Mh jk historia itakuhukumu kama si wewe vizazi vyoko tusifike huko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh jk historia itakuhukumu kama si wewe vizazi vyoko tusifike huko

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Joblube, Nov 21, 2011.

 1. J

  Joblube JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hivi Mh Rais husomi hata alama za nyakati ukajua kuwa Watanzania wameamka kwa sasa si rahisi kuwadanganya kama mnavyodhani. Nilikuwa nimemsikilza Selina Kombaini yule waziri wa sheria na katiba akisema eti CHADEMA ilisema itakuja na katiba mpya ikiingia madarakani ktk siku 100 za kwanza nikashangaa lakini mama huyu ilibidi nimsamee kwa kuwa kweli uwezo wake hata ukisikiliza wakati anazungumza bungeni utagundua kuaw ni mdogo sasa. Kilicho niacha hoi ni pale JK alipoirudia kauli ili nilichoka kabisa kwa kuwa wakati wa kampeni hasa za CHADEMA nilihudhuria na kilichozunguzwa ni kuwa CHADEMA kikiingia madarakani mchakato utaanza ndani ya siku mia baada ya kuapishwa. Hivi mtu mwenye hadhi ya JK kupotosha kwa malengo ya kupotosha hamuoni munajaharibia zaidi na watu tuzazidi kuwadharau.

  Hivi Mh Rais ukiweka mazingira mazuri ya kupatikana kwa katiba mpya kwa haki bila upendelee utapungukiwa na nini. Lazima ujue mkuwa sio lazima kuwa nyinyi mtakaa madarakani milele lazima kuna siku kuwe kuna Katiba mpya au la mtatoka tuu hilo wala msijidanganye. Hivi hamuoni badala ya kupunguza hasira za wanachi mnazidi kuzipandisha,kweli sikio la kufa halisikii dawa.

  Mheshimia Rais hivi kunaubaya gani kufanya zoezi hili likakaubalika na kila upande utapungukiwa na nini kama siokujiongezea umaarufu na kukuwezesha kustaafu kwa amani. Fikiria Watoto wako utakapoaachia nchi ikiwa vipandevipande itakusaidia nini. Kumbuka umepewa ushauri wa Bure na Mhe Salim A Salim na Kitine ujaribu kutumia busara kutuunganisha watanzania badala ya kuendelea kutugawa mara kwa mara ukidhani mtaendelea kututawala. Kumbuka huu ni ufa wa pili utatuachia nchi na watoto wako wakiwemo, ufa wa kwanza ulileta udini, sasa unaleta tena ufa huu wa katiba. Nakusihi ufikiri upya Mh Rais.
   
 2. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Bila shaka ujuimbe huu utamfikia, ni kweli viongozi wa leo wanajisahau sana.
   
 3. T

  TULIBAHA Member

  #3
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Viongozi wote wa ccm ni waongo hata huwa sidriki kuwasikiliza hawana jipya.
   
Loading...