Profesa
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 905
- 624
Nimependa sana mijdala inayohusu vyama vilivyogombea upinzani uliojitokeza ni wa juu sana unaoimarisha demokrasia ya nchi yetu, sikufurahia kebehi na matusi ambavyo vlinionyesha udhaifu binafsi wa mgombea na kuzidiwa na hoja. Nilipenda utani na mizaha ya wazi kuhusu sera za kila mmoja wapo. Ninataka kuwakutanisha hawa wagombea wote hapa kwenye hii forum na nimewa-tag. Sikuweza kuwapata wote ila nimewapata wagombea wa vyama vikuu vitatu.
Ila nadhani mjadala huu utakuwa mtamu pale ambapo kila upande mtajadili hoja na ubora bila kutumia matusi na kejeli, hebu tuone tathnimini ya uchaguzi kwa vigezo na data,
1. Elimu zao (Rasmi na zisizo rasmi) zinakidhi haja?
2. Nani anauzoefu katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa (maana lazima viende pamoja)?
3. Vipaumbele vya kila chama katika orodha, je vinaashiria hali halisi ndani ya watu wetu (wote kwa ujumla wao)
4. Alipokuwa Jukwaani:
- aliongea nini? Kina mvuto?
- Kina maana?
- Kinaukweli ndani yake?
- Kama kuna mipango yoyote iliyotajwa inaumuhimu kwetu?
- Ni ya kudumu au geresha tu ili awe madarakani?
-Je ni ahadi zinazolinda madaraka yake kati ya wasio na uelewa au ni mikakati ya kutuendeleza itakayodumu hata akiwa hayupo inayoeleweka na waelewa na wasiowepesi wa kuelewa?
5. Alikuwa mwepesi wa kuongea na wananchi kwa kujiamini au alikimbia wananchi na kuhofia mijadala? Na kama alihofia tunadhani ni nini kinamwogopesha?
7. ALisema nini kuhusu watu masikini na wenye shida, watu wanaohangaika na tabu mbalimbali, makundi yenye mahitaji maalumu? Kuna mpango wowote chama chake na mgombea wake alisisitiza kuhusu watoto (sio elimu maan inajulikana ila kuhusu unyanyasaji na ulinzi, kufikia huduma mbalimbali, watoto wenye mahitaji maalum wa mitaani nk), Wenye ulemavu, Wazee, vijana wasio na ajira na mikakati ya kudumu kupunguza tatizo hilo, akina mama na nafasi yao katika maendeleo,
8. Vipi kuhusu uwazi katika utafutaji, ugawaji na utumiaji wa rasilimali za nchi kuna loltoe limejadiliwa lenye kuleta matumaini ya upatikanaji na utumiaji bora wa rasilimali na wamekuwa na mipango yoyote kuhusu uwazi?
9. Vipi kuhusu ubora wa Elimu? Maana kwa idadi tuko juu, hayo mengine kuna yeyote ametuletea hoja muhimu?
10. Anasema nini kuhusu chama chake na miaka hamsini ijayo? Tanzania gani tuitarajie miaka angalau hamsini kwa sisi tunaopiga kura kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni? [kujua kama anaipenda nchi hii au anaipenda miaka mitano tu ya kukaa madarakani]
9. Vipi kuhusu kujitegemea kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni, maana no vilitufanya tukataka uhuru, bado wanahubiri misaada zaidi au mikakati ya kujikwamua kimisaada kwa ajili ya uchumu imara, (Mwlm Nyerere alisisitiza hili akiongezea vigezo vya kutufanya tuendelee Watu [wenye elimu na ufahamu na busara/ustaarabu], siasa safi zenye kujali maslahi ya wengi, uongozi bora unaowawezesha watu kufikia malengo waliyojiwekea kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.
Basi kama mengi ya maswali hayo na mengine uliyonayo wewe Mtanzania hayakujibiwa, Tuanze leo kujipanga miaka mitano si mingi tunaweza kuleta mabadiliko makubwa ndani ya vyama vyetu na au kwa nchi hii kupitia demokrasia.