Mh.Gaudencia Kabaka - Je Unayajua Majukumu Yako ya Kizalendo nchini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh.Gaudencia Kabaka - Je Unayajua Majukumu Yako ya Kizalendo nchini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by zubedayo_mchuzi, Aug 2, 2012.

 1. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  HISTORIA YA

  WIZARA Wizara hii ni moja ya Wizara kongwe katika muundo wa Serikali tangu Uhuru mwaka 1961. Jina na muundo wake vimekuwa vikibadilika. Baada ya Uhuru Serikali iliunda Wizara mbali mbali ambapo mojawapo ni Wizara hii ya Kazi. Kati ya mwaka 1972 na 1984 ilibadilishwa na kuitwa Wizara ya Kazi na Ustawi wa jamii. Kuanzia mwaka 1984 hadi 1987 ilibadilishwa tena na kuitwa Wizara ya Kazi na Utumishi. Mnamo mwaka 1987 muundo wa Wizara ulibadilishwa na kuitwa Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo. Mwaka 1990 hadi 2000 jina lilibadilishwa na kuitwa Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana. Hata hivyo mwaka 2000 muundo wake ulibadilishwa tena na kuitwa Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo hadi ilipofika mwaka 2005 ambapo muundo huo ulibadilishwa na kuitwa Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, mwaka 2010 jina lilibadilishwa tena na kuitwa Wizara ya Kazi na Ajira baada ya kuondolewa Idara ya Maendeleo ya Vijana.

  MUUNDO WA WIZARA

  Ili kufanya kazi kwa ufanisi na kutimiza malengo yake, Wizara ya Kazi na Ajira ina Idara nne, ambazo ni Idara ya Usimamizi Kazi na Huduma za Ukaguzi, Idara ya Huduma za Ajira, Idara ya Utawala na Utumishi na Idara ya Sera na Mipango. Aidha Wizara ina vitengo vya Fedha na Uhasibu, Ukaguzi wa Ndani, Msajili wa Vyama Huru vya Wafanyakazi na Waajiri, Habari, Elimu na Mawasiliano na Kitengo cha Ununuzi na Ugavi. Vilevile Wizara inasimamia shughuli za mashirika na taasisi zifuatazo:-

  Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA),
  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
  Shirika la Tija la Taifa (NIP),
  Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya jamii (SSRA).

  HOJA YANGU.
  Hoja yangu itagusa makundi mawili makubwa ambayo hutegemea sera za wizara ya kazi.
  Kundi la kwanza ni Vijana wasio na ajira,kundi hili lina nguvu na msukumo mkubwa wa kujikwamua kimaisha kwa kutumia Elimu zao,nguvu zao na ubunifu wao ambao mwenyezi mungu amewajalia vijana.UZembe wa viongozi wachache wenye tamaa..na wasio wazalendo hulidharau kundi hili na kulisahau kabisa katika ajenda zao na kuwadanganya kila siku.Waziri wa Kazi Sijui kama ulishawahi fanya kongamano au mkutano na kundi hili mkoa kwa mkoa wilaya kwa wilaya kuwasilikiza na kupata maoni yao wewe kama wewe? Kundi hili huwa ni hatari kwa maslah ya Taifa ,kadri linavyokuwa hushawishika kufanya maamuzi ya kupambana na kundi la wale wachache wanaotumia rasmali za nchi yao kwa kujinufaisha wao.kundi hili likivumilia vya kutosha hushawishka kuliingiza taifa katika machafuko.

  Kundi la pili,ni lile la wafanyakazi wenye kipato kidogo,ambao hunyonywa na kuönewa na kundi la wanaojilipa mishahara posho kubwa na kulikandamiza kundi la hao wadogo ambao ndo watendaji.Kundi ndo watendaj kundi hili hufanya kazi kwa uzalendo kuficia madudu mengi ya serikali kwa uvumilivu mkubwa sana.
  Kundi hili nalo linapodharauliwa matokeo yake ni kuwa na serikali itayofanya kazi si kwa kiwango bora kinachostahili.Kuvuja kwa siri za serikali ni matokeo ya dhara kwa kundi hilo dogo.
  Makundi haya mawili ustawi wao hutegemea Sera,mipango na vipaumbele vya wizara katika kuwapa nyenzo katika ustawi wa taifa. wizara hii imekosa weledi na kutojari kbs makundi haya mawili.
  waziri wa kazi kaa na haya makundi yako mawili wasikilize,Kazi yako kubwa ya msingi kila uamkapo na ulalapo ikumize ubongo wako ni ustawi wa haya makundi 2.
  Mytake.Taesa ivunjwe.
   
Loading...