Mh. Jaji Lubuva, 'Huru' na 'Haki' ni maneno mawili tofauti

Nena

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
2,297
892
Naomba kumwambia jaji lubuva hayo maneno yana maana tofauti. Uchaguzi unaweza kuwa huru na haki au mojawapo. Bila shaka waangalizi wamempa sababu zao.

Ukweli wa uchaguzi anaujua yeye na asitegemee kila mtu akubaliane naye. Kila mtu ana mtazamo wake na mwongozo wake wa kutekeleza majukumu.We all have to live with our choices wrong or right. Including him.

Waliosifia, wamesifia. Waliokosoa wamefanya hivyo.
 
Na uchaguzi wa Oct.25 haukuwa huru wala wa haki..

Uchaguzi wa marudio ZNZ duh nashindwa mpaka kusema maana hata kwa binocular huoni kitu kinaitwa Haki wala huru
 
Nilijua kama ungemueleza huo utofauti uliopo kati ya huru na haki ila kwenye contents hakuna hiyo kitu...
 
Kwa tume hizi za uchaguzi zisizo huru inaonyesha dhahiri 2020 watanzania wengi hawatakwenda kupiga kura ikiwemo mimi mmojawapo.
Kama tukiendelea na tume hizi za chama kimoja ambao watendaji wakuu wanateuliwa na raisi aliyeko madarakani kwa minajili hii hakuna haja ya kupoteza muda kupanga Poleni wakati matokeo yanajulikana.
 
Swali langu kwa Mwenyekitu wa Tume ya Uchaguzi: Hivi uchaguzi kuwa huru na wa haki ni kitu cha kufikirika? kwa nini hata baada ya kila mtu kushuhudia "madudu" mengi katika uchaguzi uliopita, yeye bado anawalalamikia wanasema uchaguzi haukuwa huru/haki? Je ni kweli kwamba mwenyekiti yeye hakuyaona na kuyasikia malalamiko na kasoro tulizoziona sisi wengine? Mathalani, hakuona hata kwenye TV malalamiko ya watu waliokosa kupiga kura siku ya uchaguzi katika jiji la Dar? hakusikia habari ya kuwepo kwa watu hewa katika daftari la kupiga kura? hakusikia kilichotokea Sumbawanga? Hajasikia kasoro nyingi katika mfumo wa kuhesabu kura na kutoa matokeo ambao umefanya baadhi ya wagombea kwenda mahakamani wakidai kwamba kwa mujibu wa matokeo katika fomu na. 21 wameshinda, lakini kwa kura zilizoko kwenye masanduku wametangazwa washindi wengine? Mwenyekiti huyu anaishi wapi huko ambako mambo haya yote hayasikii???
Ninapofikia hapa, huwa najiunga na lile kundi linalolalamika kila siku kwamba Tume hii INATUMIKA na wanasiasa.
 
Na uchaguzi wa Oct.25 haukuwa huru wala wa haki..

Uchaguzi wa marudio ZNZ duh nashindwa mpaka kusema maana hata kwa binocular huoni kitu kinaitwa Haki wala huru

Kweli kabisa Mkuu, kwa standard zetu, hata uchaguzi wa ZNZ ulikuwa HURU na HAKI! Tatizo ni kwamba Tume zetu zinaharibu uchaguzi kwa makusudi kisha zinapokosolewa zinaanza kuwalalamikia wanaozikosoa.
 
Huyu Lubuva yupo yangu enzi ya Nyerere,
mzee anang'ang'anua tuu. Hawezi kwenda kinyume na watawala wanaompa 'ugali' wake.
 
Mzee lubuva Haki IPI unayozungumzia? Labda utuambie uchaguzi ulikuwa wa Amani kama viongozi wa dini wanavyosema.Haki katika chaguzi za Tanzania haiwezi kutokea ona wa Zanzibar ona wa Meya Tanga Na Dar.
 
