Mh Jakaya Kikwete tunakukumbuka sana

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945
Ni miaka miwili sasa Mh Rais mstaafu Luteni Kanali mstaafu Dr Jakaya Mrisho Kikwete tangu ustaafu rasmi Ukuu wa nchi.
Mh Rais mstaafu umepumzika katika majukumu ya kuongoza nchi, Baba yetu mpendwa Jakaya kikwete nakumbuka sana ulipokua unaongea na chama cha wafanyakazi baada ya aliekua kiongozi wao ndugu Mgaya kukuomba kuongea na chama cha wafanyakazi ama shirikisho la wafanyakazi nchini
Baba yetu hukusita wala hukuchukia ulitabasamu na kumjibu uongozi huo chini ya Mgaya.

Baba yetu tunakukumbuka ulikua unaongea na wananchi wako kupitia luninga na uliwaita na kuongea na wazee wa Daresalaam kila mwezi na kutoa muelekeo na mikakati mbalimbali ya kimaendeleo kwa tabasamu kabisa.
Mh Rais Mstaafu maarufu kama JK katika
ninakumbuka pia zaidi uliporuhusu mchakato wa kupata katiba mpya kwa kuijadili Katiba pendekezwa.

Pamoja na kupumzika bado umeona uanzishe taasisi ya Maendeleo ya Jakaya Kikwete lengo lako ni kusaidia elimu, afya, vijana na mabadiliko ya hali ya tabia nchi na mazingira na ulisema tunajenga nyumba moja yaani Tanzania haina haja ya kugombania fito
Mungu akupe maisha mema na afya njema Mheshimiwa Rais mstaafu
 
Na bado mtamkumbuka sana maana mliyemuweka badala ya huyo unaemsema anadhan urais ni kukaa ikulu na kutumbua maadui zake huko kwa Bashite akijifanya kiziwi.
 
Yeye akapumzike tu kwa raha zake alikuwa na mazuri yake na mabaya yake tena mengi tu alikaa miaka 10 kuna aliyoweza na mengine yalimshinda kaacha shule nyingi tu hazina maabara madawati kaacha sehemu kubwa wananchi hawana maji umeme ki ufupi ni kwamba tumpongeze tu kwa alipoachia mm huyu JPM nitamhukumu baada ya miaka yake kuisha
 
Back
Top Bottom