MLA PANYA SWANGA
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 5,159
- 5,399
Kauli ya Mheshimiwa bungeni kuwa bei iliyopanda ya mahindi ni faida kwa wakulima hakika si kweli na uwazi kuwa hujui tabu za wakulima.
Mahindi huanza kuvunwa mwezi wa 4 hadi wa 7 na ndiyo miezi ambayo wakulima huhitaji mazao yao yanunuliwe na serikali au na wafanyabiashara kwa bei nzuri ili waweze kulipa ada na mahitaji mengine.
Kwa bahati mbaya, serikali hainunui bali huwaachia wafanyabiashara wanaonunua kwa bei ya kunyonga na wakati huu wakulima maghala yamekauka wananunua mahindi waliyouza mteremko kwa walanguzi.
Leo Waziri anasema mkulima anafaidika wakati sio kweli, anayefaidika ni mfanyabiashara kwa sasa. Waziri usipende kupata sifa za uongo wakati serikali kuhusu kilimo ilishachemka.
Mahindi yote yanayouzwa bei ghali yanatoka katika maghala ya wafanyabiashara na sio wakulima.
Waziri rudi ukajiridhishe sioni mipango mizuri ya kumuokoa mkulima zaidi ni propaganda tu.