Mh. Abood (MB), Meya wa Moro na Wasomi vyuo vikuu Moro mlifata nini Kata ya Kihonda?

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
380
573
Jana jioni kulikuwa na vituko cha aina yake ktk kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro. Wakazi wa Kihonda walivamiwa na kundi la wanafunzi wa vyuo vikuu vya Mzumbe, SUA, Jordan na Morogoro Muslim walioletwa na Mh Abood na Meya. Mkutano haukuwa na wakazi wa kata ya Kionda zaidi ya wapita njia, muda mwingi walitumia kutambulishana viongozi wa vyuo husika, Mh. Abood alishindwa kuhutumbia na ndani ya chini ya dakika 4 maneno yalikauka akalazimika kukaa. Meya alijisifia kwa kuorodhesha vyeo vyake. Muda wote walishambulia CDM kana kwamba ndicho chama tawala. Ushauri wangu Serikali iboreshe mazingira ya kuwekeza, wajasiriamali kama akina Abood warudi kwenye uwekezaji siasa ni kuwatesa. Na hii itasaidia kuongeza ajira hasa kwa wasomi wetu hawa wanaokimbia masomo vyuoni na kutumiwa na wanasiasa kwa matengemeo ya kujulikana kwa wanasiasa ili wamalizapo masomo waalau waumbulie hata u DC. Jamani nafasi hizi ni chache mno.
 
Back
Top Bottom