Mh. Abood (MB), Meya wa Moro na Wasomi vyuo vikuu Moro mlifata nini Kata ya Kihonda? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Abood (MB), Meya wa Moro na Wasomi vyuo vikuu Moro mlifata nini Kata ya Kihonda?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by DT125, May 25, 2012.

 1. D

  DT125 JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 203
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Jana jioni kulikuwa na vituko cha aina yake ktk kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro. Wakazi wa Kihonda walivamiwa na kundi la wanafunzi wa vyuo vikuu vya Mzumbe, SUA, Jordan na Morogoro Muslim walioletwa na Mh Abood na Meya. Mkutano haukuwa na wakazi wa kata ya Kionda zaidi ya wapita njia, muda mwingi walitumia kutambulishana viongozi wa vyuo husika, Mh. Abood alishindwa kuhutumbia na ndani ya chini ya dakika 4 maneno yalikauka akalazimika kukaa. Meya alijisifia kwa kuorodhesha vyeo vyake. Muda wote walishambulia CDM kana kwamba ndicho chama tawala. Ushauri wangu Serikali iboreshe mazingira ya kuwekeza, wajasiriamali kama akina Abood warudi kwenye uwekezaji siasa ni kuwatesa. Na hii itasaidia kuongeza ajira hasa kwa wasomi wetu hawa wanaokimbia masomo vyuoni na kutumiwa na wanasiasa kwa matengemeo ya kujulikana kwa wanasiasa ili wamalizapo masomo waalau waumbulie hata u DC. Jamani nafasi hizo mbona chache mno.
   
 2. M

  Mnyonge Namba1 JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Njaa....njaa...njaa....Kali sana.Kipindi hiki boom limechelewa kuja watu wanaponea pesa za mafisadi.Hawa hujali matumbo yao tu,hawajali jinsi majority wanavyonyonywa na utawala huu dhalimu wa ccm.
   
 3. e

  environmental JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,054
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Mkoa wa morogoro unahitaji mabadiliko makubwa karibuni wabunge wote waliopitia na waliopo wanamiliki makampuni ya mabasi kuazia na Marehemu Gulamali alikuwa anamiliki mabasi ya Sharuks inaonekana wamorogoro wanakuwa naimani sana na watu hawa sasa ni wakati wa kugeuka kuangalia mchango wa watuu wengine
   
 4. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  1. moro wote magamba tu. amkeni.
  2. wanachuo wengi ni njaa tu zinawasumbua
   
 5. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mkuu umesema kweli/ Lakini, kumuka kwamba gulamali alimshinda judge (samahani nimesahu jina). gulamali na his Sharuks (sanifu Lazaro, Mwamba Kizota, e.t.c), aliweza sana kuwasaidia wananchi wa kule ambao walikuwa hawana usafiri. Kumbuka kwamab Gulamali alitengeneza/kukarabati madaraja ya kwenda Jimboni kwake. Sasa Wananchi wanahitaji nini zaidi ya Mbunge anayeweza kuleta maendeleo kwa watu wake? The list is endless (Cleopa Msuya, Mkono, Dewji na wengine)???

  Kuhusu Abood, kila mtu anajua ni kwa nini amekuwa hapo. Kumbuka kwamba Abood alishinda katika kura za maoni mwaka (2000 and 2005) kwa uwezo wake wa kuhonga wapira kura wote. CCM wanalijua hili fika. Abood ni mfanyabiashara mkubwa, anatoa mabasi yake kwenye mazishi ya wakazi wa Moro. Kwa wenyeji hilo ni jambo kubwa sana na utawasikia wanasema KANIZIKIA BABA YANGU! jamnbo ambalo halina tija kwa maendeleo, kwa maana bila hata Abood, baba yako angezikwa tu!!

  Unajua kwa nini Mstahiki Meya wa Morogoro amepata nafasi hiyo? Unajua ni Majungu gani walimpigia Prof Ishengoma asigombee Udiwani na nini walifanya ili Diwani (Prof Urio) asipate umeya na badala yake wakamweka aliyepo sasa?
  Unajua baba wa mstahiki Meya wa Morogoro ni nani?

  Ukipata majibu ya maswali hayo utakuwa umezifahamu siasa za Morogoro.
   
 6. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mwaga majibu ya kwenye bold!!!
   
 7. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Hovyooo
   
 8. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Weka vitu bwana unatuacha hewani ili iweje
   
 9. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huu mkoa nao umelala fofofo
   
 10. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  njaa zitawapeleka kaburini. Moro ni magamba wacheza bao round abt. Prof. Ishengoma alibadilisha mji km mayor ubunge wakampikia majungu.
   
 11. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #11
  May 25, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  Aziz Abood ni mfanyabiashara Mkubwa wa mjini Morogoro ambaye amedominate route ya Dar-Moro. Nani asiyejua Abood Bus Serivce? Aziz alirithi Kampuni hiyo kutoka kwa marehemu Baba yake. Katika vitu alivyorithi, ni pamoja na Dereva aliyependwa sana na baba yake, ambaye sasa mzee huyu ndiye msimamizi wa routes za Dar-Moro. Ukienda kwenye kituo cha mabasi cha Msamvu kwenye mabasi ya abood utamkuta. Mzee huyu ndiye BABA MZAZI WA MSTAHIKI MEYA WA MOROGORO MUNICIPAL. Nadhani hadi hapo sasa unanipata, Meya ni mtoto wa Msimamizi wa mabasi ya Abood, na Mbunge Aziz ni Mmiliki wa Makampuni ya Abood.

