Mh Freeman Mbowe, jiuzulu uwenyekiti wa chama

Hivi inawezekanaje mtu unakuwa senior member kwenye Forum ya wasomi halafu unaandika pumba. Tunakubali mawazo ya kujenga na siyo ya kuboboa. Ungetakiwa uwe Dodoma kumpigia Chenge Kampeni hili mkimalize CCM kama mlivyofanya hawamu ya kwanza kwenye uteuzi wa mawaziri.

Hii ni Forum ya Wasomi?
Forum hii imejaa wanung'unikaji wa chama fulani wanaopendelea kutumia zaidi kauli za matusi.
 
Mtakuwa na tofauti gani na chama tawala kama hamtaki hata kusikia mawazo tofauti? Sisi mawazo haya haya ya chama kuwa sacrosant na chenye wenyewe ndiyo yaliyotufikisha hapa? Kama badala ya kumtukana Amanikwenu, mngemjibu kwa hoja wote tungeona na kufurahia maturity ya chama chenu. Kwa kufanya mlivyofanya mnakitia dosari chama chenu. Au hilo ndilo lengo lenu? Nina wasiwasi na uanachama wenu maana kuna tofauti kati ya mwanachama na shabiki. Nadhani wengi wenu ni mashabiki na wanachama wa kwenye keyboard msio na uchungu na hicho chama.

Amandla.......
 
Hivi inawezekanaje mtu unakuwa senior member kwenye Forum ya wasomi halafu unaandika pumba. Tunakubali mawazo ya kujenga na siyo ya kuboboa. Ungetakiwa uwe Dodoma kumpigia Chenge Kampeni hili mkimalize CCM kama mlivyofanya hawamu ya kwanza kwenye uteuzi wa mawaziri.
Sasa hapo kubomoa ni kupi na kujenga ni kupi??? sijakuelewa mkuu:A S confused:
 
Nawashukuru wote walionipinga kuhusu wazo nililolitoa. Napenda kuwaambia kuwa ushauri wangu uko palepale na mtakuja kuniambia mbele ya safari.
 
Napendekeza Mwenyekiti Mbowe ajiuzulu uwenyekiti wa chama ili kutoa nafasi kwa Dr. W Slaa kuwa Mwenyekiti mpya wa CHADEMA ili aweze kuijenga CHADEMA ipasavyo toka ngazi ya chini kabisa. Pia hii itakuwa ni heshima kubwa kwa Dr. Slaa kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa katika kukikuza chama chao na hatimaye kufika hapa walipofika. Mchango wa Dr. Slaa katika uchaguzi wa mwaka huu hautasahaulika kamwe na utaingia katika historia ya nchi hii.

nani anakazi kubwa katika kujenga chama kati ya mwenyekiti na katibu mkuu?
akiwa katibu mkuu anazuiwa na nini kujenga chama?
 
kwani heshima ni kuwa Mwenyekiti, au unataka tuwe kama ccm. wanashindwa hata kumuajibisha hata mwanyekiti wao kwakuwa pia ndiye mwenye dola(RAIS).
 
Kama unaona unakereka hapa JF si uondoke tu kwa amani??
 
siitoi wala nini??
mimi dam dam yan nataman tungekua tunaweka open profile ze2 msingenitukana

Mimi nadhani huu si wakati muafaka wa kujadili vyeo bali ni wakati wa kuchapa kazi. Kama Dr. Slaa angetaka uenyekiti alikuwa na nafasi ya kugombea lkn hakufanya hivyo. Jamaa hawa wanaelewa kwamba kijengacho si cheo bali dhamira. Zaidi ya hayo, Ukatibu ni nafasi nyeti na ukitaka kujua unyeti wake angalia upeo wa Makamba na matokeo yake ndani ya CCM. Hoi!!! Mtoa hoja kateleza
 
Mbona mnamshambulia pass jamani wakati yeye katoa tu maoni yake na sii amri! inafaa kumrekebisha tu kwamba hyo haitafaa kwa sbb hii na hii na c maneno ya kukashiff hii cyo ze utamu jamani:A S angry:
 
Sidhani kuwa ni lazima awe M/kiti ndo ajenge. kaza buti twende!

Ila wewe nina wasiwasi ni mmoja wa waliotumwa kuvuruga chama. Chadema wanaoutaratibu wao. Slaa bado katibu Mkuu, Mbowe mwenyekiti waacheni tu, tuangalie kazi tu.

Mhhh... Usishangae ukasikia njemba ni wa kabila ile ya Mbowe na hataki homeboy achomolewe hapo alipo! Ndiyo mikwara mingi ya kuchafua mtoa hoja!
 
Mi naona huo ushauri mpelekee Babu madevu wa upande wa pili wa nchi,labda utawafaa zaidi
 
kama nafuniwa sawa.ila ushauri huu hauna dira kama kinyesi cha uharo kipitapo ktk 'anas'
 
Napendekeza Mwenyekiti Mbowe ajiuzulu uwenyekiti wa chama ili kutoa nafasi kwa Dr. W Slaa kuwa Mwenyekiti mpya wa CHADEMA ili aweze kuijenga CHADEMA ipasavyo toka ngazi ya chini kabisa. Pia hii itakuwa ni heshima kubwa kwa Dr. Slaa kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa katika kukikuza chama chao na hatimaye kufika hapa walipofika. Mchango wa Dr. Slaa katika uchaguzi wa mwaka huu hautasahaulika kamwe na utaingia katika historia ya nchi hii.

Mimi najua wewe si kwamba unaitakia mema Chadema, ila umetumwa kwa sababu unajua Dr. Slaa anapendwa na watu ndio maana wanakupongeza baadhi. Issue hapa ni kwa nini wewe ndo useme kwani wewe ni nani, una nia gani Chadema,Je hayo ni mawazo yako au umetumwa? je Mbowe na Dr. Slaa kuna tofauti gani? wewe unafikiri dr. Slaa ni mpenda vyeo kama hao wengine wanaokutuma au unajipendekeza tu, Ulishawahi kumwona Dr. Slaa anagombania uongozi au pale anapoona anahitajika. Acha umasikini wa akili.
 
Mbowe, ushauri wangu bado uko palepale. Ni muhimu sana ukajiuzulu umwenyekiti wa chama.
 
Napendekeza Mwenyekiti Mbowe ajiuzulu uwenyekiti wa chama ili kutoa nafasi kwa Dr. W Slaa kuwa Mwenyekiti mpya wa CHADEMA ili aweze kuijenga CHADEMA ipasavyo toka ngazi ya chini kabisa. Pia hii itakuwa ni heshima kubwa kwa Dr. Slaa kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa katika kukikuza chama chao na hatimaye kufika hapa walipofika. Mchango wa Dr. Slaa katika uchaguzi wa mwaka huu hautasahaulika kamwe na utaingia katika historia ya nchi hii.

Mchango gani?
 
kwanza ni vema ukajua chama hakijengwi na mtu mmoja. Pili ktk uongozi katibu ndio mtendaji mkuu. Tatu kila chama kina utaratibu wake wa kupata uongozi. Mwisho, JF sio mali ya Chadema kwa hiyo fika kinondoni au tawi lililo karibu nawe la Chadema uwafikishie maoni yako!
 
Inabidi tufanye utafiti vizuri wa akili ya badhi ya members hapa.. Hadhani wengine wana mtindio wa ubongo..

Wanaandika pumba sijawahi one.. Hivi kweli tuwafanyeje hawa???
 
Chadema ni taasisi inayojegwa kwa misingi ya uwajibikaji pamoja na madilili yake ikiwa chama ndiyo kilimchagua Mbowe kupitia mkutano mkuu wa chama kuwa mwenyekiti wa chama walijua kabisa akikiongoza CDM Kwakufuata misingi hiyo huku akitekeleza majukumu yake pamoja na mikakati ya chama na si mambo yake au matakwa yake binafsi hi basi ikiwa Kamati kuu, na vingozi wengine wanaona kuwa Mbowe anaonekana anapwaya au hafai basi kupitia taratibu ambazo chama kimejiwekea wanaweza kumuomba awajibike au yeye atapima upepo hivyo anaweza kujiuzulu lakini kwakuwa inaonekana anatimiza majukumu yake kwa sasa hakuna haja ya kufanya hivyo pia lazima ujue kuwa katibu mkuu wa chama nimtendaji mkuu wa chama ananafasi kubwa ya kutumia muda wake na wajibu wake kujenga chama tofauti na mwenyekiti ambaye hutoa miongozo na kuendesha vikakao vya chama lakini sehdmu kubwa hufanywa na watendaji wa chini yake.
 
PAS, nimeshakwambia na ninarudia tena, wewe ni mbomoaji sio mjengaji na huifahamu Chadema, siasa, na wanachadema, wewe ni CCM 100%, na umetumwa kuvuruga kama Mjumbe mmoja alivyosema, heshima kwake.

Hivi kipimo cha M/kiti bora na frequency yake ya kugombea uraisi? Mbowe binafsi namheshimu sana na nikiongozi mwelevu na makini, wakati Dr. Slaa anapitishwa kugombea Uraisi, Mbowe (Mh. Mwenyekiti/Mbunge) alisema Chadema kimefanya utafiti wa kisayansi na kugundua kuwa Dr. Slaa ndie anayehitajika sana na watanzania (ni hii ni kweli sote tumeona), hivyo hakuwa na budi ya kurudi jimboni na kumwaacha Dr. aendelee, na hii ndio demokrasia ya kweli.

Ombi langu kwako wewe PAS
Toa bendera yetu mapema iwezekanavyo.

Onyo zuri, big up. Nami nimshauri rafiki yetu PAS kuwa logo yake inang'aa sana na huwa naifurahia sana lakini ajaribu kufikiri vema anapo post comments zake maana vijana wa chadema wako safi, hawana mawazo mgando kama wa CCM, na ndio maana wengi wamefikiri kuwa yuko huko kwenye chama kilichopoteza dira!

Kizazi cha CDM ni safi, makini na tayari kuifanya Tanzania ing'ae tena kama ambavyo ilitakiwa kuwa. Hawa ndio viongozi bora na wachapakazi wa kuijenga Tanzania mpya ifikapo 2015. Tunajua miaka hii mitano ya sasa itakuwa migumu kwa nchi kama tujioneavyo sasa, tunamuomba Mungu atuvushe salama.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom