TEMILUGODA
JF-Expert Member
- Feb 11, 2012
- 1,389
- 285
Pamoja sana wanaJf! Ni hapo jana waheshimiwa H.Mdee,Sungura,J.Heche na wengine kadhaa walitembelea tawi la CHADEMA la chuo kikuu cha Mwenge kilichopo Moshi.Walizngumza mengi,kwa Mdee; aliwataka BAWACHA wasiwe minofu kwani mbwa watawalamba na hatimaye vita dhidi ya rushwa itakuwa ngumu kwani wanawake CDM WANATAKIWA'KAMATA MWIZI MEEEEEEEN',wana CDM wote ni lazima kuunganisha nguvu katika chaguzi mbalimbali,hivi sasa tuunganishe nguvu pale Ar.mashariki ili ushindi upatikane tena kwa tofauti kubwa ya kura.Aliwataka walimu kuwa na ujasiri na kuacha woga kwani kwa hilo watawafundisha wanafunzi ujasiri badala ya kuwa waoga. Mwenyekiti wa BAVICHA mh.HECHE alikemea vikali juu ya propaganda za CCM za kukumbatia udini jambo ambalo litaliingiza taifa hili katika machafuko,hivyo ccm kipuuzwe kwa nguvu zote kwani kimeshajichokea,kiwekwe pembeni.MH.Sungura aliwataka wasomi wawe chachu ya mabadiliko katika jamii wanamoishi kwa kuwaelimisha wanajamii juu ya haki na mambo mengine ya uraia.Kwa ujumla ziara ya Makamanda hao ililenga kuhamasisha wanachama wa CDM katika tawi hilo kuu la vyuo vikuu mkoani K'njaro na kuzindua tawi la BAWACHA hapa chuoni, ambapo jumla ya sh.735,200/=zilichangwa kwa ajili ya maendeleo ya tawi hili.NAWASILISHA. Source: Mimi mwemyewe nilihudhuria mkutano huo