  Prof Ishengoma alikuwa Meya wa Moro kati ya 2005-2010, na utendaji wake wa kazi unafahamika kwa kila mkazi. Alikuwa mwiba mchungu kwa madiwani wenzake. Pesa za kuliwa hovyo hivyo, miraji ya kijinga kijinga na utapeli, ilipotea kabisa. Alikuwa kikwazo kikubwa kwenye ulaji. Matokeo yake, baadhi wa madiwani walijitahidi sana kumchafua na kumkwamisha, kwa mfano kukwamisha ujenzi wa daraja moja ambalo limekusudiwa kupunguza msongamano wa magari hapo mjini. Akiwa Meya, Prof Ishengoma alikuwa na mpango madhubuti wa kuvunja soko la sasa, (ambalo ni chafu sana na mvua ikinyesha wakazi wa Moro wanaweza kuwa mashuhuda) na badala yake kujenga soko jipya la ghorofa. Hii ni baada ya kuona kwamba soko la sasa ni dogo na halitoshelezi mahitaji ya wakazi wanaongezeka kila kukicha. Hili halikuwapendeza baadhi ya watu wanaopenda ulaji. Kuna mtu alijua kwamba Moro nayo itakuwa na foleni ya magari?

  wakati wa mchakato kwa uchaguzi wa 2010, wapambe walijipanga na kumshawishi Prof Ishengoma agombee ubunge, badala ya udiwani. walijua fika kwamba huko hatafanikiwa maana atapambana na Abood, ambaye anaweza kuwatembelea kiana wapinga kura wote! Kama ilivyotarajiwa, Abood akaibuka kidedea na kuwa Mbunge.

  baada ya kupata ubunge, kazi ikabaki Moja, kuondoka elemets za wasomi kwenye kinyanganyiro cha Umeya. Ikumbukwe kwamba madiwani walikuwa na kumbu kumbu za jinsi walivyonyimwa ulaji wa peza wa wananchi na Prof Ishengoma. walishaumwa na nyoka, kila wakiona unyasi (msomi) wanashtuka. hapo ndipo ilipofanyika kampeni ya nguvu ya kuwatoa watu kama Prof Urio na Bwana Massawe kwenye nafasi hiyo na kumsafishia njia Meya wa sasa.

  Ndio hali halisi ya Morogoro, na ndio maanaa DT125 anashangaa jana walifuata nini Kihonda. hawana la kuwaambia wananchi, wapo wapoi tu, kulinda maslai na biashara zao.
   
 12. i

  iseesa JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu Okada umeuliza swali halafu ukatuacha njia panda hukulijibu. Tujulishe basi kuwa baba wa mstahki Meya wa Morogoro ni nani ili nasi tumjue kama wewe? Je kujua baba yake ni nani itatusaidia kulikomboa jimbo kutoka kwa MAGAMBA?
   
 13. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #13
  May 25, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135


  Fuata details zangu utamjua tu!
  Mbona nimeweka wazi kila kitu?
  Naomba nisimtaje jina.
   
 14. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #14
  May 25, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Huo ndio mji kasoro Bahari, Yemeni ya Tanganyika.
   
 15. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #15
  May 25, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kweli kabisa.
  Mafuta (petrol na diesel ) bei ndogo kuliko hata Dar.
   
 16. s

  sawabho JF-Expert Member

  #16
  May 25, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
   
 17. s

  sawabho JF-Expert Member

  #17
  May 25, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Sio aina nzuri ya maisha na sio endelevu, bali ni vitu vya msimu. Afadhali bei ingekuwa kubwa kama ya Kigoma, maana siku huyo anayetoa subsidy akiacha kutoa wataona maisha magumu maana wamezoezwa vibaya. Ni vuzuri watu wakaishi maisha yao kuliko kuishi maisha ya mtu/watu wengine.
   
 18. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #18
  May 25, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Unanua kwa nini Sangarara amesema Morogoro ni Kuwait ya Tanganyika?
  Of course hata mimi sio kama nakubaliana na hilo jambo!
   
 19. K

  Kolero JF-Expert Member

  #19
  May 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2010
  Messages: 493
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Morogoro tatizo lao hawajui hata wana matatizo gani na wanahitaji kitu gani kutoa matatizo yao, hakika itachukua muda sana watu wa Morogoro kujitambua, wao ni rahisi mno kudangaanywa kwa vitu vidogo sana, mbaya zaidi hawaoni kama wanahusika na Morogoro hasa mjini, wanajali zaidi wilaya zao nyingine na kuona hapo mjini ni shamba la bibi. Hakika inasikitisha, sijui nani atawakomboa, hata mkihamishia vyuo vyote pale, bado mji utabaki ulivyo, watu watakuja, watasoma, wataondoka. BADILIKENI KWA KUANZA KULITAMBUA TATIZO LENU NA BAADA YA HAPO LIFANYIENI KAZI HILO TATIZO
   
 20. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #20
  May 25, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  majibu utupe wewe tuupate ukweli!mimi nakula kabisa nguruka hapa nasubiria utujuze zaidi
   
Loading...