Mh. Amani Abeid Karume Rais Mstaafu Zanzibar mbona sikuoni kwenye hafla mzee wangu?

Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
7,905
13,360
Shikamo Mzee,

Mzee wangu Mh. Karume mbona sikuoni kabisa kwenye hafla za kitaifa au hata matukio makubwa makubwa yanayotokea katika taifa.

Juzi Mh. Mkapa mzee wetu kazindua kitabu sijakuona Mzee wangu ila siyo juzi tu yapo matukio mengine pia sijakuona hata kwenye picha za viongozi wetu wakifurahi pamoja sikuoni mzee wangu kulikoni!?.

Nikutakie heri na mapumziko mema baada ya kipindi kigumu cha uongozi na siasa, ila usiadimike hivi mzee wangu.

Wasalimu.
 
Majukumu ndugu yangu, nikipata wasaa panapo majaaliwa nitakuwa nahudhuria.
 
Dah kuna kitu kinafikirisha hapa mkuu ni eidha mzee umri umesonga sana au ni ishu ya afya ama mzee ameamua kupumzika kweli kweli hataki mbilinge mbilinge tena mana sina imani kua eti wanampotezea hapana sio rahisi kiasi hicho
 
Hapa pangu anakunywa whisky tu,ardhi yote alioichukua kimabavu inarudi serikalini kimya kimya
 
Dah kuna kitu kinafikirisha hapa mkuu ni eidha mzee umri umesonga sana au ni ishu ya afya ama mzee ameamua kupumzika kweli kweli hataki mbilinge mbilinge tena mana sina imani kua eti wanampotezea hapana sio rahisi kiasi hicho
Kwa umri, hilo ninalikataa. Umri wa miaka 60 hauwezi kuzuia mtu kutembea na kuhudhuria matukio.

Tusemeje kwa rtd Mwinyi mwenye 90+, lakini 'yupoyupo sana'?
 
Back
Top Bottom