Mh Aesh Khalfan Hilaly anasaka cheti milembe kumuokoa Patrick Maufi

Mwamakula

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
1,890
382
Taarifa za uhakika kutoka sumbuwanga mjini zinaonyesha kuwa ccm mkoa wamekaa kikao cha siri na kupanga njama za kumutoa katibu mwenezi bw patrick maufi ambaye ameswekwa rumande mpaka sasa kwa kosa la mauaji ya mke wake.

Mwezi uliopita patrick maufi alimubamiza mkewe kwenye ukuta na kumuua kwa kosa wivu wa mapenzi.
Mipango imesukwa na ccm mkoa inayosimamiwa na mbunge wa sumbuwanga mjini mh aeshi.
Aeshe anatajwa kuwango kamati ya siasa wilaya ikiongozwa na patrick maufi na kupitisha jina la aeshi kwenye kinyang'anyilo cha ubunge huku akiwa na tuhuma za kumupa mwanafunzi mimba na kumulawiti mhindi.

Ccm imepanga makundi mawili moja lina kwenda muhimbili na lingine linakwenda milembe , wote wakilenga kutafuta cheti cha kufiji ili kuonyesha kuwa patrick maufi aliwahi kuugua kichaa na wanapanga kughushi cheti cha matibabu ya clinic kuonyesha trend za matibabu ili wazitumie kumutoa mtuhumiwa mahakamani.

Mda si mrefu ccm wapo mbioni kuwasilisha hoja ya ukichaa ili kumutoa na tuhuma hizo kwa kuwa kesi hiyo inachafua ccm
 
Huyu si yule ambaye alitamba baada ya uchaguzi kwamba amezika msalaba!!!!???? au labda masikio yangu hayaoni vizuri, hebu endeleeni kutujuza ili tujue kinachoendelea.
 
Dah huyu jamaa kamua dadangu jamani tena alikuwa mpole sana huyu dada. kisa miwivu ya kijinga tu.
 
viongozi cdm mpo?
mmelipata hili? karata nzuri sana hii, najua network yetu ni pana pls data isipotee hata moja tuwapate ksama panya mtegoni
 
kama ni kweli wanataka kufanya hivyo on the other side swali litakuja aliwezaje kuaminiwa kushika post hiyo ilhali walifahamu ni mwendawazimu, will be another proof ya magumashi za ccm. lets wait and see
 
Poosuta! Naifahamu S'wanga. Niliwahi kuishi pale. Mji ule na vitongoji vya karibu ni wako juu sana kwa elimu ya uraia na pia hawayumbishwi - licha ya ukarimu na upole wao. Sasa sielewi huyu mbunge walimuokota wapi? Ni mhuni wa kiwango cha kutisha!
 
Sasa kama hilo jamaa lilikuwa jehu mitaani lilikuwa linangoja nini,si angekuwa teyar milembe?mambo mengne hawa sisiem watumie brain
 
Poosuta! Naifahamu S'wanga. Niliwahi kuishi pale. Mji ule na vitongoji vya karibu ni wako juu sana kwa elimu ya uraia na pia hawayumbishwi - licha ya ukarimu na upole wao. Sasa sielewi huyu mbunge walimuokota wapi? Ni mhuni wa kiwango cha kutisha!
Inasemekana walichakachua..
 
Umbumbumbu wa viongozi wa ccm ndio huu basi yani wao wanafanya lile wanaloona linawafaa lakn sio kutizama side effects,ngoja tuone itakuaje.
 
Itakuwa kichekesho kingine cha mwaka! Kama walikuwa na mtendaji mkuu wa chama ambaye ni kichaa bac hapo chama hakuna!
 
yaani hawa jamaa, kufikiri kwao ni kimasaburi saburi, cjui watabadilika lini, bora vichwa vyao vingekuwa na vilusekero.
 
Damu ya huyo dada itamtafuna na kumla hadi immalize yeye na watakaomsaidia,waache maovu jamani du,ni mbaya sana ctaki hata kuwaza,
 
Mambo ya CCM hayo; kulinda wahalifu na kufunga wasio wahalifu!

Hivi; nikifikia conclusion kuwa CCM wote ni wahalifu nitakuwa nimepotoka?
 
With CCM kwa kweli ilo lawezekana
Yaani nimekosa imani nao kabsaaa wanaiendesha nchi kama gari lisilo na dreva
 
Patrick Maufi, muuaji!ndiye aliyemsaidia Aishe kwa udi na uvumbi kuiba kura za CDM mwaka jana na kesi bado ipo mahakama ya rufaa Sumbawanga. Yeye mwenyewe alifoji cheti cha elimu ya sekondari na darasa la saba na akapitishwa na Makamba kuwa mgombea wa CCM dhidi ya wagombea wenzake.

Sasa kama ni kweli anampango huo mwisho wake wa upuuzi wake ndo unakaribia. Ovyo kabisa huyo kijana wa magamba!!!!!!!!!!
 
Sasa naanza kukubaliana na yule Kibajaji mbunge wa Mtera alipoliomba Bunge liwapime akili, nazani huyu jamaa alikuwa najua kabisa ndani ya chama chake si wazima wa akili! hahahaha, ukweli bana hata uufukie vipi ipo siku tu utaibuka, kwa nini wasimpeleke kabisa wodi za vichaa akambane na vichaa wenzake kuliko kufoji vyeti!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom