Elections 2010 Mh. Dr. Slaa, CHADEMA sasa kumekucha!

Oct 22, 2010
78
0
Tarehe 31 October 2010 ilikuwa ni siku ya muhimu na ya kipekee kwa Tanzania na nchi washiriki. Ni siku ambayo watanzania tuliisubili kwa muda mrefu na hatimaye ikafika na sasa imepita. Ni siku ambayo watanzania tuliowachache (tunaoujua wajibu wetu kwa nchi) tulijitokeza kupiga kura kufanya maamuzi mazito yanayolihusu taifa letu lenye umri mkubwa lakini lisilokuwa! Watanzania wengi, kutokana na matatizo mbalimbali yanayoikabili nchi yetu ambayo japo yanaweza kuondolewa, utawala wa CCM ambao umekuwa madarakani kwa muda mrefu umeshindwa kuyaonda, hatukuwa tayari kuurudisha utawala wa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu wa Tanzania 2010.

Naamini kila mpenda mabadiliko anashangaa kwa kinachoendelea kutangazwa na tume ya uchaguzi Tanzania ambayo kutokana na utendaji wake wa kuipendelea CCM umetuthibitishia kuwa si huru wala haitendi haki. Kutokana na mazingira yaliyopo hivi sasa, inawezekana kabisa kuwa litakuwa suala gumu kwa tume kukubali makosa yake na kutenda haki kwa kurudisha ushindi kwa mshindi halali Mh. Dr. Slaa. Siombei, lakini kama hali itakuwa hivyo, Mh. Dr. Slaa, CHADEMA, wana CHADEMA na watanzania wote kwa ujumla hatuna haja ya kukata tamaa. Sasa kumekucha! Tuhakikishe tunajiandaa kwa kila namna kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Tumeyaona makosa na madhaifu ya 2010, tujipange kuyasahihisha 2015. Tumezijua mbinu chafu za CCM na serikali yake, tujipange kuanzia sasa kupambana nazo 2015. Tumejua kwamba NEC si huru, tudai haki yetu ya kuvunjwa kwa NEC ya sasa na kuundwa NEC ya kitaifa itakayovitazama vyama vyote vya siasa katika hali ya usawa. Vilevile tudai haki yetu ya kupewa elimu ya uraia nchi nzima.

Mapambano haya yaanze sasa! Lakini pia tudai haki yetu kwa njia ya amani kwa uonevu wote tuliofanyiwa 2010. Wapo wengi wanaochekelea bila aibu ushindi fake wa CCM, watu hawa ni wabinafsi na hawafai hata kidogo kuwepo katika jamii yetu. Hawa wanafurahia maovu ya CCM, wanafurahia ukosefu wa huduma muhimu kama za elimu na afya, wanafurahia ufisadi, wanafurahia na huduma mbovu zinazotolewa na mashirika na ofisi mbali mbali za umma pasipokujua! Ni watu wapumbavu wasiojua lolote! Nawaomba watanzania wapenda mabadiliko chanya kutokata tamaa. Tulishirikiane kwa nguvu zote kupambana na majambazi haya yaliyovamia nchi yetu na kutumia mali za umma kwa manufaa yao. Roma haikujengwa siku moja! Nyerere hakuipatia uhuru Tanzania ndani ya siku moja ipo siku tutashinda! Long live CHADEMA, long live Mh. Dr. Slaa, long live wanachadema. Mungu ibariki Tanzania.
 
zubeda,ivuga, bull... hivi mnakurupuka au mmetumwa???
:nono::nono::nono::nono::nono:
 
Amina!!!
 
Invisible, Naona ufute na topic nzima kabisa, Sioni sababu ya kufuta comments zote hizo....Au ndio una hasira ya kushindwa kwa Slaa?
 
invisible, naona ufute na topic nzima kabisa, sioni sababu ya kufuta comments zote hizo....au ndio una hasira ya kushindwa kwa slaa?
kama wameandika upumbavu uachwe tu na wewe ni mmoja wao nn......utafikiri watu sio watanzania jinsi wananyopinga?
 
The topic is good and people need to be civilised. Basi. Actually the end of this election (with all the erros and mistakes done by NEC) is the beginning of the 2015 election process.

Cheers for a good thread
 
Back
Top Bottom