Mgonjwa wa Ukimwi yupo katika stage ya mwisho naombeni ushauri

Status
Not open for further replies.
Dah kwanini Aache dozi sasa? Ubaya ukiacha dozi hali ikawa mbaya so rahisi dawa kufanya kazi tena. Na kila dawa INA stages zake sasa kama alishafika dawa stage ya mwisho. Tumuombee tu .
Inawezekana kama ulivyosema kila dawa ina stage zake huyu naye zilishafika mwisho wa kumsaidia,tatizo mleta mada nae kakimbia wakati kuna waliomshauri vizuri huko juu au sijui ndo yupo kwenye vikao kumpumzisha nduguye!!!

Mtaani vijana wanaziloweka mbichi tu hakuna anayejali wenyewe wanakwambia ukimwi malaria tu hatari cancer na figo.
 
"Note ameshaacha dawa ARV"

Shida iko hapo,,na kama alishaanza na ameacha ndo kabisa anajitafutia balaa arudie tu dozi asogeze siku japo kifo mipango ya Mungu unaweza ukaondoka mwenye afya akabaki mgonjwa.
 
Hawezi kupewa ile ile lazima atabadilishiwa dawa.
Kuna ukweli Mchungu nlitaka kuusema lakini si vizuri..!! Pole sana ndugu yangu lakini USIJARIBU KUACHA DAWA ZA UKIMWI yani hata ukijakuziirudia ulizoiacha unakuta hazifanyi kazi virus washakuwa suguu.. Wengi huwa hawaponiii.
 
Inawezekana kama ulivyosema kila dawa ina stage zake huyu naye zilishafika mwisho wa kumsaidia,tatizo mleta mada nae kakimbia wakati kuna waliomshauri vizuri huko juu au sijui ndo yupo kwenye vikao kumpumzisha nduguye!!!

Mtaani vijana wanaziloweka mbichi tu hakuna anayejali wenyewe wanakwambia ukimwi malaria tu hatari cancer na figo.
Daah ni kweli kabisa mkuu. Wanachukulia kitu simple sana. Aisee kuna watu wanateseka sana na hili gonjwa basi tu mungu ndio anaejua.
 
Alifanya big mistake kuacha dawa lakini pia alitakiwa ahudhurie kila mara kwenye vituo vya care and treatment kwaajili ya ku pewa dawa na kitu kingine kufanyiwa ni determination ya progress ya ugonjwa. Ambapo huchukuliwa CD4, Viral load, Lever function test, Renal function test nk.
Sasa hapo kazi ipo. Arudi CTC atashauriwa nini cha kufanya.
 
Yesu ndio dawa, mshauri na umpeleke kwa Mchungaji ili aokoke mapema
Ni sahihi. Huyo ndugu ampokee Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yake ili aupate uzima wa milele. Maisha haya tunayoishi yana mwisho wake. Mwisho wa maisha haya ni mwanzo wa maisha mengine. Mungu alimuumba mwanadamu aishi milele. Ukiamwamini Yesu unaishi maisha ya amani na furaha milele. Usipowamini Yesu unaishi maisha ya tabu na kuteseka milele. Wakati wa kufanya maamuzi ni sasa.


JESUS IS SAVIOR
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom