Mgonjwa wa pumu ana hali mbaya sana yeyote anayejua tiba yake anisaidie

Inategemea na aina ya mgonjwa !
Salbutamol kwangu mie hata ile pumu ya mwanzo kabisa huwa hainisaidiii ,napona na aminophylline!

Mm salbutamol ni kwa ajili ya zile pumu za ucku km baridi feni vumbi na zinazonibana kwa kupata allergy tu mara moja ila zile ambazo zinakuja na kikohozi cha kukohoa na flue bac kwa cku tatu mfululizo nipate hydrocortisone sindano mbili mbili na nubilizer hapo tena nitafka mwez pumu hazjanibana na zikija zinakuja za kawaida tu nikipata tu salbutamol inhaler bac mambo yanakua safi
 
Jamani jamani nahitaji msaada wenu kuna mgonjwa wa pumu ana hali mbaya sana yeyote anayejua tiba yake tafadhali.

Naombeni msaada.

Pamoja na tiba kwa mgonjwa wa pumu ili kumsaidia kwa kumpatia dawa ya kufungua mapafu. Ni vyema kufahamu kuwa bado mgonjwa anahitaji kufahamu juu ya:
1: Pumu ni nini?
2: Vianzisha pumu mbalimbali
3: Kujua ugonjwa wake uko kwenye kiwango/stage kipi?
4: Dawa gani hutakiwa kutumia katika wakati upi (kutibu vs kuzuia).
5: Kuwa na daftari la kumbukumbu ya mara ngapi hupata dalili ya kifua kutokuwa sawa na matumizi ya dawa zake.
6: Matumizi sahihi ya dawa/dozi
7: Nk....

NB: Matumizi ya Aminophillyne kutibu pumu hayapo kwenye miongozo kwa sasa, hii ni kutokana na shida yake kwenye moyo. Hivyo ni muhimu pia kuchukua tahadhali juu ya hilo.(Haitakiwi kutumika).

Ni muhimu sana kuhakikisha unapata maelezo mahususi hapo juu kwako mgomjwa au ndugu yako. Usipende kutibu kwa mazoea ni rahisi sana pumu kukutenda siku moja. Onana na mhudumu wa afya kwa ushauri zaidi na tiba.
 
mama yangu alikua nao, alienda hospital ya kcmc moshi kuna vikopo akaambiwa yawe mafuta yake alipewa happ hapo hospital na imekua tiba mpaka leo hatoki harara wala upele wala hawashwi sana sana anatumia tetmosal kama sabuni ya kuogea
 
mama yangu alikua nao, alienda hospital ya kcmc moshi kuna vikopo akaambiwa yawe mafuta yake alipewa happ hapo hospital na imekua tiba mpaka leo hatoki harara wala upele wala hawashwi sana sana anatumia tetmosal kama sabuni ya kuogea
Mafuta gani alipewa
 
Back
Top Bottom