Swali langu kwa Mwenyekitu wa Tume ya Uchaguzi: Hivi uchaguzi kuwa huru na wa haki ni kitu cha kufikirika? kwa nini hata baada ya kila mtu kushuhudia "madudu" mengi katika uchaguzi uliopita, yeye bado anawalalamikia wanasema uchaguzi haukuwa huru/haki? Je ni kweli kwamba mwenyekiti yeye hakuyaona na kuyasikia malalamiko na kasoro tulizoziona sisi wengine? Mathalani, hakuona hata kwenye TV malalamiko ya watu waliokosa kupiga kura siku ya uchaguzi katika jiji la Dar? hakusikia habari ya kuwepo kwa watu hewa katika daftari la kupiga kura? hakusikia kilichotokea Sumbawanga? Hajasikia kasoro nyingi katika mfumo wa kuhesabu kura na kutoa matokeo ambao umefanya baadhi ya wagombea kwenda mahakamani wakidai kwamba kwa mujibu wa matokeo katika fomu na. 21 wameshinda, lakini kwa kura zilizoko kwenye masanduku wametangazwa washindi wengine? Mwenyekiti huyu anaishi wapi huko ambako mambo haya yote hayasikii???
Ninapofikia hapa, huwa najiunga na lile kundi linalolalamika kila siku kwamba Tume hii INATUMIKA na wanasiasa.
Mkuu
Ataishije? Kumbuka Lubuva ni mstaafu hiyo privilege lazima ailinde na alinde waliomweka.
Uchaguzi wa haki na huru ni pale tu zitakapoundwa tume huru as uchaguzi.
 
Huku bara pia haukuwa wa haki.maana hadi mhe lowassa wamechuana vikali na magu ujue bila uchakachuaji lowassa alikuwa mshindi.
 
Kwa tume hizi za uchaguzi zisizo huru inaonyesha dhahiri 2020 watanzania wengi hawatakwenda kupiga kura ikiwemo mimi mmojawapo.
Kama tukiendelea na tume hizi za chama kimoja ambao watendaji wakuu wanateuliwa na raisi aliyeko madarakani kwa minajili hii hakuna haja ya kupoteza muda kupanga Poleni wakati matokeo yanajulikana.
Wacha wewe 2020 tutakwenda kwenye uchaguzi kwa tume hizi hizi za kibwege ili tu halalishe mapinduzi ya kweli wakituletea ungese tena!
 
Kwa tume hizi za uchaguzi zisizo huru inaonyesha dhahiri 2020 watanzania wengi hawatakwenda kupiga kura ikiwemo mimi mmojawapo.
Kama tukiendelea na tume hizi za chama kimoja ambao watendaji wakuu wanateuliwa na raisi aliyeko madarakani kwa minajili hii hakuna haja ya kupoteza muda kupanga Poleni wakati matokeo yanajulikana.
Kwahiyo hakuna haja ya kuwa na vyama pinzani?
 
uchaguzi umeishaaaaa.....................,
MBONA KURUDIA RUDIA......
cha msingi waliochaguliwa watende HAKI....
 
Mzee lubuva Haki IPI unayozungumzia? Labda utuambie uchaguzi ulikuwa wa Amani kama viongozi wa dini wanavyosema.Haki katika chaguzi
za Tanzania haiwezi kutokea ona wa
Zanzibar ona wa Meya Tanga Na Dar.

Alafu wamekalia hivyo viti kwa kuapa kwamba watatenda haki kwa wananchi huku nafsi zao zinaonyesha dhahiri zinawasuta.
 
Naomba kumwambia jaji lubuva hayo maneno yana maana tofauti. Uchaguzi unaweza kuwa huru na haki au mojawapo. Bila shaka waangalizi wamempa sababu zao.

Ukweli wa uchaguzi anaujua yeye na asitegemee kila mtu akubaliane naye. Kila mtu ana mtazamo wake na mwongozo wake wa kutekeleza majukumu.We all have to live with our choices wrong or right. Including him.

Waliosifia, wamesifia. Waliokosoa wamefanya hivyo.
Strange, huyu Jaji alikuwa one of the best ever Judges, lakini kanyweshwa maji ya siasa, ameshabadirika. Ukiangalia judgements zake zina very high legal reasoning
 
Back
Top Bottom