Mh. Jakaya Kikwete: Upole, Udhaifu na Ukimya wako unatuumiza Watanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Jakaya Kikwete: Upole, Udhaifu na Ukimya wako unatuumiza Watanzania!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Feb 6, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mh. Jakaya Kikwete,

  Kwa mara nyingine hapa JF tunajitolea kusema kile tunachoamini ni ukweli.

  Ukweli unaoambiwa na WanaJF ndio hali halisi ambayo wananchi wengi wanakumbana nayo iwe kwa uzuri au ubaya. Kila anayekulaumu anawakilisha watanzania si chini ya Milioni 5 idadi sawa ya waliokupigia kura. Haraka haraka washauri wako wanaweza kukupotosha au kukudanganya kama walivyozoea 'hayo ni mawazo ya wapinzani wako! JF ni wapinzani na hawakupendi'. Tuamini sisi, wao ndio hawakupendi!

  Mh. Jakaya Kikwete, kama wangekuwa wanakupenda wasingekuwa wanatengeneza barabara wakati tu wa ziara zako. Wanamdanganya nani? Siku ambayo umepanga kutembelea eneo fulani greda la halmashauri litatengenezwa, litawekwa mafuta, dereva atalipwa posho barabara itachongwa? Unahitaji research katika hili? Najua wasaidizi wako watakwambia waambie walete ushahidi. Shahidi wa kwanza ni wewe mwenyewe!

  Mheshimiwa Jakaya Kikwete, wanaokulaumu si chini ya Milioni 5 kwa sababu zifuatazo;

  A) watanzania watu wazima (zaidi ya miaka 18) wako zaidi ya Mil 15.

  B) waliokupigia kura ni Mil 5+ na waliompigia kura Mh. Dr Slaa na Mh. Prof. Lipumba ni Mil 2+.

  C) Toka tarehe uliyochaguliwa mpaka leo hakuna badiliko lolote katika hali ya maisha ya mtanzania zaidi ya bei ya nishati kupanda, mgao wa umeme kuendelea, bei za vitu kuongezeka nk. Zaidi ya hayo matatizo kama Dowans, migomo, uonevu wa jeshi la polisi yameendelea. Hayo yote hayawezi kuwa yamekuongezea wafuasi. Hauhitaji research kujua hilo! Wasaidizi wako wanaweza wakataka a formal opinion poll! Ni wizi tu wa hela na njia ya kuandaa matokeo yake ili wakuridhishe bado unapendwa! Wanakudanganya! Angalia idadi ya kura ulizopata na hicho kiendelee kuwa kipimo cha muonekano na kukubalika kwako kwa wananchi. Kipimo hicho kinaelekea chini sio juu!

  Kwa sababu hizo mbele ya watanzania wengi wewe ni wa kulaumiwa tu! Hawakuonei hata kidogo. Haya yote unajitakia na pia ndicho wanachokutakia uliowateua kukusaidia katika uongozi wako.

  Mh. Jakaya Kikwete, umekuwa kinara wa kujaribu kuvunja makundi. Muda mwingi wa uongozi wako umeutumia kuasa wanaCCM na wananchi kwa ujumla waache makundi lakini wewe mwenyewe umeendelea kuyakuza! Kwa upole wako, udhaifu wako na ukimya wako!

  Kutokana na ukimya wako, upole wako ambavyo ni udhaifu badala ya sifa makundi yameendelea kuwepo mpaka mlangoni kwako! Ni kutokana na makundi hayo watanzania tunaumia! Tunaumia sana. Kila mtu anasema, kila mtu ni mzungumzaji!! Kuhusu dowans kuna kauli zaidi ya kumi! Tumsikilize nani? Kuhusu mauaji Arusha kulikuwa na kauli ya OCD, RPC, IGP, Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa TAMISEMI, Waziri Mkuu nk! Jana umetoa kauli yako! Zile za Makamba na Chitanda tusiziseme hapa maana zitawakera sana wengine! Watu wanakufa, amani ya nchi inakuwa mashakani kiongozi analeta kejeli na majibu ya kitoto! Hii si sahihi! Halafu wewe unakuwa kimya!

