Mh. Bashe unawadanganya wakulima

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
5,159
5,398
Kauli ya Mheshimiwa bungeni kuwa bei iliyopanda ya mahindi ni faida kwa wakulima hakika si kweli na uwazi kuwa hujui tabu za wakulima.

Mahindi huanza kuvunwa mwezi wa 4 hadi wa 7 na ndiyo miezi ambayo wakulima huhitaji mazao yao yanunuliwe na serikali au na wafanyabiashara kwa bei nzuri ili waweze kulipa ada na mahitaji mengine.

Kwa bahati mbaya, serikali hainunui bali huwaachia wafanyabiashara wanaonunua kwa bei ya kunyonga na wakati huu wakulima maghala yamekauka wananunua mahindi waliyouza mteremko kwa walanguzi.

Leo Waziri anasema mkulima anafaidika wakati sio kweli, anayefaidika ni mfanyabiashara kwa sasa. Waziri usipende kupata sifa za uongo wakati serikali kuhusu kilimo ilishachemka.

Mahindi yote yanayouzwa bei ghali yanatoka katika maghala ya wafanyabiashara na sio wakulima.

Waziri rudi ukajiridhishe sioni mipango mizuri ya kumuokoa mkulima zaidi ni propaganda tu.
 
Tikiti Sokoni linauzwa sh elf 4 mkulima shamban anauza sh 500. Kama waziri atakua anaangalia bei zilizopo sokon na kusema mkulima ana faidi basi tutegemee hali mbaya kwa wakulima. Wafanyabiashara na madalali watakua wameshangilia sana
 
Ndugu nimeona jambo hili limezungumziwa na id kadhaa humu ikiwa ni katika maada kama hizi, sasa basi katika hali ya kawaida bidhaa yoyote ile itakuwa na thamani kubwa kama ni adimu, wakati wa mavuno mahindi yanakuwa ni mengi sana hivyo lazima sokoni bei iwe ndogo.
Kinachotakiwa wakulima wasiuze kiasi chote wakati wa mavuno ili bei zinapopanda basi nao wafaidike na wapo wanaofanya hivyo na wanafanikiwa.
Vinginevyo labda serikali iwa-subsidize wakulima kwa kununua kwa bei kubwa wakati wa mavuno. Hili nalo linaathari zake mfano mzuri ni kwenye korosho na watu wakaanza kulalamika kuwa serikali imeingilia soko na inapaswa kuacha nguvu ya soko iamue.
 
Tikiti Sokoni linauzwa sh elf 4 mkulima shamban anauza sh 500. Kama waziri atakua anaangalia bei zilizopo sokon na kusema mkulima ana faidi basi tutegemee hali mbaya kwa wakulima. Wafanyabiashara na madalali watakua wameshangilia sana
Huo ndo ukweli na nilimaanisha hicho.
 
Bashe ni mpiga kelele tu kama wapiga domo wengine hawezi kuwa na mpango wa kuwakomboa wakulima.
Hajawahi kuwa na uwezo huo na haitatokea akawa nao.
Kauli ya Mheshimiwa bungeni kuwa bei iliyopanda ya mahindi ni faida kwa wakulima hakika si kweli na uwazi kuwa hujui tabu za wakulima.

Mahindi huanza kuvunwa mwezi wa 4 hadi wa 7 na ndiyo miezi ambayo wakulima huhitaji mazao yao yanunuliwe na serikali au na wafanyabiashara kwa bei nzuri ili waweze kulipa ada na mahitaji mengine.

Kwa bahati mbaya, serikali hainunui bali huwaachia wafanyabiashara wanaonunua kwa bei ya kunyonga na wakati huu wakulima maghala yamekauka wananunua mahindi waliyouza mteremko kwa walanguzi.

Leo Waziri anasema mkulima anafaidika wakati sio kweli, anayefaidika ni mfanyabiashara kwa sasa. Waziri usipende kupata sifa za uongo wakati serikali kuhusu kilimo ilishachemka.

Mahindi yote yanayouzwa bei ghali yanatoka katika maghala ya wafanyabiashara na sio wakulima.

Waziri rudi ukajiridhishe sioni mipango mizuri ya kumuokoa mkulima zaidi ni propaganda tu.
 
Anatangaza bei ya mahindi wakati mahindi tumevuna tangu mwezi Wa Tano? Tumewauzia wafanya biashara huko mjini, leo hii bei inauzwa Mara nne ya tuliyouza...
Halafu waziri anasema wakulima tunafaidika,
Hivi katembelea huku mashambani au analima kwenye magodown?
 
Bashe anakuwaje naibu waziri wa kilimo halafu hajui misimu ya mazao kama mahindi ambalo ni moja ya mazao makuu ya chakula nchi hii? Hapo hapo anaigiza hafahamu kwamba kuna kangomba karibu kwenye kila zao nchini? Then hiyo nafasi haiwezi maana yuko out of touch na wakulima na kilimo chenyewe in general.
 
Bila mkulima kujitoa na kuanza kulima kihiashara na kutafuta taarifa sahihi kuhusu masoko basi siku zote wakulima wataendele kulialia bila msaada na watabaki maskini.
Anayefaidi ni mtu mwenye akili kubwa , mwenye uwezo wa kuongeza thamani kwenye bidhaa yake na akaitangaza.
Sasa mkulima anavuna kisha anahifadhi mazao ndani anasubiri dalali aje ampangie bei lini atapata faida.

Waakati mwngine njaa ya mkulima inamfanya auze kwa bei mbaya sana.
Ukimsubiri waziri au serikali ikusaidie kwakweli mkulima utakufa maskini.
 
Kabla hajakaribishwa mezani Bashe
1573791812067.jpeg
 
mwanao bashe amesema tuu ila wanaoneemeka ni walanguzi maana mkulima akipatwa na njaa, ada na mahitaji mwngine ya shule anauzia hata shambani
 
Mleta mada bado upo mbali sana. Mahindi siku hizi yanavunwa mara 4 kwa mwaka. Anza kulima kisasa ufaidike, achana na mazoea.
Uko sahihi lakini huo ukulima wa kisasa una maandalizi yake haufanywi kiholela bila miundombinu ya gharama.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom