hali halisi ya watanzania, tangia JK achukue nchi tunajuta kwa haya yafuatayo.
  Akiwa na waziri wake Meghj alipandisha ushuru wa ndani wa kulipia gari kutoka elfu ishirini kwa mwaka kwenda 180,000.00, sijui alitumia vigezo gani, watu wengi mitaani wanatumai Road Licence feki maana wanaona kupata mpya ni vigumu inaonekana kama kuwa na gari ni adhabu tosha kwani unaonyesha anasa. serikali inakosa mapato mengi kutoka na kukomoa wenye mali ambao ndio wanapashwa kulipa ushuru huu kama ungekuwa na haki ya kufanya hivyo, sasa ushuru wa gari upo juu kabisa, angalia mtu anashindwa kununua tairi jipwa wewe unamdai laki tatu na fine kubwa kama akichelewesha. nauliza mbona utawala wa miaka hii umekuwa adhabu kwa watanzania, kupanda kwa vitu kumetugalimu sana hakuendani na hali alisi ya mishahara yetu.
   
Loading...