  Mh. Jakaya Kikwete, unatutenga kwa itikadi za vyama! Hilo ni kundi! Kuna CCM, CUF, CDM, NSSR nk. Ukweli ni kwamba wananchi wenye kadi za vyama vya siasa hawafiki Mil. 15! Hawafiki! Ina maana hili hulijui, haulioni au halina maana kwako?

  Hapa JF lina maana kubwa sana. Kutokana na idadi kubwa ya wananchi kutokuwa wanachama wa vyama vya siasa kitendo chako cha kuongelea masuala mazito ya nchi kwa minajili ya CCM inakuweka mbali na wananchi ambao sio wafuasi wa vyama! Ni wengi kuliko unavyodhani au unavyoambiwa!

  Mh. Jakaya Kikwete, mfano, suala la Dowans unaongelea kwenye Kamati Kuu ya CCM na kwenye Kamati ya Wabunge wa CCM!! Unategemea nini? Suala hilo haliongelewi kwenye baraza la mawaziri chombo ambacho hakitakiwi kuwa na itikadi hata kama kimetokana na CCM! Chombo hicho kinawatumikia wananchi wote! Hata hili hujaliona?

  Mh. Jakaya Kikwete, unatuambia Mh. Chiligati kalizungumzia! Jamani, kweli watanzania wote wanatakiwa kusikiliza na kufuata alichosema Chiligati! Wewe unahaki ya kuwa kimya!

  Huo ni udhaifu! Ukimya wako ndio udhaifu wako! Unaruhusu yale ya kuyasemea na kukemea yasemwe na kukemewa na wengine! Unawaamini sana? Au ni upole? Inawezekana si kwamba unawaamini au wewe ni mpole! Itakuwa ni kitu kingine zaidi, udhaifu!

  Mh. Jakaya Kikwete, nafasi yako ni ofisi sio cheo! Masuala yanayowagusa wananchi yanazungumzwa na Ofisi ya Raisi! Siyo na Ofisi ya Chama! Watendee haki wananchi walio wengi ambao si wafuasi wa CCM, CDM, CUF nk! Wao ni watanzania na wako wengi!

  Taabu za watanzania ni za jumla! Shida haichagui CCM wala CDM! Wote tunalala giza, wote tunalipa bei sawa kwa mahitaji yetu! Tujibu kwa umoja wetu na si kwa vyama vyetu! Huko ni kutengeneza makundi! Baada ya kutugawa kwa UCCM na UCDM ndani ya CCM kutakuwa na kundi la U-sitta na U-rostam! Kamati Kuu na UVCCM! Au huoni mkuu?

  Mh. Jakaya Kikwete, mazuri yako hayaonekani! Kama yapo kuanzia tarehe 31 October 2010 mpaka leo hatuyajui! Hakuna dhambi kujitokeza hadharani na kuyataja mwenyewe! Inawezekana ukimya na upole wako ambavyo kwetu ni udhaifu vinakuathiri hata wewe mwenyewe! Unashindwa kujisemea na kujikemea! What a vicious circle!!

  Naamini unaweza kuangalia haya niyoyaweka humu jamvini! Hata kama hutayasoma basi kuna atakayekufikishia! Uwezekano wa anayeleta kuyachakachua ni mkubwa lakini sisi tumesema!! Usidharau au kupuuzia unayoyasoma humu, leadership has a price and unfortunately the price for your leadership is constant criticism and blame! Your leadership deserve each and every blame!

  Stay well BUT watanzania wanaumia, wanateseka!!
   
 2. Quinty

  Quinty JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ngozi ya kundoo
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Feb 6, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,562
  Likes Received: 3,858
  Trophy Points: 280
  Msando are you begging Kikwete to speak out!!

  Kikwete aliishashindwa kabla hajawa rais, anything you are saying now it means you have hope in him!!!

  Msando najua hili ni mfupa mgumu kwa chadema, ni muda wa Kikwete kuondoka madarakani kupitia mtaani,wewe unaweza hili.....kusubiri sanduku la kura ni kupoteza muda. Ameshindwa kazi aondoke!! haya yote is a wastage of time!! nadhani unajua maana ya mapinduzi maana ulitaka kupindua serikali yangu DARUSO..... you know what I mean?? aina ya post kama hizi zimejaa kila blog, facebooks,e-mails, humu JF ziko nyingi sana. tuwaze kimapinduzi zaidi CCM must go..begging Kikwete has a different meaning

  Mtaani ni solution, believe me.
   
 4. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #4
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  kikwete si mpole ila anafuata utawala wa sheria,ametupa uhuru wa maoni na kuhoji mambo hata yale ya ndani kuliko enzi za mkapa kulikuwa hakuna mtu aanaeweza kuhoji wala kutoa maoni hata kuchokonowa mambo yaliyo ndani na ya ni siri, kama huamini hilo mwulizeni MUNISHI ALIYEKIMBILIA KENYA atawapa jibu,sasa kwa uongozi wa kikwete tupo huru kuhoji na kuuliza thats why mambo mengi yanaonekana sasa

  hivi kikwete akiwa kama Hu Jintao wa china je haya yote tungeyasikia? hata jamii forum isingekuwepo,hakuna takataka yeyote hapa bongo itakayo sema chochote juu yake,lakini kwa kuwa anafuata utawala wa sheria ndio maana hayo yote yanatokea

  msema ukweli hapendwiiii daimaaaaa:popcorn::clap2:
   
 5. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Webs, nakubaliana nawe kwamba njia mojawapo ya kubalisha uongozi mbovu ni kwa wananchi kuingia mtaani. Tatizo langu;

  Kama ilivyokuwa ngumu kupindua serikali yako ya DARUSO kuna ugumu wa kuiondoa serikali ya CCM kwa kuingia mtaani. Naamini hukumaanisha MSITUNI!

  Kundi la CCM bado ni kubwa, kuna watu wako tayari kuifia. Leo nimeongea na mzee mmoja kuhusu kikwete akakataa kunipa mkono wakati namuaga na ameapa kutotaka kuongea na mimi tena! Kisa kikwete hana tatizo hata kidogo!

  Tunahitaji kuhamasishana kwa kufikisha ujumbe kwa wananchi kupitia Jakaya mwenyewe! Nadhani utakubaliana na mimi kwamba kama tusingekuwa tunapashana habari kwa njia hizi basi tungeandika na kumpostia moja kwa moja. Kwa wengine kusoma inasaidia kufikishiana ujumbe kati yetu!

  Siamini kwamba kutakuwa na mabadiliko makubwa leo wala kesho! Angalia UVCCM! The hatching ground for future leader! Nani ulikuwa nae DARUSO? Au kwenye uongozi wa vyuo vingine?

  So, mtaani au msituni Webs?
   
 6. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Quinty, nadhani unamaanisha Kondoo! Ni nani huyo anayo au ameivaa?
   
 7. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  we kiazi, JK hapandishi bei ya nishati bali wanaopandisha ni wale wenye visima kule Uarabuni.
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Feb 6, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,467
  Likes Received: 4,126
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo kazi ya serikali yake ni nini?
   
 9. w

  warea JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Heri Hu maana anasikiliza, likitokea jambo mara moja anasikia na kulitolea uamuzi. Serikali yetu inasikia haya yanayoandikwa humu? Inayaona maoni ya wananchi? au wao wananchi ni wanaCCM? Chiligati ni nani ktk serikali ya Tanzania, makamba ni nani ktk serikali hii.

  Gharama za maisha zinavyopand kila siku serikali haijui? au mpaka bunge liunde tume ya kuchunguza? Haya labda waheshimiwa wabunge wataunda hiyo tume juma lijalo!

  Mi najua serikali ni ya watu wote na rais ni wa watu wote. Nasubiri rais aseme, sio mwenyekiti wa CCM. Hayo ya uenyekiti na ya vikao vya CCM ni yao wenyewe.
   
 10. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Nani kasema Kikwete ni mpole na mkiya? Kikwet ni Jeuri, Kiburi na fisadi papa wa nchi yetu.
   
 11. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #11
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  So what exactly are you trying to say? Nakushauri kujifunza kwanza maana ya leadership na utawala wa sheria (rule of law) then come back with some constructive ideas. Incase you are confused thread ya Msando inazunguzia leadership ya JK na si utawala wake ni wa sheria au la!
   
 12. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #12
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Kwanini unazunguka Msando? Sema neno moja, UNAFKI WAKE NDO UNAIHUJUMU NCHI.
   
 13. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #13
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  naelewa lengo lako nikufurahishe labda kwa kusema neno baya juu ya raisi hapo utafurahi,lakini nachokizungumzia namaanisha sina haja ya kwenda rudi,mala nyingi ya kaisali huwa nampa kaisali na ya mungu huwa nampa mungu,kama unafikilia zaidi ya hapa utanipata lakini kama unafikilia chini ya hapa huwezi kunipata mkuuu

  msema ukweliii hapendwiiii daimaaaaaaaaa:clap2:
   
 14. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #14
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sikupingi UKG! Unafiki! 'Mbaya sio mimi' 'sihusiki'....mbaya nani? Anayehusika nani? Hapo ndipo wananchi wanabaki njia panda! Kama wewe hujui nani anajua? Mh. Jakaya anaiweka nchi mahali pabaya! Haya mawazo ya 'tufanye nini' kuna siku yatakuwa kweli!
   
 15. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #15
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Muongo mkubwa we!!! Bei ya umeme wamepandisha wenye visima kule uarabuni???!!!
   
 16. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #16
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Sidhani kama hii forum ya Great thinkers ni kwa ajili ya kusema maneno mabaya juu ya wengine kwa hivyo sitarajii kama una nia hiyo. Ni wazi kabisa kuwa you are oblivious na mada nadhani kwa sababu ya ushabiki. Nafikiri mtu ku-question integrity ya mtu au utendaji wake kama kwako ni maneno mabaya basi nakupa pole sana. Vinginevyo lengo langu lilikuwa kukuweka sawa juu ya mada husika.
   
 17. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #17
  Feb 6, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 711
  Trophy Points: 280
  huyu jama ni jeuri na mshenzi mkubwa, mwizi, mnafiki na muongo hana lolote kikwete........

  hapo alipo hajui kama yeye ni raisi wa nchi ndio maana mambo makubwa yahusuyo nchi nzima anayatolea tamko kwenyr vikao vya chama


  mpuuzi tu hana jipya
   
 18. i

  ibange JF-Expert Member

  #18
  Feb 6, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  kuna watu hawajui ku analyse mambo. kuna tofauti kati ya udhaifu na kuwa diplomatic. jk ni dhaifu . nitajie kiongozi yeyote duniani ambaye ni most democratic tuone kama pia ameshindwa ku provide leadership kama kikwete
   
 19. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #19
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Chama cha mafisadi sasa ndio kinachoamua maisha ya watanzania wakikaa vikao vyao vya NEC, sio serikali tena fisadi Kikwete ni mpumbavu nilishasema siku nyingi kuwa nchi imemshinda Mkwere anachosubiria nguvu ya umma ingie mitaani na kumfukuza aende huku Saudia akapakatwe:twitch:
   
 20. l

  lukule2009 Senior Member

  #20
  Feb 6, 2011
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Ahahaha unaweza kupunguza bei ya mafuta bana kwa kufanya yafuatayo:

  1.Weka sera nzuri na punguza idadi ya kodi kwenye mafuta.Kwa mfano nasikia asilimia 40 ya bei ya mafuta ni kodi za serikali(this means kama bei ni shs 1700 kwa lita basi ka shh 600 hivi ni kodi , so ukiweka kodi shh 300 ina maana bei itapungua hadi 1400,nimeweka mfano rahisi uelewe)

  2. Imarisha thamani ya shilingi : kwa kuwa mafuta yanauza kwa dola ina maana kuwa kwa sasa tunalipa kama dola moja na centi 40( assumption 1usd=1500, so shsh 1700 kwa lita ni sawa na dola 1.30 roughly ) .Kwa hiyo kwa mfano shs ikiimarika (yako mambo unaweza kufanya shiling ikaimarika ...hii ni kazi ya watalaam wake ila akitaka tumsaidie aseea).So shs ikiwa say 1usd=1100, ina maana mafuta ya dola 1.30 itakuwa ni sawa na shs 1400 pungufu ya shsh mia tatu.Cha kujiuliza nini sera ya BOT kweney kuhakikisha kuwa exchange rate haisaababishi inflation?


  Yani hata cement kuuzwa elfu tano bandugu inawezekana ni sera tu na kuelewa uchumi ....aisee
   
Loading...